Uhuru wetu hautoki kwa Kikwete au Rais yeyote; Rais hawezi kuwa "Dikteta kidogo" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhuru wetu hautoki kwa Kikwete au Rais yeyote; Rais hawezi kuwa "Dikteta kidogo"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 19, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ninaendelea kuonesha makosa ya kimantiki na kifalsafa ya hotuba ya Rais Kikwete jana. Mojawapo ya mambo ambayo aliyadai akikanusha kuwa yeye si Dikteta ni kauli hii ambayo sidhani kama watu waliielewa uzito wake. Rais alidai kitu kingine ambacho nacho pia hana!


  Rais amedai vitu ambavyo vinahitaji kukataliwa mara moja kwa sababu tukivukubali tu tunampa nguvu ambazo hana.

  1. Rais ndiye anayetoa uhuru wa kutembea, vyombo vya habari na hata kuwa (the freedom to be)
  2. Rais ndiye anayetoa uhuru kwa watu, vyama vya siasa tena "mkubwa mno"
  3. Anaweza kuingilia kati uhuru huo kwa kuwa "dikteta" kidogo.

  Ndugu zangu, Uhuru wa Watanzania hautoki kwa Rais - awe Kikwete au yeyote mwingine. Katiba yetu inasema hivi kuhusu uhuru wetu: (Ibara ya 12:1)

  Maneno hayo yanaweza kuonekana ni shallow au hollow lakini ni makubwa sana. Yanatueleza kwamba kila Mtu (mimi, wewe, mtoto, mzee, kijana, msomi, mjinga, kichaa, mwenye akili sana, mlevi, mzinzi hata shoga!) huzaliwa 'HURU NA SAWA'! Kwa maneno mengine uhuru wetu hautokani na rais au chama cha siasa unatokana na kuzaliwa kwetu kama BINADAMU. Ndio maana tunasema "binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa".

  Kwa hiyo, hoja ya kuwa uhuru wetu unatoka kwa rais au kwamba RAis anafikiria kuwa sisi tuko huru kwa sababu kaamua kutugea uhuru haina msingi, ni ya kukataliwa na kwa mara nyingine haina msingi wa Kikatiba (lacks constitutional basis whatoever).

  NI kutoka katika kutambua kuwa sote tunazaliwa huru ndipo Katiba sasa inatambua uhuru huo na kuuhakikisha (the constitution recognizes and guarantee that freedom). Kumbe wananchi wanazaliwa wakiwa huru na kwa kutumia katiba yao wanajihakikishia uhuru huo - Rais hatoi wala kuhakikisha uhuru huo bali anasimamia kuwa uhuru huo hauondolewo - iwe na maadui wa ndani au wa nje - na hii ina maanisha hata na yeye mwenyewe!

  Je ni uhuru gani tunazaliwa nao ambao hauwezi kuondolewa kiholela kama Rais alivyoashiria? Nitataja tu kama Katiba inavyoanisha sasa:

  Uhuru wa kuwa hai (rais hawezi kuja na kumwambia polisi 'mpige huru risasi' halafu mtu akapigwa risasi kwa vile 'rais kasema'). Ili kuhakikisha hili Katiba imeweka wazi kuwa "itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake". Kwa maneno mengine ni kuwa kauli ya Rais anaweza kuwa dikteta kidogo na kuzuia uhuru wawatu haina msingi ni ya kuikataa kwani hana madaraka wala uwezo huo (nililisema hili siku ile aliposema Bungeni kuwa angeweza kuagiza Dr. Slaa akamatwe na akakamatwa)!

  Uhuru wa mawazo na maoni - kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
  kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
  mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
  Kwa maneno mengine ni kuwa hakuna mtu anayeweza kumlazimisha mtu mwingine kufikiri au kuwa na maoni anayoyataka yeye! Kiila mtu anahaki ya kufikiri na kujenga maoni ayapendayo yeye bila kulazimishwa. Hii ina maana kuwa uhuru huu hautoki kwa Rais. Rais hawezi kutuambia kuwa sote tunatakiwa kufikiria hivi au vile na tukifikiri tofauti basi ni makosa!

  Uhuru wa imani
  - Katiba inatambua kuwa kila mtu ana uhuru wa kuamini au kutoamini dini yoyote. Na katiba yetu inaenda mbali zaidi na kusema kuwa mtu anayo haki ya kubadilisha imani yake. Kwa maneno mengine mtoto aliyezaliwa katika familia ya kikristu akiamua kuwa Muislamu serikali au mtu yeyote hawezi kwenda na kumlazimisha abadili. Wanaweza kumshawishi au kumuonesha makosa lakini mwisho wa siku uamuzi ni wake. Na mtu akiamua kutoamini Mungu au akiamini minazi hakuna mtu wa kumlazimisha kuwa abadili imani! Rais hawezi kulazimisha watu waamini vyovyote apendavyo yeye.


  Hiyo ni mifano michache tu. Kwa ufupi ni kuwa kauli ya Rais kuwa yeye ndiye anatoa uhuru na kuwa anaweza kuuondoa uhuru huo wa kuwa "dikteta kidogo" haina msingi. Uhuru wetu hautoki kwa Rais. Period.
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hivi niambieni haikuwa busara kwamba tungerekebisha baadhi ya vifungu vya sasa kwenye katiba tunayoitumia ili kupuguza madaraka yake na kuongeza vipengele vinavyofanya serikali na dola iwe juu ya wananchi ,kwa kweli kulikuwa na maeneo mengi kwenye hotuba yake ambayo yametupa kiulizo ,manake huelewi alikuwa anatueleza kama taifa maamuzi yake au na yeye alikuwa anaendeleza mipasho lakini kwa lugha ya chini
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,558
  Likes Received: 1,903
  Trophy Points: 280
  Ile hotuba ya jana kwa kweli ndiyo maana alienda kuongea na hao "wazee wa Dar" halafu eti kuna wanoadai ni ya kitaifa?

  Zile zilkuwa porojo kwa kiasi kikubwa,kama tu za kwenye ghahawa.

  Inaonyesha wazi kabisa kuwa viongozi walioko madarakani hawafanani na sisi hata kidogo.

  Sometime huwa najiuliza,hivi iilkuwaje hawa ndiyo wanatutawala?
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,812
  Trophy Points: 280
  Mkuu jmushi1, mie nilitabiri hapa jana kabla hata msanii hajazungumza baada ya kufuatilia hotuba zake za nyuma kwamba hakutakuwa na lolote la maana katika hotuba hiyo zaidi ya blah blah ambazo hazina kichwa wala miguu. Na utabiri wangu ukawa kweli. Yaani unasikia hata uvivu kumsikiliza akiendeleza usanii wake halafu huku wakithubutu kuita Serikali yake eti ni "Serikali Sikivu" Sijui ni lini walianza kuwa wasikivu.
   
 5. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,451
  Trophy Points: 280
  Asante tena MM, endelea na kazi nzuri Mh.

  Nakiri mi wala sikuwa na muda wala utashi wa kumsikliza. Eti hivi huyu jamaa kweli ni Rais?

  Nampinga Kikwete na kupinga kwa nguvu zote maneno uliyonukuu hapo juu. Samahani wadau inabidi niwe makini hapa, it's too provocative.
   
 6. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nilijiluliza swali hilo hilo, hotuba hii ni nani kaiandika? Ok forget 'bout it, kwa nini amekubali kuisoma? Au ali edit?
   
 7. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu MMJ jamaa alikurupuka hat speech ilikuwa ya kukurupuka jambo la kujiuliza Je! ilikuwa ni hotuba yake ya mwisho wa mwezi? kama ndio, Je? ya Mwezi October na sept alitoa? kama Ndio, Je? ilikidhi misingi ya kuwa na hotuba ya kila mwezi? kama ndio, Je taifa linakabiliwa na mambo mawili tu 1. uchumi 2. katiba kama ndio, Je? mambo yaliyotokea punde kabla ya hotuba yake hayakuwa na maana kwa wazee ( wanachama wa CCM) kama issue ya MBEYA, ARUSHA na TABORA? kama ndio kwa nini hotuba zote za mwiza wa mwezi huwa anaongelea mambo yaliojiri ama yatayojili punde? kama ndiyo. vipi siku ile anaongea nao (wazee) na kusema hahitaji kura za wafanyakazi? ALIKURUPUKA
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,555
  Likes Received: 18,245
  Trophy Points: 280
  Wanabodi, Aliyoyazungumza jana ni ya kwake na ndiyo yanayotoka moyoni mwake, haya ni mambo ya I.Q, kwa waliomsikiliza in between the lines, wanaelewa nazungumzia nini!. Ndio maana kuna wengine wanafanya Ph.D na kui earn na wengine wanasubiri za kupewa, na kupigiwa tarumbeta za shangwe na mapambio, Dr fulani, mpaka kwenye taarifa za habari amepewa title hiyo ya Dr!.Kwa hili la kuitwa Dr silaumu kwa sababu sheria yetu inaruhusu, ndio maana tuna Dr. Kifimbo, Dr. Nguzukululu Jilala (RIP) na , maprofessor kibao, akiwemo Prof. Maji Marefu etc, lakini mtu unapotunukiwa doctorate ya heshima, angalau, ufananie kwa maneno na matendo!.Nimeambiwa UDSM enzi zile, wate wanaongia walikuwa lazima wagraduate, kulikuwa hakuna DISCO, hivyo vilaza wote walikuwa wakipoozwa kwa PASS ya GPA ya 2.0! ili angalauwatoke, na haya ndiyo matokeo!.
   
 9. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #9
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  tumewazoea kwani kuna siku mliwahi kusifu hotuba
   
 10. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  yote anayoongea Mbowe ni sahihi lakini yote anayoongea Jk sio sahihi
   
 11. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #11
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kwa kweli nyinyi wafusi wa Rais aliyeshindwa uchuguzi wa mwaka jana mnaota ndoto mbaya mkithani maneno yenu dhidi ya mtu binafsi yatatuondoa hapa tulipo na kusonga mbele.
   
 12. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #12
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  watanzania tulipoacha kujenga hoja na kutumbukia kwenye mijadala ya kuwalenga watu ndio tukaanza kukwama kusonga mbele. Hali hii imetuathiri hadi kwenye mijadala ya kimataifa kwani hatuna kawaida ya kuongelea issue tunaongelea watu. muda mwingi tunautumia na kupoteza katika kukosoa
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 415,867
  Trophy Points: 280
  hii hotuba ya jk imemtia aibu sana................pale anaposema ya kuwa hata muundo wa muungano, bunge na mihimili mingine hatuwezi kujadili kama huo siyo udikteta nini?
   
 14. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #14
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Rais hafanyi kazi peke yake kwa hiyo kumlenga yeye binafsi muda unapotea sana. tungejikosoa na kusahihisha makosa yetu wote kwa mtu mmoja mmoja pengine tungepunguza athari za mtu tunayedhani katufikisha hapa tulipo lakini tunalala kwa kuhesabu makosa ya JK na kuchambua kwa kina. Muda huo huo tungeutumia kuchambua kwa kina sehemu yetu ya kazi makosa anayofanya JK kama kweli yapo yasingekuwa na impact kubwa kwetu lakini nasisi tumejiingiza kwenye makosa hayo hayo ya kushinda kutwa tukisutana kwa miaka 4 ijayo ya utaokuwa uongozi wa JK
   
 15. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #15
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mzee wa dar Pipijojo najua ulikuwepo Please angalia my signature! hivi alikuwa amejipanga? mbona kipindi hiki atakuwa anakurupuka kila mara... kwa mwendo huu tutamsifia 1+1=5 ama kweli alikuwa anaongea na wazee wa bagamoyo. full waganga
   
 16. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #16
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Kikwete ameshindwa kazi! Anafikia kiwango sasa anaanza kutisha watanzania kwa kofia yake ya Urais.Akumbuke kuwa ana miaka minne tu atakuwa Raia wa kawaida kama walivyo wengine....Awe makini,Dunia sasa inabadilika yaliyomkuta Aroyo yasije yakamkuta nae!
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Nov 19, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Huwezi kuwa kilaza ukawa rais wa nchi yeyote Duniani

  Lazima uwe na uwezo wa ku-manuva na kufanya kile ambacho wengine hawakiwezi..(IQ)

  Tatizo lako unafikiri IQ ni kufaulu kwa A darasani tu....far from it..

  Kwa hiyo hoja yako ni muflis na wanaofikiri kama wewe nao ni muflis..

  "soma kitabu cha Tony Blair the Journey" gordon brown alikuwa na IQ kubwa sana kupita tony lakini U-PM ulimshinda sana..

  huu upupu ulioandika hapa unakupunguzia heshima
   
 18. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #18
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wakati mwingine ananipashida najiuliza alikuwa anawaza nini mpaka kutamka hayo,lakini ukiludi nyuma ukajiuliza YAMEKWISHA TOKEA NA HAKUNA JINSI NDIO HIVYO TUNATATIZO LA KITAIFA NA WENGI NDIO HAO,TULIONAO HUKO JUU.

  Manake wakati mwingine tuwalaumu wanasaikolojia na madaktari wetu kwa kuwa wahoga na waficha ukweli kuwa tunatatizo la msingi ambalo lilihitaji msaada wao kuweka mambo sawa na kutoa mbinu za kuepuka haya.
   
 19. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #19
  Nov 19, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Uhuru wa uhuru wa maoni unatokana na katiba lakini Rais dikteta anaweza ku-tamper na katiba na kuwaondolea watu uhuru wao, ndicho alichokuwa anamaanisha JK. Alikuwa na pointi katika hilo na wala hujamkosoa chochote hapo. Kwani wewe MMM unataka kusema nchi zenye madikteta hazina katiba nzuri? Usitake kukosoa kitu kisichokosolewa hapo ila badala yake mwambie Mbowe ajibu kwanini alimsifia JK bungeni halafu baadaye anaanza kumgeuka kuwa hana haki ya kuunda tume ya katiba.
   
 20. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #20
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  nimejaribu kutafuta furaha kwa njia ya kukosoa wengine bado sijapata. nimejiuliza mchango wangu kwa taifa langu bado sijaona. njia pekee nimeona niendelee kumwandama JK kwani ndio njia iletayo maendeleo
   
Loading...