Uhuru na Mapinduzi ya Zanzibar

Ng'wanamalundi

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,163
1,359
NCCR Mageuzi wataka siku ya uhuru wa Zanzibar

Fidelis Butahe

CHAMA cha NCCR-Mageuzi, kimeibuka na hoja mpya ya kutaka kutambuliwa kwa siku ya uhuru wa Zanzibar ,kama ilivyo kwa siku ya uhuru wa Tanganyika.

Chama hicho kimeelezea matumaini yake kuwa kwa pendekezo hilo, serikali itaona umuhimu wa kuifanya Desemba 9 kuwa siku ya Uhuru wa Tanganyika na Desemba 10 kuwa siku ya uhuru wa Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mkuu wa idara ya organaizesheni na uenezi ya chama hicho, Faustin Sungura alisema hiyo inatokana ukweli kwamba nchi hizi, zilipata uhuru Desemba, za miaka tofauti.

"Tanganyika ilipata uhuru wake Desemba 9 mwaka 1961 na Zanzibar ilipata uhuru wake Desemba 10 mwaka 1963…watu wanaposheherekea miaka 45 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, watengenishe mambo mawili yanayofanywa kuwa jambo moja ambayo ni uhuru na mapinduzi," alisema.

"Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar zinatuambia kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika Januari 12, 1964",

"Mapinduzi haya yanatualika katika umoja wetu kwa maslahi ya ustawi wa historia ya Zanzibar, kujua kama kabla ya mapinduzi ya mwaka 1964 Zanzibar ilikuwa tayari imeshajipatia uhuru au la, na kama Zanzibar haikuwa imepata uhuru iliwezekana vipi yakafanyika mapinduzi kwenye nchi ambayo haikuwa huru" alisema Sungura

Sungura alisema kuwa mwaka 1961 Zanzibar kulifanyika uchaguzi mara mbili ambapo mara ya kwanza, vyama vya siasa vya ASP, ZNP na ZPPP vilivyoshiriki katika uchaguzi huo, havikutoa mshindi licha ya matokeo kuonyesha kuwa ASP ilipata kura 10 na ZNP kura 9.

"Katika uchaguzi wa pili wa Juni 1961 machafuko makubwa yalitokea ambapo watu 48 walikadiriwa kupoteza maisha na wengine 400 kujeruhiwa, Julai 8 mpaka 11, 1963 kulifanyika uchaguzi mwingine ambapo vyama vya ZNP na ZPPP viliungana na kupata viti 18 ambapo ASP ilipata 13",

"Septemba 20 mpaka 24, 1963 ulifanyika mkutano nchini Uingereza ambapo pia ulijadili katiba ya Zanzibar, lakini Desemba 10, 1963 ndiyo siku ambayo Zanzibar, ilipata uhuru wake kutoka kwa mkoloni wa Kiingereza" alisema Sungura

Alisema baada ya Zanzibar kupata uhuru, Seyyid bin Thuweni, ikiwa Sultan na mkuu wa nchi aling’olewa madarakani Januari 12, 1964 baada ya kufanyika kwa mapinduzi.

Sungura alisema kutokana na historia inavyoonyesha umefikia wakati Tanzania ikisheherekea uhuru Zanzibar nayo isheherekee siku yao ya uhuru kama ilivyo kwa Tanzania.



Mimi nadhani hatuna budi kuchagua siku moja tu: ama kuitambua siku ya tarehe 10 Desemba 1963 au siku ya tarehe 12 Januari 1964. Kwa ufahamu wangu "uhuru" uliopewa Zanzibar hiyo tarehe 10 Desemba 1963 ulikuwa batili. Siyo uhuru wa kwelikweli. Ndiyo maana yakafanyika mapinduzi. Kama tutasherehekea tarehe 10 Desemba kama siku ulipopatikana uhuru wa Zanzibar, itakuwa sawa na kusema kwamba mapinduzi yaliyofuatia hayakuwa halali. Kwa hiyo hakuna maana kusherehekea mapinduzi ya tarehe 12 Januari 1964. Maoni yangu ni kwamba tuendelee na kusherehekea tarehe 9 kama siku ya uhuru wa Tanganyika; tarehe 12 Januari kama siku ya Mapinduzi (kuzaliwa uhuru wa kweli) wa Zanzibar; na tarehe 26 Aprili kama siku ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar (siku ya kuzaliwa Tanzania).
 
SAHIHISHO: sultan aliyeng'olewa mwaka 1964 ni Sayyid Jamshid bin Abdallah na si sayyid bin thuweyn
 
Mahindi, kwa kigezo kipi uhuru wa zanzibar ulikuwa batil?
kwani zanzibar walipata uhuru kutoka kwa nani?
kuna data zozote zinazothibitisha ushaguzi wa 1963 hawkuwa halali ?
jee uongozi halali uliingia madarakani? kama khiana ilifanyika wakulaumiwa nani? Rudi kwenye historia ndipo uboronge maoni!
 
