Uhuru wa Mtanzania wa kuishi na kimaendeleo upo mikononi mwa dola au yeye mwenyewe?

Fasta fasta

JF-Expert Member
Feb 15, 2011
1,126
725
Wanna jamvi?
Nimeuliza maswali mengi sana mpaka nikajikagua Mimi mwenyewe na wenzangu ninavyosikia sauti zao huku mitandaoni kuhusu kufanya Jambo ambalo unataka na wenzako washiriki kwa Nia nzuri lakini dola wanazuia.

Mfano makongamano yanapoandaliwa na kuomba kibali polisi Ina maana yapo ndani ya katiba ya nchi. Haya makongamano yanamadhara gani kwa taifa? Nimachojua yanawapa watu uimara zaidi na kujenga mawazo shirikishi ambayo yanatumika kuendeleza taifa letu.

Wanapoomba kibali inamaana hata hao polisi wamealikwa pale na kulinda usalama wa raia wao. Na yatawasidia polisi na watu wa usalama kuwajua watu na uelewa wao, mambo yaliyopo huko mitaani kwa sababu wanasungumzia maisha yao.

Polisi wasimame upande wa raia ili wafikie ndoto zao kulingana na nipango yao. Ki ukweli watanzania wanataka katiba mpya sio Siri. Dola iwaache wananchi wapeane mawazo yao kwa sababu humo ndani Kama watakuwepo ambao hawataki watajibizana humo ndani na watafikia muafaka na maisha yataendela.

Kuwafunga watu mdomo ndiyo hayo mtu anaishi kwa mashaka na dukuduku shingoni akiogopa dola itamkamata na kumtupa gerezani.

Ukiangalia Hamza wa sallenda unaweza kupata kitu kwake, halafu alikuwa kada wa chama tawala.

Dola itafute mbinu ya KUISHI na serikali kwa kuwashirikisha chama tawala na wapinzani bila ubaguzi. Dola iwe ni kiunganishi kisiwe chombo Cha kubagua.

Angalieni maneno yaliyopo mitaani na mitandaoni ni polisi polisi polisi ni kwa Nini?

Rais ameshaona mbali juu yenu Ina maana kanawa mikono. Hata ikitokea kesi huko ICC yeye atasema niliwaambia.
 
Watanzania tuamke tunaendeshwa kama matoroli tuikatae CCM na mfumo wao mbovu kwa nchi yetu.
 
Samia alishatahadharishwa kuwa akiachia vyama vyote vifanye siasa, CCM kitakufa. Usalama wake kubakia madarakani ni kwa njia ya udikteta unaosimamiwa na polisi na majeshi pekee. Dalili zinaonyesha kuwa amechagua udikteta.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom