UHURU: Serikali yamwagiwa sifa na CCM-Mara kwa kushughulikia kwa Umakini Mgogoro Mgodini North Mara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UHURU: Serikali yamwagiwa sifa na CCM-Mara kwa kushughulikia kwa Umakini Mgogoro Mgodini North Mara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 2, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wednesday, 01 June 2011 20:21 newsroom  NA MWANDISHI WETU
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara, kimeipongeza serikali kwa kushughulikia kwa umakini mgogoro uliotokea hivi karibuni katika mgodi wa North Mara na kusababisha vifo vya watu watano. Serikali pia imepongezwa kwa kudhibiti udanganyifu na matumizi mabaya ya fedha zilizotolewa na mgodi huo kwa ajili ya kuwalipia ada wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vya elimu ya juu. Pongezi hizo zilitolewa jana na Kamati ya Siasa ya CCM mkoa wa Mara. Chama kimesema kama suala hilo lisingesimamiwa kwa umakini, lingeweza kuleta maafa makubwa kutokana na kuchochewa na kuratibiwa na viongozi wa CHADEMA.

  Katibu wa CCM wa mkoa huo, NdengÂ’asso Ndekubali, alisema kamati imeshangazwa na mwenendo wa CHADEMA wa kutoheshimu miili ya watu waliokufa kwenye uvamizi wa mgodi wa North Mara.Ilielezwa viongozi wa chama hicho waliwashawishi ndugu wa marehemu kususia maiti. Mwezi uliopita takriban watu 800 walivamia mgodi huo kwa lengo la kuiba mchanga wenye dhahabu, ambapo polisi katika kuwadhibiti watu watano walikufa kwa kupigwa risasi na wengine kadhaa wakiwemo askari walijeruhiwa.

  Kamati hiyo imeishauri serikali kuhakikisha wachimbaji wadogo wanaandaliwa eneo la uchimbaji nje ya mgodi na wasaidiwe ili kufanya kazi zao vizuri. Ndekubali alisema kamati imeiagiza serikali kuwatambua wakazi wa eneo hilo na tabia zao, kwani wapo wananchi ambao si wakazi na kwa mara kadhaa wamekuwa chanzo cha vurugu. Kamati ya siasa imeshauri kubadilishwa mfumo wa ulinzi katika eneo hilo, kwa kuwatumia wenyeji wa vijiji vinavyozunguka mgodi na kampuni binafsi badala ya polisi.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  SO CCM knew about the problems @ the North Mara - na walipewa pesa za kusaidia wananchi CCM wanatumia Authority kuwanyima wananchi haki zao.

  So ni UFISADI Ndani ya Serikali ya CCM; So what Chadema did is to influence the people to get their rights

  The key to successful leadership today is influence, not authority.
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280

  Na hiki ndicho walichokuwa wanataka na si zaidi ya hapo
  maana wananyanyaswa kama madini hayako kwenye ardhi yao na waliahidiwa kuwa watapewa maeneo ya kufanyia kazi ila kwa nguvu hawajaona lolote
   
 4. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Watu 800 walivamia mgodi kuiba mchanga wenye dhahabu!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 5. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Magamba wanachekesha sana, wanawafanya watanzania kama watoto wa chekechea, kwani cdm walihimiza wananchi kususia maiti ili iwe nini? Lengu ni uchunguzi ufanyike kabla ya maziko japo wao magamba walitaka wazikwe bila taarifa ya mauaji, kwa mtaji huu wanazidi kujiweka uchi kwa wananchi wakidhani kwamba ndio watasafisha nyota yao
   
Loading...