Hivi Mainland tukijiunga tena na Komoro na baadae Ushelisheli,

Je tutakuwa na siku ngapi za uhuru?
 
WAZANZIBARI WANA JAMBO MUHIMU LA KULISHUGHULIKIA NA SIO TOFAUTI ZA TAREHE. UHURU ULIKUWA HALALI NA MAPINDUZI NI HALALI NA KWA VILE KIMEKUJA MWISHO TUTAYAHESHIMU NA KUYASHEREHEKEA KAMA KIGEZO CHA UTAWALA WA SASA.

Tatizo linalotukabili sasa ni mfumo mbaya wa Muungano unaotufanya hata tuhisi bora kabla ya Mapinduzi.
 
Kujuwa nini kilitokea siku ya mauwaji kwa jina jingine mapinduzi na kina nani walikuwa wakifanya hayo mapinduzi utagunduwa hawakuwa wazanzibari angalia hii clips mpaka mwisho kupata picha yenyewe hasa naimani wengi tutakuja na maoni kuhusiana na kilichotokea sikiliza kiswahili kinacho zungumzwa humo [ame=http://www.youtube.com/watch?v=YTEYDJ5ykCw]YouTube - ZANZIBAR[/ame]
 
Gozigumu, Uhuru halali baada ya siku 31 nchi kupinduliwa halali, na baada ya siku 105 kuungana na nchi nyengine, upande wa pili wa bahari HALALI! tena twaulamiani muundo wa Muungano? eti leoo baada miaka 44 ya muungano ndio twabaini makubaliano ya asili yamekiukwa!
Tuendele kuwa koloni tu, jana la Muingereza leo la Tanganyika! SOJI TU LIMEBADILIKA!
 
...political opportunists, ...mbinu mbadala za kutafuta kura mbili tatu huko visiwani. Msituchanganye jamani!
 
Mahindi, kwa kigezo kipi uhuru wa zanzibar ulikuwa batil?
kwani zanzibar walipata uhuru kutoka kwa nani?
kuna data zozote zinazothibitisha ushaguzi wa 1963 hawkuwa halali ?
jee uongozi halali uliingia madarakani? kama khiana ilifanyika wakulaumiwa nani? Rudi kwenye historia ndipo uboronge maoni!

1832 Sultan Seyed Said established his residence on Zanzibar and in moved his capital from Muscat to Zanzibar.

Germany led by Bismarck claimed a lot of land in Tanzania. In 1890 Zanzibar and Pemba fall under British protectorate rule.

Zanzibar gained independence in 1963 with Sultan Jamshid ibn Abdullah as head of state and Prime Minister Muhammad Shamte Hamadi, as a series of democratic elections had resulted in the Arab minority retaining the hold on power it had inherited from Zanzibar's former existence as an overseas territory of Oman.

...Uhuru kwa muendelezo wa Usultani pamoja iliyokuwa Coalition 'puppets' Government ya ZNP na ZPPP au sio? ...no wonder Wapemba waonekana wasaliti.

just buzzing with cheap comments, save it for unfounded claim

...excuse me?


View attachment 4173

...bilauri weye bilauri unaiangaliaje?
 
Gozigumu, Uhuru halali baada ya siku 31 nchi kupinduliwa halali, na baada ya siku 105 kuungana na nchi nyengine, upande wa pili wa bahari HALALI! tena twaulamiani muundo wa Muungano? eti leoo baada miaka 44 ya muungano ndio twabaini makubaliano ya asili yamekiukwa!
Tuendele kuwa koloni tu, jana la Muingereza leo la Tanganyika! SOJI TU LIMEBADILIKA!

Sio kweli kuwa hakukuwa na harakati za kujinasua na muundo wa Muungano. Karume Baba alisema kuwa Muungano ni kama koti likitubana tutalivua na wkati wake kila kitu cha Tanganyika kiliishia Chumbe na Zanzibar tulikuwa na kadi zetu za uraia kuonyesha kuwa zilikuwa ni nchi mbili ndani ya muungano. mwaka 1977 kuliungaishwa vyama na Tanganyika wakachukua nafasi ya kuimeza zanzibar na kuanzia hapo harakati za Wazanzibar zikawa zinzimwa kichama. Mwaka 1984 Wazanzibar walidai haki zao na Jumbe akafukuzwa kazi na Kina Seif Bakari wakatiwa ndani. Wasaliti wa Jumbe walipofahamu Makosa yao nao walidai haki ya Zanzibar (kina Seif Sharif) wakafukuzwa chamani na serikalini. Sasa kusema kuwa kwa kipindi chote hicho tulikuwa kimya si sahihi hata kidogo.
Hivi sasa ni kwa kuwa ni sera ya KIkwete kuwapa watu uhuru wa kusema ndio unaona harakati hizi zinatushirikisha hata sisi kwani huko nyuma kuzungumzia Muungano ilikuwa ni Uhaini.
 
Ndugu zetu,



Assalaam Alaaykum,



UMOJA, UHURU, UADILIFU



Qauli ya Umoja wa Wazalendo

Kukhusu Siku ya Uhuru wa Zanzibar



Date::4/6/2009

NCCR Mageuzi wataka siku ya uhuru wa Zanzibar
Fidelis Butahe

CHAMA cha NCCR-Mageuzi, kimeibuka na hoja mpya ya kutaka kutambuliwa kwa siku ya uhuru wa Zanzibar, kama ilivyo kwa siku ya uhuru wa Tanganyika.




Shukrani za Dhati Kutoka Moyoni mwa Wazanzibari

Hapana shaka Wazanzibari tutakuwa si wenye fadhila iwapo hatutatoa “shukrani zetu za dhati” kwa ndugu zetu NCCR, Mageuzi; viongozi na wananchi, bali khasa kwa Mhishimiwa Bwana Faustin Sungura kwa hili pendekezo adhimu kabisa la kutaka, “kutambuliwa kwa siku ya uhuru wa Zanzibar…….”, Disemba Kumi, 1963.



Dola Huru Ya Zanzibar
Kwa Rehma za Mwenyezi Mungu Mtukufu Subhaanahu wa Taáala, na juhudi za pamoja za kila Mzanzibari; taarikh 10 Disemba, 1963; Nchi yetu Zanzibar, ilipata Uhuru wake na kuwa ni Dola Huru Kaamili miongoni mwa dola za ulimwengu.


Sherehe Za Uhuru
Wananchi wote, wakubwa na wadogo, wanaume na wanawake, waliupokea Uhuru wa nchi yetu kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu Subhaanahu wa Taáala na kwa fura*ha na bashasha kubwa. Mji uling’ara kwa mapambo ya namna mbali mbali. Tamasha hizi na zile zilifanywa na wananchi kwa kufurahikia Uhuru wao. Sherehe na mapambo hayakuwa Mjini tu, bali mashamba kote. Na huko Pemba nako kulifanywa sherehe kama za Unguja, tangu mijini mpaka mashamba. Wazanzibari tulijaa tamaa na matumainiyo ya kwamba baada ya juhudi na kazi ngumu ya kuleta Uhuru wetu na kwa kuondoka mtawala Muingereza sasa tutaweza kujenga Nchi yetu kwa pamoja. Haya yalielezwa hivyo na kiongozi wa Afro-Shirazi Party (ASP), Mzee Abeid Aman Karume katika munasaba wa siku hii adhimu kwa kusema:



“Leo mwezi 10 Disemba, 1963, ZANZIBAR imekuwa Huru. Hii leo sisi watu wa visiwa hivi tumepata haki ya kuchukuwa mahala petu kuwa ni Dola sawa na nyengine katika umoja wa Nchi za Dola za Commonwealth. Kwa uchache, kuwa mwanachama katika umoja huo, kuna maana kwamba nchi hii ni huru chini ya mpango wa serekali ambayo msingi wake umejengwa juu ya kuendeleya kwa ridhaa ya wananchi.



Ili kufikiliya matarajiyo yetu hayo tunayo moja katika Katiba zenye msingi madhubuti iliyohusika na shuruti za haki za binadamu, haki za mambo ya siyasa na uhuru wa dola yoyote nyengine. Ni wajibu wa watu wote wa dola yetu mpya, kila mmoja katika sisi bila ya kujali fikra zetu za siyasa au madaraka yetu kusaidyia kweli kweli Katiba yetu iweze kufanya kazi. Pamoja na manufaa, haki na uhuru ambayo yote hayo yamepatikana baada ya nchi kuwa huru.



Tuliyoyapata leo mwezi 10 Disemba ni mipango ya mwanzo tu ya kuweza kufanya juhudi kwa ukamilifu dhidi ya maadui zetu nao ni ujinga, umasikini na maradhi na kuweza kuleta imani penye khofu na shaka na kuleta masikilizano mahala ambapo hata hivi sasa adawa ipo, na kuleta mapenzi mahala ambapo pana chuki, ili dola yetu mpya ichomoze katika neema, umoja na furaha.



Kwa hivyo katika hii siku ya leo na tumwombe Mwenye Enzi Mungu Mtukufu Subhaanahu wa Taáala, Inshaallah atuweke tuifanye na tuitimilize kazi kubwa ya kujenga taifa letu ili dola yetu mpya ya ZANZIBAR ipate baraka ya matunda mema ya kazi zetu. Uhuru na Umoja, Uhuru na kazi!”



Kusitishwa Kumbukumbu za Uhuru wa Zazibar

Baada ya Tanganyika chini ya utawala wa Mwalimu Julius Nyerere kuivamia Dola Huru Kaamili ya Zanzibar na kuitia chini ya makucha yake kwa kisingizio cha huu wenyekuitwa muungano, hata pia bila ya ridhaa ya ndugu zetu wananchi wa Tanganyika; hapohapo ilisitishwa siku hii adhimu, siku ya Uhuru wetu, Disemba Kumi, 1963. Ilisitishwa kumbukumbu za Uhuru wetu na kuletwa hii nyimbo tunayoendelea baadhi yetu kuiimba mpaka hii leo “uhuru wa bandia”.



Wazanzibari Wanaikumbuka Siku ya Uhuru Wao

Kwa Rehma za Mola wetu Mlezi Subhaanahu wa Taáala na kwa kuzidi Uzalendo nchini mwetu, Zanzibar; Wazanzibari siku ya Disemba Kumi, 2008 walikusanyika kuikumbuka siku hii adhimu. Wazanzibari bila ya kuzingatia itikadi zao za kisiasa walikusanyika kwa kusoma maulidi ya Mtume wetu Mpenzi s.a.w. na kuwaombea duwa wazee wetu waliowania Uhuru wetu, walio tangulia mbele ya haqi na waliohai nasi. Sherehe hizi zilifanyika katika zaidi ya mitaa kumi na tano Nchini kote.



Pia waliwaombea duwa viongozi wetu, wa Sirikali na wa vyama vyote viliomo Nchini. Bali pia waliiombea duwa Nchi yetu kwa jumla, na khasa kumuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu Subhaanahu wa Taáala atuondolee mfarakano na kutupa uwezo na tawfiiq ya kujenga Umoja baina yetu kwa maslaha ya Nchi yetu na vizazi vyetu. Alhamdulillah, kila ishara inathibitisha kwamba Wazanzibari tumo khatuwa na khatuwa katika kubomowa mfarakano na kujenga Umoja baina yeetu, wajibu shukra kwa kila hali na kila wakati kwa neema hii kuu.



Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu Subhaanahu wa Taáala atuzidishie tawfiiq kwa kila kheri kwa Nchi yetu na vizazi vyetu, Aamyn.



Wa Billahi Tawfiiq



Umoja wa Wazalendo

Zanzibar

April 07, 2009
 
Kujuwa nini kilitokea siku ya mauwaji kwa jina jingine mapinduzi na kina nani walikuwa wakifanya hayo mapinduzi utagunduwa hawakuwa wazanzibari angalia hii clips mpaka mwisho kupata picha yenyewe hasa naimani wengi tutakuja na maoni kuhusiana na kilichotokea sikiliza kiswahili kinacho zungumzwa humo

...haijalishi kama kiswahili hicho kilikuwa cha kipemba au cha kinyamwezi, Mapinduzi pekee ndiyo yaliyoikomboa Zanzibar toka kwenye utawala dhalimu wa Kisultani.

Huo uhuru mnaouzungumzia haukuwa kwa manufaa ya wazanzibari wote, bali kwa utawala wa ki Sultani toka Oman, pamoja na waarabu wachache.
 
..Waafrika hawakuutambua "uhuru" wa mwaka 63, ndiyo maana wakafanya MAPINDUZI.
 
..Waafrika hawakuutambua "uhuru" wa mwaka 63, ndiyo maana wakafanya MAPINDUZI.

Nawe usipotoshe mambo zaidi. Ni Wazanzibar iambao hawakuutambua uhuru bandia. Hao ndio waliofanya harakati za kuleta Mapinduzi. Kama Waafrika walikuwemo katika uwanja wa kivita basi ilikuwa ni kama watu wa kusaidia tu-inawezekana kuwa walikodiwa- huwezi kujua.
 
NCCR wamechemsha maana 1963 Uhuru wenyewe nchi iliendeshwa na Sultan, (actually Uhuru halisi wa Zenj ulikuja baada ya Karume kufa - April 7th)(yes i kno wengine mtakasirika kusikia hiyo...)
 
NCCR wamechemsha maana 1963 Uhuru wenyewe nchi iliendeshwa na Sultan, (actually Uhuru halisi wa Zenj ulikuja baada ya Karume kufa - April 7th)(yes i kno wengine mtakasirika kusikia hiyo...)
Unaingia mwenyewe kundini! ....kundi la vinibu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom