Kuna magazeti ya aina mbili. Broadsheet na Tabloid. Magazeti ya broadsheet huwa ni mapana na yana kurasa nyingi. Habari zake huandikwa kwa kina, zinahaririwa na kuthibitishwa uhakika wake. Lugha inayotumika ni fasaha. Wasomaji wa magazeti haya wengi ni wasomi wenye elimu zao.
Waandishi wa magazeti haya wana taaluma ya uandishi wa habari. Muandishi asiyejua tofauti ya R na L hawezi kupata kazi katika magazeti haya.
Kutokana na ubora wake magazeti haya mengi yamejijengea sifa ya kuaminika hasa na vyombo vya serikali. Na yanauzika sana. Kuna mengine hata stori ukiitaka inabidi kuilipia (subscription).
Magazeti ya aina ya pili huitwa Tabloids. Haya huwa ni madogo, habari zake zinaandikwa kwa kifupi na zinaweza zisithibitishwe. Uhariri wake si madhubuti na lugha ya mitaani inaweza kutumika. Mengi ya magazeti haya si ya kutumainiwa.
Gazeti la Broadsheet linaweza kuandika hivi. "Maafisa wa polisi wamekamata madawa ya kulevya" . Habari hiyo hiyo kwenye Tabloid inaweza kuandikwa hivi "Manjagu wamebamba unga".
Pamoja na kelele zote za uhuru wa vyombo vya habari jiji la Washington DC lina magazeti makuu ya kila siku mawili tu ambayo yanachapishwa kwa staili ya Broadsheet. Magazeti hayo ni The Washington Post na The Washington Times.
The Washington Post lilianzishwa mwaka 1877. Ni moja ya magazeti yanayotegemewa kwa nchi nzima yakiwemo New York Times, L.A Times na The Wall Street Journal. Gazeti hili huandika habari za siasa, habari za kimataifa, habari za nyumbani, utamaduni na michezo. Ni maarufu pia kwa matangazo hasa ya nafasi za kazi. Bango la gazeti hili ni "Democracy dies in darkness"
The Washington Times linafanana na Washington Post. Gazeti hili huandika habari mbali mbali haswa za siasa za Marekani. Bango la gazeti hili ni "America's Newspaper".
Zaidi ya hapo kuna matabloid machache ambayo yamejijengea sifa na heshima.
The Express ni gazeti la bure. Liko chini ya Washington post.
The Hill ni gazeti la siasa linachapisha habari za bunge.
The Politico ni gazeti la siasa linachapishwa kuzungumzia bunge, siasa za ndani na nje, vyombo vya habari na habari za uraisi.
The Roll Call ni gazeti linalochapishwa jumatatu mpaka ijumaa wakati bunge likiwa linaendelea.
The Stars and Stripes ni gazeti linalozungumzia mambo ya wanajeshi.
Ukiachana na magazeti hayo utakutana na yanayojulikana kama supermarket tabloids yakiongozwa The National Enquirer. The Star na The Globe. Haya yanajulikana wazi ni ya umbea na uongo. Utayakuta yametundikwa kwenye supermarkets. Wakati unasubiri kwenye mstari ulipe unaweza kusoma umbea fulani na kurudisha gazeti kwenye shelf bila ya kulipa.
Magazeti haya ndio huandika skendo za mastaa, ndio huandika habari zisizothibitishwa kama kashfa zinazotolewa hivi sasa na baadhi ya wasemaji.
Magazeti haya yanaweza kuandika rais ni shoga na yakapuuzwa tu. Habari hiyo hiyo ikiandikwa kwenye Washington Post nchi nzima patakuwa hapatoshi. Habari za magazeti haya hazifiki na kujadiliwa bungeni.
Sasa homework ninayowapa ni hii haya magazeti ya Tanzania mnayaweka katika kundi gani hapo.