Kagondo
JF-Expert Member
- Jun 6, 2016
- 296
- 79
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (Tanzania Human Rights Defenders Coalition ‘THRDC’ ) ambao ni mjumuiko wa asasi zisizo za serikali zinazotetea haki za binadamu hapa nchini, imetoa tathmini yake juu ya mapendekezo ya haki zilizo pendekezwa kutumika nchini.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu katiba na utawala bora, Bahame Nyanduga akiongea na baadhi ya wajumbe waliohudhulia vikao vya majadiliano ya haki za binadamu.
Mwaka jana 2015, wadau mbali mbali kutoka asasi zisizo za serikali chini ya mtandao (THRDC), walipeleka mapendekezo 227 ya haki za binadamu katika mkutano uliofanyika nchini Geneva, lengo likiwa ni kupatikana kwa haki mbalimbali za utetezi wa haki nchini.
Makundi ya haki yaligawanywa katika Nyanja tisa, nazo ni haki ya uhuru wa habari, watoto, wanawake, wafugaji/wakulima, siasa, mahitaji maalum, haki za kijamii, uchumi na aridhi pamoja na haki za binadamu kwa ujumla.
May 2016, THRDC ilipata marejesho ya mapendekezo hayo, ikiwa jumla ya mapendekezo 130 kati ya 227 yalikubaliwa na serikali yatumike kisheria, 72 yaliwekwa kama mswada, na 25 yalikataliwa yasitumike kisheria.
Takwimu hizi zimeamsha hisia za wanaharakati wa haki za binadamu, ambapo imeonekana kuwa bado ni idadi kubwa ya haki za binadamu ambazo ni ukombozi kisheria zimekataliwa, na hivyo kupelekea kupitiwa upya ikiwa ni njia ya kuishawishi serikali kuyafikiria upya mapendekezo yaliyokataliwa na yale yaliyowekwa kama mswada ili kukubalika.
Vyombo vya habari ikiwemo watu kuwa huru kutoa maoni yao, itasaidia upatikanaji wa haki za binadamu kwani kupitia vyombo vya habari wananchi wataweza kuchangi maoni yao na mapendekezo yao.