Uhuru wa kuabudu unahitajika kuwekewa mkazo, tupinge ubaguzi na udini

Zumaridi anamakosa kisheria na kesi ipo mahakamani haina haja ya kumjadili.
Suala lolote la kiimani ukilileta kisheria linakuwa kosa.

Mfano wakatoliki jumamosi tunakusanyika majumbani Mwa watu zaidi ya watu 30 je tunahitaji kibali cha kukusanyika.

Ukienda vilingeni kwa waganga utakuta watu wa rika yote wakipata tiba je wanahitaji kibali au mganga nae apewe kesi ya usafirishaji haramu.

Kwa mtazamo wangu ishu ya zumarid ni bifu la police kama kumkomoa fulani hivi baada ya zumarid kuwagomea sababu police hawakufuata taratibu za ukamataji

Thus wamempiga kitu ambacho ni against human right,kwann wampige.

Alipelekewa wito kuripoti police akakataa?

Ishu ya human trafficking Hakuna ground pale labda uzitafute degree za kesi hio kwa torch.
 
Hizo za asili zilishindwa vipi kutusaidia tusichukuliwe utumwani.
Kama zilishindwa kupambana na hizi za kuletewa uoni ya kwamba zilikuwa ni dhaifu.
Ukweli wa Mambo dini ya kweli kwako ni Ile unayoiamini Ila Mungu yeye anajua wakinanan wanafata kile ambacho yeye anataka kifwate ili sisi jukumu letu ni kila mtu kufata lake analoliamini,na kusoma sanaaa ili kuongeza maarifa sababu Kuna watu watahukumiwa au wanahukumiwa mpaka Sasa hapa duniani kwa ujinga wao tu.
 
Suala lolote la kiimani ukilileta kisheria linakuwa kosa.
Mfano wakatoliki jumamosi tunakusanyika majumbani Mwa watu zaidi ya watu 30 je tunahitaji kibali cha kukusanyika.
Ukienda vilingeni kwa waganga utakuta watu wa rika yote wakipata tiba je wanahitaji kibali au mganga nae apewe kesi ya usafirishaji haramu.
Kwa mtazamo wangu ishu ya zumarid ni bifu la police kama kumkomoa fulani hivi baada ya zumarid kuwagomea sababu police hawakufuata taratibu za ukamataji .
Thus wamempiga kitu ambacho ni against human right,kwann wampige.
Alipelekewa wito kuripoti police akakataa?
Ishu ya human trafficking Hakuna ground pale labda uzitafute degree za kesi hio kwa torch.
Mzee kumbuka kila taasisi Ina isajili kisheria yeye alifungiwa kanisa kwa hiyo ukijitafakari kidogo utagundua ni kweli analo shitaka la kujibu.
 
Ukweli wa Mambo dini ya kweli kwako ni Ile unayoiamini Ila Mungu yeye anajua wakinanan wanafata kile ambacho yeye anataka kifwate ili sisi jukumu letu ni kila mtu kufata lake analoliamini,na kusoma sanaaa ili kuongeza maarifa sababu Kuna watu watahukumiwa au wanahukumiwa mpaka Sasa hapa duniani kwa ujinga wao tu.
True.
Pia dini sio mpango wa Mungu bali ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu.Hakuna mahali ambapo Mungu alianzisha dini.
Kuheshimiana na kuvumiliana imani tofauti ndio dini yenyewe.
 
Ngoja Kidogo.., Mimi nina Kampuni yangu ambao the only thing mwisho wa siku ni uzalishaji..., Sasa wewe unataka katika muda wangu wa uzalishaji nikupe muda wa kufanya Ibada ? Kwanini usifanye nyumbani....

Au unachukua kazi ya Ulinzi ambapo katika yale masaa yangu ninayokulipa wewe inabidi uwe macho alafu eti unafumba macho ili usali (je wakiiba) ?

Kwani nilikuajiri uje kutangaza dini au kuniombea au dini ni kwa manufaa yako ?

Kweli haya mambo yanaweza kuleta shida tukichanganya imani za watu na kazi. Ukizingatia Kazi ulizoomba kwenda kufanya zina Katiba yake nayo ni Uzalishaji (uzuri ukiona tatizo unaweza kuacha hio kazi)...,

Nafurahi sana waliowaza na kuona manufaa ya Kwamba Serikali yetu haina Dini..., Na nadhani katika kampuni inayojali faida Dini yake ni Uzalishaji (kwahio kama unazalisha hata kama kimoyo moyo unasali / unswali ) 24/7 who cares...
 
Mzee kumbuka kila taasisi Ina isajili kisheria yeye alifungiwa kanisa kwa hiyo ukijitafakari kidogo utagundua ni kweli analo shitaka la kujibu.
Akisema hakuwa kanisani,bali nyumbani kwake tena ndani ya fence yake bila bughudha ya mtu mwingine je.
Kukusanyika nyumbani ni hadi idadi ya watu wangapi itakuhitaji kibali.
 
True.
Pia dini sio mpango wa Mungu bali ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu.Hakuna mahali ambapo Mungu alianzisha dini.
Kuheshimiana na kuvumiliana imani tofauti ndio dini yenyewe.
Sasa hiyo pia ni fikra yako na Imani yako kwamba dini sijui ni mpango wa binadamu ,lakini mm ninachokazia hapa tuheshimiane na tuvumiliane turudi katika misingi yetu Kama Taifa umoja na upendo ili amani itamalaki
 
Hiko ni kitu ambacho huna ushahidi nacho mkuu,Mimi nadhanj tujikite katika kukemea na kukomesha ubaguzi pasi na kuendeleza ubaguzi wa dini Kama hizi zakwetu zile zimeletwa kila mtu aamini anachoamini alimradi Imani yake haikiuki utu wa mtu mwingine na Sheria zanchi yetu.
Ona huyu
 
Ngoja Kidogo.., Mimi nina Kampuni yangu ambao the only thing mwisho wa siku ni uzalishaji..., Sasa wewe unataka katika muda wangu wa uzalishaji nikupe muda wa kufanya Ibada ? Kwanini usifanye nyumbani....

Au unachukua kazi ya Ulinzi ambapo katika yale masaa yangu ninayokulipa wewe inabidi uwe macho alafu eti unafumba macho ili usali (je wakiiba) ?

Kwani nilikuajiri uje kutangaza dini au kuniombea au dini ni kwa manufaa yako ?

Kweli haya mambo yanaweza kuleta shida tukichanganya imani za watu na kazi ulizoomba kwenda kufanya Hizo kazi zina Katiba yake nayo ni Uzalishaji (uzuri ukiona tatizo unaweza kuacha hio kazi)..., Nafurahi sana waliowaza na kuona manufaa ya Kwamba Serikali yetu haina Dini..., Na nadhani katika kambuni inayojali faida Dini yake ni Uzalishaji (kwahio kama unazalisha hata kama kimoyo moyo unasali / unswali ) 24/7 who cares...

KILA Kazi inataratibu zake kama zinakubana imani yako ni ruksa kuangalia kwingine.
Kwa mfano huu ndo maana waislamu wengi awapo Kazi za kuajiriwa wengi ni wafanyabiashara.
 
Sasa mkuu hapo hoja yako ni nzuri Sana Ila nafikiri kabla ya kuomba kazi Kuna kuwa na taratibu na vipengele vya kazi husika Sasa Kama wewe huna Imani na Mungu na unakataa watu wasiabudu ni bora kumpa mtu taratibu mapema ili ajitathmini,endapo atakubali then baadae akabadilika hilo ni tatzo lingine.Mimi nazungumzia taasisi na sehemu ambazo kimsingi zimejipambanua kuwa Kuna Uhuru wa kuabudu ndipo nyundo yangu inapogonga sio taasisi za kimadhehebu Wala mashirika ya kidini ,Sababu waswahili husema ondoka twende waaganao kila kazi inakanuni zake na Sheria na Kuna hiyari ktk kukubali au kukataa .
 
KILA Kazi inataratibu zake kama zinakubana imani yako ni ruksa kuangalia kwingine.
Kwa mfano huu ndo maana waislamu wengi awapo Kazi za kuajiriwa wengi ni wafanyabiashara.
Aliyekwambia hivyo nan? Hzo takwimu umepata wapi?
Mkuu kumbuka sijizungumzii Mimi tu nimeamua kuwa mfano Mimi cos ni muhanga wa hayo mambo ,but nazungumzia jamii na pengine wapo watu wengi yanawakuta wanashindwa kupaza sauti.
Lengo ni kupata Taifa lenye umoja na upendo ili kuleta amani .
Penye dhuluma Amani haiwezi kusimama
 
Back
Top Bottom