Uhuru wa Vyombo vya Habari unavyobinywa na Jeshi la Polisi

Emmanuel R. Ntobi

JF-Expert Member
Sep 23, 2014
691
1,489
Kumekuwa na sintofahamu kuhusu matukio yanayoendelea katika mkoa wa Shinyanga.

Inaelezwa kuwa matukio yanapotokea Kamanda wa Polisi ambaye tangu aje mkoani Shinyanga ameonekana kutokuwa na ushirikiano na vyombo vya habari kuwa kubana kutoa taarifa za matukio kama wanavyofanya makamanda wengine wa polisi mikoa mingine.

RPC wa Shinyanga ambaye amekuwa akitaka kupigiwa simu ili aeleze kuhusu matukio yanayojiri hata anapopigiwa simu na waandishi wa habari amekuwa akionesha kusita kutoa ushirikiano na endapo mwandishi mmoja akibahatika kuongea naye kwa simu, mwandishi mwingine akipiga simu au akienda moja kwa moja ofisini kwake kufuatilia tukio , RPC huyo amekuwa akiwataka waandishi wampigie mwandishi aliyepiga simu kwa mara ya kwanza kwamba hawezi kuzungumzia tukio moja kila wakati kwani ameongea na mwandishi mwingine. Amekuwa akikaririwa akisema ‘Siwezi kuzungumzia tukio moja ambalo tayari nimeshazungumza na mwenzenu aliyepiga simu, mtafuteni awape habari niliyoongea nae’.

Lakini pia wakati mwingine pindi waandishi wanapofuatilia matukio ili waihabarishe jamii RPC huyo amekuwa akiwaeleza waandishi wa habari kuwa hiyo siyo habari.

Kumekuwa na matukio ya ajali,taarifa za vifo vya watu mfano kule Tinde lakini Jeshi la polisi limekuwa kimya tu hali inayoleta sintofahamu katika jamii.

Wananchi wamelamikia vyombo vya habari mkoa wa Shinyanga kwa kuwanyima haki ya taarifa juu ya matukio ya mkoa jambo ambalo linasababishwa na ushirikiano hafifu wa vyombo vya habari na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga.

Madhira haya ya kutotolewa taarifa kwa vyombo vya habari na kuwanyima wananchi haki ya taarifa wa mujibu wa katiba ya nchi si mwenendo mzuri kwa haki ya taarifa kwa mkoa wa Shinyanga na harakati za vyombo vya habari katika kutetea usalama na amani ya mkoa huo.

Tusiamini dhana ya kuwa taarifa za matukio mabaya ndani ya mkoa yanayotolewa na jeshi la polisi ni hali ya kuchafua mkoa husika katika maendeleo bali ni kuijenga jamii kutambua ukweli na kusukuma utendaji wa mfumo wote ya uongozi na wadau ndani ya mkoa kwa ushirikiano na jamii.

Tunamuomba IGP Simon Sirro atusaidie kumweleza RPC wa Shinyanga George Kyando kuhusu umuhimu wa kutoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya matukio yanayoendelea na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya habari kama wanavyofanya makamanda wengine wa mikoa mingine.

Taifa lolote linahitaji habari , ukimya wa habari, mwandishi wa habari ni sawa na kuifunga jamii na mara kwa mara Rais Samia amekuwa akisisitiza kuhusu uhuru wa vyombo vya habari.
 
Shinyanga hamna club/umoja wa waandishi wa habari?

Mngemwandikia barua kutoa malalamiko yenu na kopi kwenda kwa RC, waziri wake, IGP wake, na kwa Rais ingesaidia...
 
Back
Top Bottom