Uhuru wa tanzania haukuwepo, haupo, na wala hautakuwepo

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,070
253
Kuna baadhi ya watu hupenda kufanya mambo ili kuwaudhi au kuwakirihi wengine kwa kujifurahisha nafsi zao. Watu hao hufanya kila mbinu kuhakikisha kama mtu wanaemkusudia kumkirihi anakosa haiba na utu katika umuri wa maisha yao yote! Mfano mdogo ni mtu na mke mwenza wake iwapo hawaelewani. Lazima mmoja atapata fatiki tu kutoka kwa mke mwenziwe bila kukumbuka kuwa yule mbughudhi mkubwa ndio honekani matata na kila mtu kuliko yule anaebughudhiwa. Na haya ni mfano wa Serikali ya Jamhuri ya muungano, wenzetu watu wa bara dhidi yetu sisi Wazanzibari.

Wenzetu wa bara kila wanaloliona litatuudhi na kutuumiza sana basi ndio wanalolifanya ili tuonekane vinyago au vikaragosi mbele ya kaumu ya watu. Ni kwa staili hii wakajiongezea mambo tele muhimu katika mambo ya muungano na kutubakisha rakka! Wao wakafurahi na sisi tumebaki tunasononeka kila uchao. Lakini hulka hii ina madhara yake; maana unapokusudia kumlani mwenzio laana zako wewe huja mara tatu kwako na kule ulikokusudia ikabaki moja. Kwanini nikasema yote haya! Kila ninaposoma ‘mablogu’ yetu haya nasikia Uhuru wa Tanzania, uhuru wa Tanzania, mara Liberia, mara Japani alimradi fujo Ulimwengu mzima. Suali langu mimi linakuja hapa! Hivi kuna nchi iitwayo Tanzania katika nchi zilizopigania uhuru au nchi zilizopata Uhuru?

Nionavyo na ndio ukweli badala ya kusema Zanzibar si nchi, Tanzania si nchi inapokuja masuala mazima ya Uhuru. Na nasema hakuna hivyo kwa sababu kama Tanzania ni nchi iliopata Uhuru ilikuwa chini ya Utawala wa nani? Ilipata Uhuru lini?. Maana kwa ufupi kuna masuali ya kitoto mengi ambayo wenzetu wa bara hujifanya wamesoma lakini yanawashinda kujibu. Hivi wakiambiwa Tanzania ni nini watajibu nini? Ni nchi au ni muungano tu wa nchi mbili huru ; Tanganyika na Zanzibar? Hakuna kitu Tanzania hapa katika harakati za nchi zilizopigania au kupata uhuru Afrika. Kuna Tanganyika na Zanzibar ; ambazo kila moja ilipata Uhuru wake siku yake. Uhuru wa Tanganyika ni kila tarehe tisa Disemba(9/12) na ule wa Zanzibar ni tarehe Kumi na mbili Disemba (12/12).

Leo hii wenzetu wa bara huko nje na hata akina mabalozi maskini hualika watu wenye akili zao na kuwaambia leo ni Sherehe za Uhuru wa Tanzania na wakadhani kuwa wale wanaowaambia vile ni wapumbavu na wabole wa kufikiri kama wao wanavyodhani. Nchi zote balaa tupu huko Ulaya, Amerika na kwengineko zogo mtindo mmoja eti Uhuru wa Tanzania. Tanzania ipi hiyo iliyopata Uhuru na lini? Hivi huu si ugonjwa wa kensa ya fikira na mtindimao wa ubongo? Ndio hawa hawa wanaokaa wakasema siku ya Uhuru wa Zanzibar ni Januari 12, 1964, yaani Mapinduzi ndio Uhuru kwao. Ukitazama wanaosema hivi ni wasomi wakubwa ndugu zetu wabara. Wakati kwa watu mbumbumbu tu kina sisi pangu pakavu hatudanganyiki kuwa Mapinduzi ndio Uhuru kwa sababu; kiilivyo Mapinduzi hayatokezei katika nchi iliyochini ya Ukoloni. Unapoung’oa Ukoloni haiitwi Mapinduzi hayo bali ndio Uhuru wenyewe. Na unapoondosha utawala wowote usio wa kikoloni nchi yoyote ile hayo ndio huitwa mapinduzi yawe ya amani au ya kijeshi au mavamizi ya wahuni tu ya akina Okello na Said Washoto.

Hivi kama mapinduzi ndio Uhuru, kweli wale waliopindua wangeweza kumng’oa Mngereza pale kwa yale mapanga na mareki? Tatizo la ndugu zetu wa bara ni kufanya wenzao wapumbavu wa kufikiri ilhali kufanya kwao huko huthibitisha umbumbumbu mkubwa wa akili na fikra zao finyu zilizojazana vichogoni mwao tu na kubakisha sehemu nyengine za kichwa zikiwa tupu. Kwa maana wao wanaona aibu kujivunia Uhuru wa Tanganyika, na ili waoneshe taswira na nia yao mbovu dhidi ya Zanzibar basi hujitangazia kuwa wao ni Watanzania ili Zanzibar izidi kupotea katika ramani ya dunia. Jamani ndugu zetu wa bara msikatae Utambulisho wenu huo ndio utukufu wenu. Mbona Wazanzibari huona fahari zaidi kujitambulishia Uzanzibar wao hapa nchini na hata nje ya nchi lakini nyie kila kitu Mtanzania, auTanzania na sio Tanganyika na Utanganyika. Hakuna kitu hicho ndugu zangu nyinyi ni Watnganyika na jivunieni na musherehekee Uhuru wenu wa Tanganyika na sio Watanzania na jifaharishieni hilo huko Ulaya na Amerika zote kwani hao mnaona munawadanganya wanawacheza shere kwani wanajuwa fikka kuwa Zanzibar ipo na nchi huru na Uhuru wa Tanzania haupo popote katika maandiko ya Kiserikali na kidiplomasia. Sisi Uhuru wenu huo hautuhusu kimsingi na ndio ukaona tunaalikwa tu kwa maana ni nyinyi mliopigana mpaka mkashindwa kumng’oa Mjerumani mkaachiwa nchi tu kwa makubaliano yenu na kanisa katoliki ndio ukaja huo Uhuru. Msituharibie jina maana kwa kufanya hivyo mnadhani mnatuchafua sisi ilhali nyinyi ndio mnaoenkana hamna akili ya kupambanua mambo kwa kushindwa kwenu kufumbua kuwa Tanzania haijawahi kupata Uhuru, wala haitopata uhuru milele maana hakuna mkoloni wala mtu aliekuwa na nchi iitwayo Tanzania tangu mkutano wa 1884-1885 huko Berlin Jerumani chini ya kansela Otto Von Bismark uliojadili kuigawa na kuitawala Afrika Tanzania haikuwemo, na kabla ya Uhuru wa Nchi za Afrika pia haikuwepo nchi iliyoitwa Tanzania. Kuweni na maarifa na mjivunie utambulisho wenu na Uhuru wenu wa Tanganyika. Huo ndio Uungwana na mnapokataa hilo ndio mkasikia kuna watu husema ni Utwana huo maana mkataa asili mtwana tu au mjakazi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom