Uhuru wa kujieleza: Ni vyema Rais Magufuli akaachia wananchi wafunguke

magis

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
391
590
Habari wapendwa,

Ktk dunia yetu,kumekuwepo na ukuwaji na uwepesi wa upashanaji habari.

Natamani sana Mheshimiwa Rais aruhusu mijadala ktk kila eneo la mjadala.

Mijadala hii iendeshwe kwa kuheshimiana na kwa kuzingatia hoja.

Kwa kuzingatia hayo,litakalosemwa ni vyema likawa la ukweli. Mijadala hii itatufundisha na hivyo kuongeza uelewa na ufanisi.

Rais asichoke kuwaelimisha watu wake kwa kuwa kubaki na mipango yake na kuitekeleza kwa kuelekeza mwenyewe, atatumia muda mwingi na tija itakuwa ndogo.

Nashauri pia kuwa kwa kuwa tutakuwa tunasema cha kweli hakuna haja ya kutumia aka ili kujuana na kukuza mahusiano na mawasiliano.

Iwapo nimekuudhi kwa wazo langu ninaomba unisamehe.
Tujadiliane bila ya kutumia lugha za maudhi.

Nimewasilisha.
 
Wazo zuri sana kwa Mustakabali wa uhuru wa Vyombo vya habari., ingawaje sina hakika kama mwenye Chombo atakubali huo Uhuru..,
 
Kuzungumzia uveterani badala ya kuwarithisha vijana na kuwasaidia kuongoza pia ni tatizo.
 
Baada ya zuio la kwenye bus sasa ni marufuku kuzungumzia siasa popote.
 
Huwezi kuamini, hiyo mijadala kinachochukiwa sio matusi japo ndio kisingizio kirahisi. Kinachoogopwa ni ukweli unaoongewa maana siku hizi unaitwa uchochezi eti kwa kuchochea chuki baina ya wananchi na serekali yao. Kwa mfano sasa hivi umeme unakatika sehemu kubwa ya nchi, yaani kuna mgao wa chinichini unaendelea na hakuna anayethubutu kuhoji hadharani kwani atakuwa analeta uchochezi.
 
Back
Top Bottom