UHURU siyo gazeti mama hapa nchini, Gazeti mama ni KIONGOZI

MdogoWenu

JF-Expert Member
Dec 23, 2009
555
915
Wote tumeona Chama Cha Mapinduzi, CCM, kimekanusha taarifa ya gazeti la UHURU kwamba Samia hatagombea urais mwaka 2025.

Lengo la habari hii siyo kanusho hilo lakini ni kitaarifa ndani ya taarifa hiyo kwamba UHUR ndilo Adam na Hawa ya magazeti yote hapa nchini.

Hivi ndivyo ambavyo historia hupotoshwa.

Gazeti la kwanza hapa nchini ni KIONGOZI limeanzishwa na Kanisa Katoliki mwaka 1935 kabla hata magazeti ya serikali. Baadaye yakafuata magazeti ya serikali.

TANU ilipoanza kupigani uhuru mwaka 1954 ikawa chama cha upinzani wa serikali. Kama kawaida ya serikali nyingi duniani huwa haziandikia habari za chama kikuu cha upinzani.

Kwa kuona hivyo TANU ikaanzisha magazeti yake, moja liliitwa SAUTI YA TANU na jingine ikaliita gazeti hilo UHURU.

Hata hivyo TANU lilipata misukosuko kama kawaida ya serikali kutia misukosuko magazeti la chama cha upinzani, kama lilivyofungiwa gazeti la MWANAHALISI, MAWIO.

Hata kesi pekee ya Julius Nyerere ni ile ambayo gazeti la SAUTI YA TANU liliandika na serikali ikaona Nyerere amewatukana wakuu wa Wilaya.

Bahati nzuri ugaidi haukuwa umeenea mno wakati huo huenda Nyerere naye angebambikiziwa kesi ya ugaidi.

All in all, UHURU siyo gezti la kwanza hapa nchini bali gazeti la kwanza na ambalo bado lipo na halijaacha kutoka ni KIONGOZI

-
 
Back
Top Bottom