Uhuru wa Kutoa Maoni Umeimarisha au Umedhoofisha Umoja na Mshikamano wa Nchi Yetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhuru wa Kutoa Maoni Umeimarisha au Umedhoofisha Umoja na Mshikamano wa Nchi Yetu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, May 31, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  May 31, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa mantiki yake uhuru wa kutoa maoni mzuri japokuwa una mipaka (Rejea Ibara ya 18 ya Katiba ya Nchi)!
  Hata hivyo tumeona matukio kadhaa ambayo, yumkini yamesababishwa na uhuru tulionao, esp kipindi hiki cha JK, ambayo yameidhalilisha Serikali kwa kiasi kikubwa mpaka heshima ya viongozi wetu iko mashakani:
  1. Tulishuhudia nyaraka za siri za Serikali zikizagaa mitandaoni na sehemu nyinginezo.
  2. Tumeshuhudia pia msafara wa Rais ukipigwa mawe.
  3. Tumeshuhudia vile vile viongozi wetu wakizomewa hadharani, jua limewaka kweupe pee!
  4. Tumemshuhudia kiongozi mstaafu Ally Hassan Mwinyi akilambwa kofi hadharani!
  5. Tumeshuhudia malumbano ya Muungano, Zanzibar kuwa nchi au la, yasiyokuwa ya kawaida.
  6. Tumesikia na kushuhudia malumbano ya kidini (Mambo ya Kadhi, OIC, Nyaraka za Kidini Kuelekea Uchaguzi Mkuu, 2010) yakishika kasi kila uchao, hata Bunge Letu Tukufu lilitekwa na jinamizi hili.
  .....nk.
  Kwa bahati mbaya sana viongozi wetu, esp JK hakemei vitendo vyote vinavyosababisha migawanyiko! He is simply passive!
  Hata hivyo kupitia uhuru huo huo wa kutoa maoni tumeshuhudia yafuatayo:
  1. Kashfa nzito zikiibuliwa na kuanikwa hadharani, km Wizi wa Deep Green Finance, Kashfa ya EPA, Mwananchi Gold, nk
  2. Tumeshuhudia mawaziri wakijiuzulu kwa kashfa zilizoibuliwa.
  3. Tumeshuhudia mawaziri wakiwekwa kiti moto Bungeni isivyo kawaida.
  4.
  .....nk.
  Je, Wapendwa wanaJF, kupitia uhuru huo wa kutoa maoni nchi yetu imeimarika na kuwa kitu kimoja zaidi au tumegawanyika na kukosa mshikamano tuliokuwa nao tangu mwanzo? Nchi kama Somalia sasa hivi haikaliki, imegawanyika vibaya sana, sijui kama imesababishwa na uhuru wa kutoa maoni au la, lakini migawanyiko ndiyo iliyoifikisha hapo ilipo!
  Kama mshikamano umepungua, Je, uhuru huo uminywe kidogo? Kwa mwendo huu wa nchi yetu tutafika jamani? Mbona inaonekana kupitia ALAMA ZA NYAKATI kwamba ipo siku tutazichapa? (Mungu apishilie mbali) Naomba tujadili!
   
 2. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2010
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mbona hukuweka lile la kukashifiwa kwa Kiongozi wa nchi na ZAUTAMU (jaraha likioweka kovu hukukumbusha)na imefikaje kesi yao ?
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  May 31, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Niliweka n.k. (na kadhalika) hapo juu, ok?
   
 4. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  May 31, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  BOTH!Isipokuwa Uimarikaji wa democracy and freedom ni zaidi ya udhoofishaji wake,ni sawa na nafaka wakati wa kusaga ni lazima utapoteza baadhi ya unga ama nafaka hizo during the proccess,hata hivyo the overall manufaa can justify it,ie watu watakula nk....the end justifies the means,ama we unaonaje?

  Kumbuka no freedom is for free or for granted,its all got to be earned,ukiona vina elea ujue vimeundwa,kama ni kuzichapa ili tuwe pamoja shida ikwapi?Ama umesahahu wagombanao ndio wapatanao?
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Jun 1, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tatizo la kuzichapa ni "unpredictable results!" Kama tungejua matokeo "in advance" ni afadhali tuzichape ili tuwekane sawa kuliko mambo yalivyo sasa! Wasomali wameendelea kuzichapa tangu 1991 lakini mpaka leo hakuna dalili ya matokeo mazuri!
   
Loading...