Uhuru wa Afrika........haijathibitika kisayansi ni wapi mkoloni alitunyonya!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhuru wa Afrika........haijathibitika kisayansi ni wapi mkoloni alitunyonya!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Malyenge, Mar 9, 2012.

 1. M

  Malyenge JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 4,402
  Likes Received: 1,365
  Trophy Points: 280
  Wakuu leo hii nimeamua nilete mada hiyo hapo juu tuijadili.
  Imekuwa ni kawaida ya wanasiasa wakati wa sherehe za uhuru zinazofanyika kila mwaka kutuhubiria kuwa wananchi walimwondoa mkoloni wa Kiingereza kwa kuwa alikuwa mnyonyaji. Na wamekuwa wakitujaza mawazo hayo ya kiukombozi ili kuhalalisha utawala uliopo madarakani kwamba upo hapo "kihalali'.
  Lakini katika kutujaza mawazo hayo ya kiukombozi bado huwa wanashindwa kufafanua ni wapi mkoloni huyo alitunyonya au kutudhulumu kiasi kwamba ikaonekana ni vema mkoloni huyo aondolewe. Kwa mfano, unyonyaji wa mkoloni unaozungumzwa saaaana ni ule wa kutumikisha watu mashambani au viwandani bila malipo au kwa malipo (ujira) kidogo sana . Na udhalimu mbaya kabisa ni ule wa kuwalazimisha watu kufanya kazi na kwa waliokadidi walichapwa viboko. Madai ya uovu wa mkoloni ni mengi sana na yanahadithiwa kwa namna mbalimbali na watu waliokuwapo kipindi kabla ya uhuru.......
  Lakini mimi nimefanya utafiti kwa kipindi cha miaka ishirini kwa kutafuta ushahidi wa madai hayo. Napenda kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuja na ushaidi wa yale niliyoyapata kama ushahidi wa "ubaya" wa mkoloni.Na ushahidi huu nilioupata (conclusion) ni ule unaoitwa ushahidi linganifu kwa minajiri kutafakari kama uhuru tulionao sasa ni uhuru wa kweli na ama hakukuwa na haja ya kudai uhuru huo kwa maana ya kwamba ilikuwa bado mapema ama hakukuwa na haja kabisa. Historia tunayoijua kuhusu Afrika kwa sasa ni ile ya upande mmoja yaani haielezi uzuri wa sisi Waafrika ulikuwaje kipindi tunatawaliwa. Na historia hiyo haielezi kutawaliwa tulikotawaliwa na wakoloni kosa lilikuwa ni la nani au nani alifanya uzembe mpaka tukatawaliwa.
  Yafuatayo ndiyo matokeo ya utafiti wangu. (Nawaomba wana JF wakosoe namna nilivyowasilisha utafiti wangu na si hoja zilizomo, maana muda wa kuipanga hii conclusion yangu sina kwa sababuu naandika huku nikiendelea kufanya kazi za watu ofisini). Na isitoshe nimewaomba mchangie na ninyi mnasemaje.


  [TABLE="class: MsoTableGrid, width: 6"]
  [TR]
  [TD="width: 55, bgcolor: transparent"]
  [/TD]
  [TD="width: 288, bgcolor: transparent"]WAKATI WA MKOLONI
  [/TD]
  [TD="width: 300, bgcolor: transparent"]BAADA YA UHURU (HASA MIAKA YA KARIBUNI)
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 55, bgcolor: transparent"]1.
  [/TD]
  [TD="width: 288, bgcolor: transparent"]Watu walilazimishwa kulima mashamba ya serikali na yao binafsi.
  [/TD]
  [TD="width: 300, bgcolor: transparent"]Watu wanahiari ya kukaa bila kufanya kazi
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 55, bgcolor: transparent"]2.
  [/TD]
  [TD="width: 288, bgcolor: transparent"]Reli ilijengwa kwa minajiri ya kusafirisha mazao na abiria
  [/TD]
  [TD="width: 300, bgcolor: transparent"]Reli imekufa na hakuna mizigo inayosafirishwa na abiria wachache sana wanaosafiri wanakwama njiani usafiri hauaminiki
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 55, bgcolor: transparent"]3.
  [/TD]
  [TD="width: 288, bgcolor: transparent"]Magereza yalijengwa na kila mhalifu aliingia humo
  [/TD]
  [TD="width: 300, bgcolor: transparent"]Magereza yapo lakini ukiwa na pesa huingii kabisa ama ukiingia unaishi kama uko uraiani
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 55, bgcolor: transparent"]4.
  [/TD]
  [TD="width: 288, bgcolor: transparent"]Watu walichapa kazi kwa moyo japokuwa waliogopa viboko
  [/TD]
  [TD="width: 300, bgcolor: transparent"]Moyo wa kufanya kazi haupo na kila mtu anataka kufanya kazi lainilaini
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 55, bgcolor: transparent"]5
  [/TD]
  [TD="width: 288, bgcolor: transparent"]Pesa ilikuwa na thamani japo upatikanaji wake ulikuwa mgumu
  [/TD]
  [TD="width: 300, bgcolor: transparent"]Pesa haina thamani upatikanaji ni mgumu kwa watu wa hali ya chini tu.
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 55, bgcolor: transparent"]6.
  [/TD]
  [TD="width: 288, bgcolor: transparent"]Madaraka yalipatikana kwa sifa na uwezo wa mtu
  [/TD]
  [TD="width: 300, bgcolor: transparent"]Madaraka yanapatikana kwa pesa na kwa kujuana
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 55, bgcolor: transparent"]7.
  [/TD]
  [TD="width: 288, bgcolor: transparent"]Mahakama na jeshi la polisi ilikuwa ni vyombo vinavyojitegemea
  [/TD]
  [TD="width: 300, bgcolor: transparent"]Mahakama na jeshi la polisi ni vyombo vinavyotegemea wanasiasa wanasemaje
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 55, bgcolor: transparent"]8.
  [/TD]
  [TD="width: 288, bgcolor: transparent"]Watu tulikuwa tunapendana sana !
  [/TD]
  [TD="width: 300, bgcolor: transparent"]Watu tumejaa chuki.
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 55, bgcolor: transparent"]9.
  [/TD]
  [TD="width: 288, bgcolor: transparent"]Umoja wa kitaifa ulikuwa katika kiwango cha juu sana.
  [/TD]
  [TD="width: 300, bgcolor: transparent"]Utaifa limebaki ni neno la kuombea kura tu.
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 55, bgcolor: transparent"]10.
  [/TD]
  [TD="width: 288, bgcolor: transparent"]Mwananchi alikuwa anategemea kazi na taaluma ndio msingi wa yeye kupata pesa
  [/TD]
  [TD="width: 300, bgcolor: transparent"]Kazi na taaluma si kigezo cha mtu kupata pesa. Kupata pesa ni ujanja wa mtu husika.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Nawasilisha wakuu.
   
 2. R

  RUTARE Senior Member

  #2
  Mar 9, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Ukoloni wa kwanza haukuwa mbaya kuliko huu wa pili,ila tofauti yake ni kwamba ukoloni wa pili uliongozwa na Mwafrika, na ule wa kwanza uliongozwa na mzungu kutoka Uingereza. Kwa hiyo tofauti ilikuwa ni viongozi wa ukoloni, na Watanzania hawakutoka katika minyororo ya ukoloni, bali walibadilika kutoka ukoloni huu kungia mwingine ambao ndio unaowatawala mpaka leo. Kwa watu wenye mawazo kama mimi, ni heri tungebaki kama tulivyokuwa maana msaada wa kweli ungetoka popote, kuliko kujidanganya kuwa tulikuwa salama na kumbe ukweli wa mambo ni kwamba tulikuwa pabaya kuliko mwanzo."
   
 3. Companero

  Companero Platinum Member

  #3
  Mar 9, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  kwanza wanaukumbuka.halafu wanausifia.mwishowe wanaurudisha.

  'kitu kizuri pekee cha ukoloni ni mwisho wake ' - walter rodney
   
 4. Companero

  Companero Platinum Member

  #4
  Mar 10, 2012
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mzungu = Wa Mungu
  Africa = Wa Afrit

  Zomba.
   
 6. domokaya

  domokaya JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2012
  Joined: Apr 22, 2010
  Messages: 3,112
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kazi kwelikwali, eti unataka uthibitisho wa kisayansi kuwa eti wakoloni walitunyonya? Uthibitisho wa kisayansi ni hiyo dini unayoiamini, wakoloni walitunyonya mpaka mawazo na kutupa dini zao na tukachukua majina yao yasiyotuhusu. Labda ulitaka kusema kitu ila tu umeshindwa kujieleza. Labda ulitaka kusema kuwa wakoloni bado wapo wanatunyonya zaidi kuliko awali ila sasa wakoloni hawa si weupe tena bali wazungu weusi ambao kwa kiasi fulani tuna nasaba nao. Kama hivyo sawa, lakini kama bado unataka uthibitisho wa maabara basi tafakuri yako itakuwa ina matatizo makubwa na mtu tafakuri yake ikisha na matatizo hayo wa nini tena thamani yake ni sawa na mtu aliyekufa
   
 7. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,916
  Likes Received: 2,341
  Trophy Points: 280
  Hii ni mada nafikiri ya pili ya kutukuza ukoloni katika jamvi.
  Naamini aliyeiandika ni mtu mjinga mjinga anayedai alifanya "utafiti" ambao hauna data wala reference.

  Kwa vile hili lipo jamvini na mtu anapenda kutawaliwa , isiwe issue, mtoa mada anaweza kumilikishwa na kutumikishwa kwa ridhaa yake hata leo.
  Ningmshauri aje kwangu awe house boy atakula , kunywa na kulipwa bila shida lakini NITAMMILIKI-na hiyo iwe trela ya kule anakotaka kwenda kumilikiwa.
  Kimsingi mtu wa aina hii(anayependa kumilikiwa ) ni mtu mvivu sana kuanzia kufikiri hadi kufanya kazi,yeye ni mtu wa kusubiri kuletewa.
  Mawazo ya kijinga kijinga namna hii yasipewe nafasi, na sijasikia kwa mfano, Mhindi(Tanzania hii hii) akiomba kazi serikalini.Mtu anaishi kwa bongo na anatajirika wakati wengine wanasubiri kufanyiwa kila kitu.
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Unataka reference mpaka iwe na jina la Mzungu ndio ujuwe imefanyiwa utafiti? na hizo "data", kwanini wewe usije na zako kupinga hoja badala kumpinga mleta hoja.

  Kuhusu la kujituma nipo na wewe, wa Afrit ni wavivu sana kupita kiasi, Mhindi ukianza kufanya kazi Serikalini sisi tule nini? Muhindi serikalini inaweza asiombe kazi wakati huu kwa sababu huko hakuna kinachofanyika, wahindi wamezoea kazi ilete tija, sio yeye anafanya kazi mwenzake kaenda kuzika shangazi kwa mara ya sita kwa mwaka huo.
   
 9. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,916
  Likes Received: 2,341
  Trophy Points: 280
  Mkuu mada sikutoa mimi and if at all nachukia maneno ya vijiwe kwenye issue ambazo basically ni nzito katika jamii.
  Rejea yako kuwa nitaamini hiyo mada kama ina ref. ya mzungu haina mantiki na haiendani na argument in question.
  Ukiulizwa kitumbua jibu kitumbua na si nazi.
  Kwa kifupi mtoa mada hajaleta argument iliyoenda shule zaidi ya kupenda kutumika na wazungu hao hao anaowahusudu.
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mpaka sasa bado unalalama lakini hujakuja na hoja mbadala. Unaleta habari za vitumua na na nazi, tukikaa kidogo utaleta nzi na mende.

  Wa Mungu anamtumikisha Wa Afrit apendavyo, hakuna cha kumzuia tena anakuwa more efficient, kwani mwenyewe hawezi kitu bila ya kuongozwa (kuswagwa).
   
Loading...