Uhuru wa kuabudu bila kumbughudhi mtu mwingine

No admission

JF-Expert Member
Nov 26, 2011
215
68
Hodi jamvini.

Leo naomba tujadili suala la kuabudu bila kuwabughudi wengine.

Tanzania ni Secular state (haina dini) kama nchi nyingi duniani. Hili ni jambo bora na linatakiwa tulilinde kwenye katiba mpya. Tatizo mimi ninalo lipata ni haya maspika ya Misikitini na mihadhara Makanisani na kwingineko ambayo kwa ujumla yanakuwa hayajali nani ni mlengwa wa ujumbe unao upitisha. Mimi nimeishi nchi nyingi na hata sasa sipo TZ kwa wenzetu kuna utaratibu lakini ukiwa TZ ni balaa. Mfano nimekuwa naishi Mtoni Mtongani ikifika saa kumi kuna mchungaji mmoja anaanza kuhubiri kwenye lod speaker kwa saa zima, anapomalizatu misikiti inaamka mpaka saa 12 asubuhi. Yaani huna kulala kila siku asubuhi kwa hizi kelele (Ujumbe ambao huutaki kwa kawaida ni kelele). Kwanini tusifikie wakati wakusema STOP. we have watch kuna kalenda etc watu wakasali bila kupiga kelele kila kona ya nchi?

Haya ni maoni yangu lakini kweli naona tunatakiwa kubadilika
 
Yes ni jambo zuri..maana mihathara hiyo imekuwa inatukana imani za watu wengine.tushukuru mungu upande unaotukanwa hauna mafundisho ya kulipiza
 
Back
Top Bottom