Uhuru wa Habari ni dhana yenye misingi yake kifalsafa hadi kisheria-Dkt.Hassan Abbas

Maramla

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
560
1,000
-Uhuru wa Habari ni dhana yenye misingi yake kifalsafa hadi kisheria;

-Kuna kosa au dhambi ya karne kwa wanaharakati wengi wanaopigania haki kutoielewa vyema dhana hii vyema na ndio leo tunasikia kelele kila mara vyombo vya habari vinapoadhibiwa;

-Katika misingi ya kifalsafa uhuru wa habari unatokana na nadharia ya kale ya haki ya kujieleza ambayo imepiganiwa sana na wanafalsafa tangu wa zama za kale, kati na hivi karibuni;

-Akieleza hili katika kitabu chake cha II katika fasihi yake _Republica_ mwanafalsafa wa kale Plato aliainisha kuwa haki ya kueleza mambo ina ukomo na kwa wakati huo alizungumzia hakuna haki ya kusema uongo;

-Katika zama za hivi karibuni mwanafalsafa wa Kiingereza John Stuart Mill anayetambulika kama _Baba wa Uhuru wa Habari_ alitetea sana uhuru huo lakini akasisitiza ukomo wake pia;

-Katika nadharia yake iitwayo "harm principle" pamoja na kupigania uhuru huo Mill pia alisisitiza uhuru huo kukoma pale mtu anaposababisha madhara kwa wengine au kwa jamii;

-Misingi hii ya kifalsafa ikawekewa pia muktadha wa kisheria ambapo Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1966 ambao Tanzania imeuridhia umeainisha misingi hiyo kwa mtindo wa haki na wajibu;

-Ibara ya 19 ya Mkataba huo ambayo ndio msingi wa ibara ya 18 na 30 katika Katiba yetu na sheria zeyu za habari nchini inaainisha vyema kuwa uhuru wa habari una haki na wajibu na kuna mambo manne hivi yameainishwa kama ukomo;

-Mkataba umetaja mambo kama kutoingilia haki ya faragha bila sababu za msingi, kutovunjia watu heshima, kutoingilia au kutaka kuharibu usalama wa nchi na masuala ya afya na ustawi wa jamii;

-Kosa moja wanalolifanya wanaharakati na watetezi wengi wa uhuru wa habari ni kufumbia macho misingi hii hasa dhana kwamba wanahabari kama wanataaluma wengine wanapaswa kuzingatia haki za wengine ikiwemo kutii sheria;

-Duniani kote Serikali zina wivu mkubwa katika kuona amani, usalama na ustawi wa jamii zao unaendelea kuwa wa utulivu na huchukua hatua ikiwemo kwa wanahabari pale wanapotaka kuwa mawakala wa uvunjivu wa amani;

-Ni kwa misingi hii basi hata sisi Tanzania hatutasita kuchukua hatua pale chombo cha habari kinapokiuka misingi ya uhuru waliopewa;

-Hakuna chombo kitachukuliwa hatua kwa kukosoa tu Serikali.Kifungu cha 51 cha Sheria ya Huduma za Habari kinaruhusu kukosoa sera na utekelezaji wake na sisi kama Serikali tutaendelea kufaidika na ukosoaji wenye tija na kwa hakika siku zote tutalienzi hilo;

-Gazeti la Mawio halikufungiwa kwa sababu ya kukosoa.Kama ingekuwa sababu ni kukosoa Serikali tu lingefungiwa siku nyingi kwa sababu sera na mtindo wa uandishi wao ni kutafuta kasoro na kuzibainisha;

-Mawio limefungiwa kwa kukiuka sheria kama nilivyoeleza kuwa dhana ya uhuru wa habari haiwezi kutumika hovyo kutusi au kushusha heshima za watu wengine bila ushahidi wa msingi au kutaka kuhatarisha amani na usalama wa nchi kwa kuungaunga habari;

