Ng'wanamalundi
JF-Expert Member
- Feb 4, 2008
- 1,165
- 1,361
NCCR Mageuzi wataka siku ya uhuru wa Zanzibar
Fidelis Butahe
CHAMA cha NCCR-Mageuzi, kimeibuka na hoja mpya ya kutaka kutambuliwa kwa siku ya uhuru wa Zanzibar ,kama ilivyo kwa siku ya uhuru wa Tanganyika.
Chama hicho kimeelezea matumaini yake kuwa kwa pendekezo hilo, serikali itaona umuhimu wa kuifanya Desemba 9 kuwa siku ya Uhuru wa Tanganyika na Desemba 10 kuwa siku ya uhuru wa Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mkuu wa idara ya organaizesheni na uenezi ya chama hicho, Faustin Sungura alisema hiyo inatokana ukweli kwamba nchi hizi, zilipata uhuru Desemba, za miaka tofauti.
"Tanganyika ilipata uhuru wake Desemba 9 mwaka 1961 na Zanzibar ilipata uhuru wake Desemba 10 mwaka 1963 watu wanaposheherekea miaka 45 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, watengenishe mambo mawili yanayofanywa kuwa jambo moja ambayo ni uhuru na mapinduzi," alisema.
"Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar zinatuambia kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika Januari 12, 1964",
"Mapinduzi haya yanatualika katika umoja wetu kwa maslahi ya ustawi wa historia ya Zanzibar, kujua kama kabla ya mapinduzi ya mwaka 1964 Zanzibar ilikuwa tayari imeshajipatia uhuru au la, na kama Zanzibar haikuwa imepata uhuru iliwezekana vipi yakafanyika mapinduzi kwenye nchi ambayo haikuwa huru" alisema Sungura
Sungura alisema kuwa mwaka 1961 Zanzibar kulifanyika uchaguzi mara mbili ambapo mara ya kwanza, vyama vya siasa vya ASP, ZNP na ZPPP vilivyoshiriki katika uchaguzi huo, havikutoa mshindi licha ya matokeo kuonyesha kuwa ASP ilipata kura 10 na ZNP kura 9.
"Katika uchaguzi wa pili wa Juni 1961 machafuko makubwa yalitokea ambapo watu 48 walikadiriwa kupoteza maisha na wengine 400 kujeruhiwa, Julai 8 mpaka 11, 1963 kulifanyika uchaguzi mwingine ambapo vyama vya ZNP na ZPPP viliungana na kupata viti 18 ambapo ASP ilipata 13",
"Septemba 20 mpaka 24, 1963 ulifanyika mkutano nchini Uingereza ambapo pia ulijadili katiba ya Zanzibar, lakini Desemba 10, 1963 ndiyo siku ambayo Zanzibar, ilipata uhuru wake kutoka kwa mkoloni wa Kiingereza" alisema Sungura
Alisema baada ya Zanzibar kupata uhuru, Seyyid bin Thuweni, ikiwa Sultan na mkuu wa nchi alingolewa madarakani Januari 12, 1964 baada ya kufanyika kwa mapinduzi.
Sungura alisema kutokana na historia inavyoonyesha umefikia wakati Tanzania ikisheherekea uhuru Zanzibar nayo isheherekee siku yao ya uhuru kama ilivyo kwa Tanzania.
Mimi nadhani hatuna budi kuchagua siku moja tu: ama kuitambua siku ya tarehe 10 Desemba 1963 au siku ya tarehe 12 Januari 1964. Kwa ufahamu wangu "uhuru" uliopewa Zanzibar hiyo tarehe 10 Desemba 1963 ulikuwa batili. Siyo uhuru wa kwelikweli. Ndiyo maana yakafanyika mapinduzi. Kama tutasherehekea tarehe 10 Desemba kama siku ulipopatikana uhuru wa Zanzibar, itakuwa sawa na kusema kwamba mapinduzi yaliyofuatia hayakuwa halali. Kwa hiyo hakuna maana kusherehekea mapinduzi ya tarehe 12 Januari 1964. Maoni yangu ni kwamba tuendelee na kusherehekea tarehe 9 kama siku ya uhuru wa Tanganyika; tarehe 12 Januari kama siku ya Mapinduzi (kuzaliwa uhuru wa kweli) wa Zanzibar; na tarehe 26 Aprili kama siku ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar (siku ya kuzaliwa Tanzania).