Uhuru wa Habari: Tuwakumbuke Mashujaa wa Habari waliopo na waliotangulia. Unawakumbuka kwa lipi?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,681
119,317
Leo tunapoandhimisha siku ya uhuru wa habari, naomba chukua fursa hii kutafakari, kwa kuwakumbuka, mashujaa wa tasnia hii ya habari, waliopo na waliotangulia mbele ya haki!.

Je, unamkumbuka nani na kwa lipi?!.

1. Mimi namkumbuka Stan Katabalo, alikuwa mwandishi wa gazeti la Mfanyakazi, aliikomalia kashfa ya Loliondo, ikamtoa uhai!.

2. Daudi Mwangosi, alikuwa Mwandishi wa Channel Ten, akauliwa na bomu la machozi, ili asiripoti mkutano wa Chadema pale Nyololo!

3. Marehemu Adam Mwaibabile "mwana".
Aliwekwa ndani na RC wa zamani wa Ruvuma Nicodemus Banduka kwa kukutwa na nyaraka zenye muhuri wa siri za serikali.

Naomba tuendelee kuwataja, wewe shujaa wako ni nani, au unawakumbuka kina nani, walikuwa wapi na unawakumbuka kwa lipi?!.

Pasco
 
Marehemu Adam Mwaibabile "mwana".
Aliwekwa ndani na RC wa zamani wa Ruvuma Nicodemus Banduka kwa kukutwa na nyaraka zenye muhuri wa siri za serikali.
 
Marehemu Adam Mwaibabile "mwana".
Aliwekwa ndani na RC wa zamani wa Ruvuma Nicodemus Banduka kwa kukutwa na nyaraka zenye muhuri wa siri za serikali.
Kitulo asante kunikumbusha Adam Mwaibabile "Mwana" nilisoma nae chuo cha uandishi wa Habari.
RIP Adam Mwaibabile, "Mwana".
Pasco
 
Nakumkumbuka wewe PASCO ambaye umeibwaga tasnia ya Tasnia ya Habari na kuwa mwandishi wa habari za kuwatetea watu binafsi wenye tuhuma za ufisadi kuanzia za Lowasa hadi za wale wanaotumbuliwa kama majipu na Magufuli.
Sema tu ukweli kwamba mpaka leo swali la Pasco kwa Magu lilikua gumu,haha :D

Na pia ni Mwandishi pekee kuitwa kamati ya maadili ya Bunge ..
 
Mashujaa gani P. Mayalla?wakati ushakuwa praise and worship team?rudi kwenye misingi mkuu! Unaetaka akuteue UDC,URAS yupo Korea ya Kaskazini akiaguliwa upepo wa kisulisuli!!!
 
Azory Gwanda huyu ni mwandishi wa Mwananchi alikuwa ni mbobezi wa habari za kiuchunguzi.Inasemekana kupotea kumetokana na kadhia ya Kibiti na Rufiji.
Mwandishi nguli na mbobezi ni yule anayeandika habari zinazoweza leta positive impact kubwa kwa jamii kubwa Mfano Betty mkwasa aliandika documentary Kali mno kuhusu tatizo la ukimwi makete ambako wanawake na watoto walikuwa wakipewa semina Hadi za jinsi ya kuchimba na kuzika na watoto wadogo Hadi miaka Saba kukuta ndio watunza familia .Ile habari ilitikisa dunia na Betty akapata award ya kimataifa ya uandishi na serikali kumpa vyeo nk

Baada ya documentary ile misaada ya kupambana na ukimwi ilifurika ka mvua ikiwemo mabilioni ya pesa za kigeni

Mwandishi nguli hatambuliki tu kwa kuandika negative information au kutukana Raisi au serikali.Unguli huo kusifiana kunaishia vyumba vya habari na jamii forums
 
Kuna yule aliyekatwa na panga la helicopter, sijui ilikuwaje lakini hadi likamkata, alikuwa anaitwa HALAHALA kama sikosei
 
Back
Top Bottom