UHURU UHURU VIPI,,,,??

seif_tanzania

Member
Nov 23, 2017
14
2
Imeandaliwa na
*ndugu IDDY SEIF HARUNA*
*UHURU UHURU*
Tarehe 09.12.1961 ni siku ambayo shangwe na nderemo zilisikika kila pande ya Tanganyika sio wazee,sio kinamama,sio vijana wote walikuwa na furaha juu ya kupata Uhuru
[HASHTAG]#Tanganyika[/HASHTAG] chini ya hayati baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambae alikuwa kinara wa juu kabisa kuupambania Uhuru ambao tunajivunia nao katika pande zote za nchini
Uhuru huu tulioupa tumeufanyia nini mpaka sasa???
Kipindi Uhuru ulipokuwa ukipiganiwa Tanganyika mwalimu alikuwa anahamasisha sana wananchi kuwa wazalendo na kwa kipindi hicho uzalendo ulikuwa mkubwa,swali la kujiuliza Je huo uzalendo sasa umeenda wapi...???
Uzalendo alikuwa akiusema mwalimu sasa umeishi kuutamka kwenye mitando ya kijamii na kuutekeleza umekuwa mgumu ...
Ikumbukwe pia wakati tunapata Uhuru mwalimu aligusia suala UMOJA NA MSHIKAMANO ni na azma ya jambo hili ni ili kujikombo kutoka katika hali ya ngumu ya kiuchumi iliokuwa inatutesa kipindi kile lakini swali la kujiuliza Je UMOJA NA MSHIKAMANO bado unatekelezwa....????
Pia ikumbukwe Uhuru ulipokuwa ukitangazwa Tanganyika mwalimu alisema ni lazima tuwe na UONGOZI SAFI NA SIASA BORA ili tuweze kuyafikia maendeleo kwa uharaka zaidi.swali la kujiuliza kwa sasa HALI YA SIASA IPOJE...??
Pia Uhuru huu ulipotangazwa ulilenga zaidi kutukomboa kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo
KIUCHUMI
SIASA
KIJAMII NA KITAMADUNI
Kwa Leo nagusia hali ya UCHUMI toka Uhuru mpaka sasa
tunaona toka Uhuru jitihada ni kubwa sana zilizochukuliwa kutukomboa kiuchumi kama
1967 kuanzishwa kwa azimio la Arusha lengo sio tu kuwa na Ujamaa lakini huo Ujamaa utusaidie kukuza uchumi wetu
Binafsi naona katika kipindi cha kwanza cha miaka 10 ya UHURU Tanganyika ijapokuwa tulikuwa na hali ngumu sana lakini jitihada za kukuza uchumi zilikuwa nyingi sana na za kipekee lakini swali la kujiuliza Jitihada hizo zipo wapi sasa.....???
Tunahitaji Tanzania kuwa ya viwanda kwa sasa lakini dhana hii ina shindwa kueleweka kwamba siku zote maendeleo ya viwanda kwa taifa lolote yanatokana na maendeleo ya watu.pia dhana hiii ambayo toka Uhuru ilikuwa ikitizamiwa kuwa ni mkombozi wa uchumi wa Tanzania lakini bado imekuwa ngumu kueleweka kwa ni tunaimba Tanzania ya viwanda lakini tunashindwa kutambua kuwa
Viwanda wapii...??
Viwanda linii...???
Na viwanda kwa akina nani.....???
Hivyo kama tumeichagua Sera hiyo ya viwanda kuwa mfumbuzi wa hali ngumu ya uchumi toka Uhuru lazima tujiulize maswalii hayoo
Mimi naona ili kuweza kukaa na kusherehekea maadhimisho ya sherehe za Uhuru nchini ni vyema dhana ya UZALENDO iwekwe mbele na SIASA ZA MAJITAKA tuzipe mgongo ili tuweze kupata Uhuru wenyenyewe kabisa
Imeandikwa tareha 09.12.2017 na
*ndugu IDDY SEIF HARUNA*
*Kijana mzalendo*
1d8b6f9babe831de1bc4ac3148a66eee.jpg
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom