Uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania wakati wa uongozi wa Hayati Magufuli

julianbonfim

New Member
May 4, 2021
4
2
Mimi ni mwanafunzi kutoka Ujerumani naandika tasnifu yangu kuu kuhusu uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania nikizingatia sera ya vyombo vya habari wakati wa Rais Magufuli. Lengo langu ni kufahamu maoni na mjadala kuhusu mada hiyo kwenye JamiiForums.

Umma wa kidijitali unafikiriaje kuhusu sera hii ya vyombo vya habari? Je, inawaathiri vipi watu katika vikao vya mtandaoni?

Labda kuna mtu hapa wa kunisaidia na kushiriki maoni yake au nyuzi muhimu au maneno muhimu ya kuangalia kwenye JamiiForums (Kiingereza na Kiswahili). Asante!
 
Kimsingi vyombo vya habari havikuwa na Uhuru at all. Pitia Sheria ya vyombo vya habari ambayo ofcoz ilipitishwa na Waziri aliyepo sasa hivi bwana Nape ndio aliisimamia.

Pia pitia Sheria ya TCRA kuhusu usimamizi wa vyombo vya habari haswa maudhui ya online TVs angalia sana Sheria ya kulazimisha kuzisajili hizo online TVs pia fees za usajili ambazo zimewekwa exorbitantly as if zile TV ni za starehe wakati zinasaidia jamii ambayo kwa sasa ndio inajizoesha kupata habari kiganjani.

Pitia regulations za Ile Sheria ya Habari zimekaa kipuuzi sana almost Sheria nzima inahinder utoaji na upatikanaji wa habari.

Kuna sheria ya takwimu nayo ilipitishwa na Magufuli nayo ina madudu mengi sana unaweza kupitia na regulation zake.

Ningekuwa nakufahamu ningekufanyia hiyo research aisee Ila pita humo nilipokuelekeza then waweza kugoogle maandiko mbalimbali yaliyohusu kubanwa kwa Uhuru wa Habari yapo mengi sana ya Jenerali Ulimwengu, Kuna matamko ya Baraza la wahariri Tanzania, Kuna Baraza la vyombo vya habari (MCT) nk hao wote walishatolea matamko kuhusu hizo Sheria na mambo kadhaa wa kadha.

Pia Kuna matukio ya waandishi mbalimbali kufungwa jela Kama Joel Kabendera, Kuna waandishi wengi sana walikamatwa wakafunguliwa mashtaka kipindi Cha Magufuli alikuwa hataki serikali yake isemwe au kukosolewa kwa lolote.

Kuna matukio ya mwandishi au waandishi kuuwawa baada tu ya kuonekana wakiripoti taarifa ambazo serikali ya kipindi kile ilikuwa haipendi. Mfano Azory Gwanda mwandishi wa BBC aliuawa katika mazingira ambayo ikionekana anaandaa makala ambayo ilisemekana angeipeleka BBC. Haya yote unaweza kugoogle na unapata habari zake.

Pia jiunge na Mwananchi Online lipia Ile fee ili uweze kuaccess library ya magazeti yote uweze kuweka proper reference.

Nitakutafutia Journals na Periodicals ambazo zimekuwa na makala za hayo mambo pia but you better find a journalist atakupatia kulingana na journals za taaluma yao but pitia LHRC watakuwa wanazo nitajaribu kumcheki Mkurugenzi wao she can be of assistance.

Naweza kuwa na msaada hasa kwenyupande wa sheria coz it's my profession.

I hope nitakuwa nimekupa mwwnga kidogo pa kuanzia.
 
Ansante sana! Hiyo inanisaidia sana. Bila shaka nafahamu sheria na kesi za Kabendera na Gwanda. Anyway nitafuata mapendekezo yako. Lengo langu ni kama nilivyotaja kupata ufahamu kuhusu jinsi watumiaji katika vikao vya kidijitali walivyochukulia sheria na kesi hizi. Asante sana!
 
Andika kijerumani tukuelewe vizuri sisi wengine hatujui sana kiswahili
Ich bin ein Student aus Deutschland und schreibe meine Masterarbeit über Medienfreiheit in Tansania basierend auf der Medienpolitik während Präsident Magufuli. Mein Ziel ist es, die Kommentare und Diskussionen zu diesem Thema in den JamiiForums zu verstehen.

Was denkt die digitale Community über diese Medienpolitik? Wie wirkt es sich auf Menschen in den Online-Foren aus?

Vielleicht gibt es hier jemanden, der mir helfen und seine Gedanken oder wichtige Artikel oder Schlüsselwörter zum Nachschlagen in den JamiiForums (Englisch und Kisuaheli) teilen kann. Dankeschön!
 
Mimi kama mtumiaji wa kawaida wa mitandao ya kijamii kama Jamii Forum, naona sheria hii ina faida na hasara zake mfano wa faida yake ni kuwa uamuzi wa serikali ya Tanzania kutaka watu wenye taaluma ya uandishi wa habari pekee ndio waruhusiwe kujihusisha na utoaji wa habari, na hasara ya hiyo sheria ni kutaka vyombo au chombo cha habari kitoe jina la chanzo cha habari kwa vyombo vya usalama kama polisi n.k ikiwa taarifa aliyotoa ni ya siri kwa ajili ya upelelezi zaidi.

hii haipo sawa, kwa mfano mimi nimetoa taarifa ambayo ni ya siri, wao wanapaswa wafanye uchunguzi kwa namna wanavyojua wao, na sio kunifata mimi moja kwa moja. na ndio maana tunatumia Jamii forum sababu huku kuna uhakika wa kutotolewa kwa taarifa zangu.
 
Back
Top Bottom