-Waziri wa Habari ana mamlaka ya kisheria chini ya kifungu cha 59 kuchukua hatua za haraka pale kunapokuwa na upotoshaji unaoweza kuhatarisha amani na usalama na ni hatua za kiutawala katika "administrative laws" anayeona kaonewa anaweza kupinga Mahakamani;

-Gazeti la Mawio kama kweli lilichapishwa Jumanne bado haliwezi kujitetea kwa kuangalia thamani ya hasara ambayo wangeipata kwa kutosambaza gazeti dhidi ya athari walizosababisha za kutuhumu watu wengine bila sababu za msingi na kutaka kuhatarisha amani na usalama wa nchi.Pia lipo gazeti la wiki la siku hiyo lilitii sheria kwa nini sio wao?Na kwa nini hawakuleta maelezo yao kabla kwa Msajili kumpa notisi luwa wameona agizo lakini walishachapa gazeti?;

-Tukiwa walezi wa taaluma hii tunachukua juhudi kubwa za kuilea tasnia ikiwemo kuwarekebisha waandishi kwa mazungumzo tena kimya kimya wanapokosea.Hata gazeti la Mawio katika uhai wake tangu lianzishwe faili lao linaonesha tumeshawaita takribani mara tano zipo nyakati walikuja kwa mazungumzo na mara nyingine walikaidi. Ukiona tunafungia gazeti ujue kuna kiwango cha juu cha ukiukaji wa sheria;

-Sheria ya Huduma za Habari ni bora zaidi ya ile ya Magazeti na imeanza kutumika na watu waisome, waijadili na kuitekeleza.Pale penye mapungufu hoja ziletwe walete hoja tutaiboresha huko mbele.Sheria imetoa haki na kinga mbalimbali ikiwemo ya kutoshtakiwa wakiomba radhi wanapokosea;

-Utekelezaji wa sheria ni kwa awamu mbalimbali kwani kwa sasa waandishi wamepewa muda wa miaka mitano kufikia kiwango cha cha elimu ambacho ni kuanzia diploma.Maeneo mengine ya sheria yanaendelea kutekelezwa;

-Sisi kama walezi tumechukua hatua mbalimbali ikiwemo kurahisisha masharti ya "press card" ili watu wafanye kazi wapate kipato wakasome na tukipata nafasi za udhamini tutazigawa kwa wanahabari wenye sifa;

-Tasnia ya habari ni fani adhimu na misingi yake ya kifalsafa na kisheria ienziwe kuliko kudhani kwamba unaweza kuandika chochote dhidi ya yeyote wakati wowote bila kufuata misingi ya kitaaluma na kisheria.

Imeandaliwa na Idara ya Habari-MAELEZO
 
chabusalu

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
7,860
2,000

Maneno mengi yaliyojaa porojo kutoka kwa watu wenye porojo. Huyo dakitari Abass angejibu swali hili:

Kifungu cha 59 cha Sheria ya Huduma za Habari namba 12 ya mwaka 2016 (hii ambayo Rais ameisaini haraka haraka) ambacho Daktari mwenzake Mwakyembe amekitumia kulifungia gazeti la MAWIO kinasema hivi:
"The Minister shall have powers to prohibit or otherwise sanction the publication of any content that jeopardises national security or public safety." na tafsiri yake kwa Kiswahili kinasema: "Waziri atakuwa na mamlaka ya kuzuia au kutumia njia nyingine kudhibiti uchapishaji wa taarifa yoyote inayotishia usalama wa taifa au usalama wa jamii."

Pamoja na mapungufu yote katika sababu alizotumia daktari Mwakyembe kufungia MAWIO, ni kwanini amelipiga ban gazeti hilo kwa miaka miwili ilhali sheria hii mpya na hususani kipengele alichokitumia, kinampa mamlaka ya kuzuia kuchapishwa kwa taarifa na sio gazeti zima?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom