Uhuru wa kifedha sio uwezo wa kuoanisha mapato na matumizi tu bali ni uhuru mpana wa kufanya kila jambo ambalo ungependelea kufanya bila kukwama

Kaaya10

Member
Dec 11, 2017
37
50
Uhuru wa kifedha ni ule uhuru wa kufanya mambo kama upendavyo au kutekeleza mahitaji yako yote kama upendavyo.

Uhuru wa kifedha sio uwezo wa kuoanisha mapato na matumizi tu bali ni uhuru mpana wa kufanya kila jambo ambalo ungependelea kufanya bila kukwama.

Ili uweze kufikia uhuru wa kifedha lazima ufanye hesabu za kiuchumi na sio zile hesabu za darasani (Hisabati).

Katika kufikia uhuru wa kifedha kumbuka kuna mahitaji ya lazima na yasiyo ya lazima. Tito 3:14 “Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo ya lazima, ili wasiwe hawana matunda.” Lazima uangalie matumizi yapi ni ya lazima na yapi sio ya lazima.

Ili ufikie uhuru wa kifedha lazima ujue maana halisi ya uhuru wa kifedha twende pamoja kwenye mfano halisi.

LUKA 14:28 “Kwa mfano, ni nani kati yenu anayetaka kujenga mnara ambaye haketi kwanza na kuhesabu gharama, ili aone kama ana kiasi cha kutosha kuukamilisha?”

Ukitaka kufanya jambo lifanikiwe lazima ukae na kuhesabu gharama zake;

Namna nzuri ya kuhesabu gharama ni kuangalia matumizi yako halisi kwa mwezi ni kiasi gani na mapato halisi kwa mwezi ni kiasi gani? Ili ujue kama una uwezo wa kutekeleza upangalo

Kumbuka kuandika matumizi halisi na mapato halisi kwa mwezi,

Mfano wa matumizi, kodi ya nyumba, nauli, chakula kazini, matibabu au bima, michango mbalimbali, marejesho, sadaka, usafi nyumbani, chakula nyumbani, mafuta ya gari, matengenezo, ada za shule n.k hapa unatakiwa uandike matumizi halisi, usijidanganye.

Kisha andika mapato yako halisi kwa mwezi mfano, mshahara, marupurupu, kamisheni, riba ya uwekezaji, kodi kutoka kwa wapangaji, kilimo n.k hapa usidanganye kipato kua unapata kingi sana ili hesabu zikubali au zikae vizuri andika uhalisia wako.

Jambo linalofuata baada ya kuandika matumizi yako na mapato ni kulinganisha mapato na matumzi yako, chukua mapato toa matumizi.

Kama matumizi yako ni makubwa kuliko mapato ambapo kwa uzoefu najua ndivyo ilivyo, kama matumizi ni makubwa kuliko mapato jiulize, *Je huo uzidio hua unaupata wapi? Tuseme matumizi yalikua 500,000 na mapato ni 300,000 hiyo 200,000 unatoaga wapi?

Namna unazotumia kujazia ni kati ya njia hizi nne;

---unaishi kwa mikopo

---unakula akiba

---umekosea hesabu, rudia

---unaiba sehemu yako ya kazi

Tafakari kwa kina,, hakikisha unasoma Makala ya pili
 
MIPANGO SIO MATUMIZI

UNASEMA UNA SAVE HELA AKIBA, MARA PAAP UNAPIGIWA SIMU ANKO WAKO KIJIJINI KAMEZA KIJIKO
 
Back
Top Bottom