Uhuru na Mapinduzi ya Zanzibar

Wapo wengi karume aliowaua
Asp wenziwe - Twala, Mdungi Ussi, Sadalla, Othman Sharif
 
Tukiangalia bila kupenda sana, mwenye kupenda sana, chongo huita kengeza. Tanganyika kabla ya uhuru wake, ilitawaliwa na Mwingereza na Zanzbar ilitawaliwa na Sultani Jamshidi ambaye utawala wake ulilindwa na Uingereza.

Utawala wa Mwingereza uliondoa utawala wake Tanganyika kwa maana ya bendera Desemba 9, 1961.

Tukafurahi sana kuwa tumepata uhuru. Lakini, ukweli ingawa Tanganyika ilikuwa huru siku ile, ilikuwa na Waziri Mkuu tu chini ya Malkia wa Uingereza.

Uhuru wa kweli kwa maana ya kujitawala wenyewe kwa Tanganyika, ilikuwa ni ilie siku ya Desemba 9, 1962 tulipoondokana na Malkia wa Uingereza na kuwa Jamhuri ya Tanganyika.

Na kwa Zanzibar ilikuwa vivyo. Ingawa bendera ya Mwingereza ilishushwa ile Desemba 10 1963 na Zanzibar ikapata Waziri wake Mkuu, lakini bado huyo alikuwa chini ya mamlaka ya Sultani kama vile Tanzania huru ilivyokuwa chini ya mamlaka ya Malkia wa Uingereza. Uhuru wa kweli ulipatikana Zanzibar siku ile ambayo alikimbilia Uingereza Januari 12, 1964.

Ingawa Sultani wa Zanzibar wakati huo alikuwa si Sultani wa Oman, lakini bado hakuwa pale kwa ridhaa ya Wazanzibari bali alikuwa pale akiendeleza matunda ya Himaya ya Sultani wa Oman kwa maana ya kizazi chake. Si mtu mwingine yeyote ambaye angeweza kuwa Sultani wa Zanzibar hata mpaka kufikia leo. Bado ulikuwa ni ukoloni mamboleo. Njia pekee waliyokuwa nayo Wazanzibari kujipatia uhuru wao wa kweli ilikuwa ni hiyo ya mapinduzi.

Sishangilii umwagaji damu wa aina yoyote ile, lakini wakati huo huo, sishangilii ukoloni wa aina yoyote ile, hali kadhalika.

Sasa basi, kwa kuwa Tanganyika inashangilia uhuru wake chini ya Malkia wa Uingereza kila Desemba 9, sioni sababu kwa nini Zanzibar isipate nafasi ya kuadhimisha siku ya uhuru wake chini ya Sultani hiyo Desemba 10. Yaliyobaki ni historia, hayawezi kufutika.
 
Kama ulikuwa hujuwi basi ni Wazanzibari wenyewe ndio waliomtunuku ufalme Sayyid Said la kwanza, na lapili katika mkutano wa mwisho kabla ya uhuru vyama vyote vilikubaliana kwamba mfalme aendelee japokua Umma Party walikubali shingo upande, na huyo mfalme alikuwepo kikatiba kwa maana hiyo bunge lingeweza kumuondoa kama wangekuwa hawamtaki.
 
Na ASP ilipata viti 13 kati ya 31 na kama kweli wazanzibari walikuwa hawamtaki mfalme basi kwa sera hii tu ya kutokumkubali mfalme ingeweza kuwapa wao ushindi tena wa kishindo.
 
dos.2020,

..ASP walipata kura nyingi kulinganisha na vyama vingine. viti 13 walivyopata havitoi picha kamili ya kilichotokea ktk chaguzi kama 3 zilizofanyika Zanzibar kabla ya uhuru wa bandia wa 1963.

..kitendo cha Muingereza kumpa madaraka Sultani ambaye utawala wake una asili ya biashara ya utumwa wa Waafrika ulikuwa ni tusi kubwa sana kwa Waafrika wa Zanzibar na bara zima la Afrika.
 
Kwamichi wacha kupotosha watu, Zanzibar haikuwahi kutawaliwa hata siku moja ,na halafu wapi uliona kuwa Sultani huchaguliwa au kila baada ya muda fulani unachaguliwa ukoo mwengine kuwa wa Kisulatani ,wapi umeona hata kwenye hadithi za Abunuwasi au Bulicheka hakuna mbadilishano.

Uhuru wa Zanzibar ndio huo huo hakuna Uhuru mwengine ,huo wa Mapinduzi huwezi kusema ni Uhuru ,hivi unajua ni nani aliepinduliwa ? Vile vile unaelewa ni nani aliepindua ? Maana hata Karume hayumo katika waliopanga Mapinduzi sasa bora ukae kimya kuliko kuwa na mshiko wa hadithi wa ncha saba ,wakati huijui ncha ipi ipo sahihi.
 
Mwiba said:

Mwiba,

..kabla Sultani hajajipachika utawala wa Zanzibar, visiwa hivyo vilikuwa ni ardhi ya Waafrika.

..mimi nadhani tatizo lenu hamuwatambui Waafrika kama binadamu kamili kama walivyo Waarabu.

..Mapinduzi yalifanywa na Waafrika kukomboa nchi ya wahenga wao toka kwa utawala wa Sultani wa Kiarabu.
 
Si kweli hizo ni kasumba tu,ukweli mnaukwepa maana ipo sababu ya Sultani kuwepo Zanzibar ,sasa kitu gani kinachowaogopesha kuusema ukweli huo ndio sielewi ,Sultani hakupinduliwa kama ambavyo mnataka ikubalike,Ni kweli Sultani alikimbia lakini iliopinduliwa ni Serikali ya Zanzibar Huru.Maana hao mnaosema kuwa walipindua walishiriki katika chaguzi za mwanzo.
Sasa ni nani alipanga Mapinduzi ? Hilo nalo mnatakiwa mlijibu na mlifahamu kwa kina sio mnavamia tu kama mnaosoma hadithi za Abunuwasi na wewe ukawakuta wasiojua kusoma ukawatolea.Ndio mnavyokwenda.
 
..Zanzibar maana yake ni NCHI YA WATU WEUSI -- WAAFRIKA.

..sasa iweje mtawala wa mtu mweusi awe Sultani mwenye asili ya Oman?

..wanaotaka kuhalisha Usultani mwisho wake watahalalisha hata biashara ya Utumwa.
 
dos.2020,

..ASP walipata kura nyingi kulinganisha na vyama vingine. viti 13 walivyopata havitoi picha kamili ya kilichotokea ktk chaguzi kama 3 zilizofanyika Zanzibar kabla ya uhuru wa bandia wa 1963.

..kitendo cha Muingereza kumpa madaraka Sultani ambaye utawala wake una asili ya biashara ya utumwa wa Waafrika ulikuwa ni tusi kubwa sana kwa Waafrika wa Zanzibar na bara zima la Afrika.

Hili ndio tatizo lenu, mnapozungumzia utumwa mnazungumza kama utumwa huo ulifanya na waarabu tu (yani waislamu) na ulifanyika Zanzibar tu. Utumwa ulikuwepo dunia nzima na hao wazungu wao walikuwa ndio waendeshaji wakubwa wa hiyo biashara. Na Zanzibar ilikuwa ndio nchi ya mwanzo Africa Mashariki kupiga marufuku biashara hiyo na Tanganyika ikiwa ndio ya mwisho chini ya utawala wa Kijerumani.

Na biashara hiyo hawakuwa wafalme wakijihusisha, ilikuwa ni biashara ya watu binafsi isipokuwa wafanya biashara hao walikuwa wakitakiwa kulipa kodi. na kwa kipindi hicho biashara hii ilikuwa halali dunia nzima. Na wala hakukuwa na mzanzibari yoyote ambaye alikuwa mtumwa, kwa kweli watumwa walikuwa wakitokea Tanganyika na Uganda na sijapata kukusikieni mkiwataja ma chief kwani wao ndio waliokuwa wakikamata watu na kuwauzia hao waarabu.
 
dos.2020 said:

..kama Sultani alikuwa akikusanya kodi kutokana na biashara ya Watumwa basi ana hatia sawa na wakamataji Watumwa.

..zaidi utawala wa Sultani ulioshamiri kutokana na biashara ya utumwa ulipaswa kusitishwa pale biashara hiyo ilipopigwa marufuku Afrika Mashariki.

..Zanzibar maana yake ni NCHI YA WATU WEUSI -- WAAFRIKA.

..sasa iweje mtawala wa mtu mweusi awe Sultani mwenye asili ya Oman?

NB:

..nadhani tatizo lako wewe humtambui Mwafrika kama mwanadamu kamili sawa na hao Waarabu wa Oman. ndiyo maana unaona ni halali kwa Zanzibar nchi ya watu weusi kuwa chini ya mamlaka ya Sultani toka Oman.
 
Mwiba,

..kabla Sultani hajajipachika utawala wa Zanzibar, visiwa hivyo vilikuwa ni ardhi ya Waafrika.

..mimi nadhani tatizo lenu hamuwatambui Waafrika kama binadamu kamili kama walivyo Waarabu.

..Mapinduzi yalifanywa na Waafrika kukomboa nchi ya wahenga wao toka kwa utawala wa Sultani wa Kiarabu.

waafrika gani hao unaowazungumzia wewe? wengi wao walikuja kama watumwa ZNZ na wengine walikuja wakikimbia kodi za vichwa makwao na ugumu wa maisha.
Au unawazungumzia washirazi? nafikiri unajua kwamba Mohamed Shamte Al-Shiraz ndio aliye kuwa waziri mkuu Baada ya Uhuru. na baada ya mapinduzi si Karume, Jumbe wala Mwinyi ambao walikuwa ni washirazi
 
dos.2020,

..Mohamed Shamte alikuwa kibaraka tu Sultani. ndiyo maana serikali yake pamoja na Sultani wake wakafurumushwa.
 
waafrika gani hao unaowazungumzia wewe? wengi wao walikuja kama watumwa ZNZ na wengine walikuja wakikimbia kodi za vichwa makwao na ugumu wa maisha.
Au unawazungumzia washirazi? nafikiri unajua kwamba Mohamed Shamte Al-Shiraz ndio aliye kuwa waziri mkuu Baada ya Uhuru. na baada ya mapinduzi si Karume, Jumbe wala Mwinyi ambao walikuwa ni washirazi

...naam, naaam, naaam, 'wandengereko' kutokana na utumwa wao kifikra, waliyanunua hayo majina ya ukoo,...kina Al-Alawi, Al-Mansoor, Al-Mashhoor, Al-Kindi... yote katika kujikweza waonekane 'waarabu'... :)
 
dos.2020 said:
Kwa hivyo karibu nusu ya nchi walikuwa vibaraka wa Sultan?

dos.2020,

..idadi ya viti walivyoshinda ASP inaficha support kubwa na wingi wa kura walizopata.

..ndiyo maana nikakwambia tuletee matokeo ya kura kwa chaguzi zile 3[kama sikosei] kabla ya Mapinduzi uone dhuluma waliyocheza Sultani na vibaraka wake.

..hakuna Mangi anatawala nchi yoyote ile ya Kiarabu, kwanini Sultani atawale nchi ya Waafrika?
 
ASP walipata kura 53% huku ZNP/ZPPP wakipata 47%. na hiyo dhulma ni dhulma gani? utaratibu ulikuwa unajulikana kwamba chama kitakachopa viti vingi ndicho kitakacho unda serekali sasa taatizo lilikuwa nini? kwanini wasipinge kabla ya chaguzi?
 
waafrika gani hao unaowazungumzia wewe? wengi wao walikuja kama watumwa ZNZ na wengine walikuja wakikimbia kodi za vichwa makwao na ugumu wa maisha.
Au unawazungumzia washirazi? nafikiri unajua kwamba Mohamed Shamte Al-Shiraz ndio aliye kuwa waziri mkuu Baada ya Uhuru. na baada ya mapinduzi si Karume, Jumbe wala Mwinyi ambao walikuwa ni washirazi
Dos 2. nafikiri sijui waongea nini wewe . Hiyo ni historia . wacha tu. Lakini kama darsa haya twende- Washirazi ndio wenyewe Nchi- Waafrika walikuwepo lakini walichanganyika na wageni ( kila ajae) . Sasa kwa zama za leo tuwe na Mzanzibari. Nashangaa hivi sasa hivi mtu unapiga debe la Uafrika na Zanzibar. Pale hakuna Mwaafrika
na hakuna pia Mwarabu wala Mngazija. Pale kuna Mzanzibari. Namsifu Seif (Hamad) kwa kupigia debe U-Zanzibari. Sasa hao CCM wenzangu ambao bado wanaiimba Uafrika -siwaelewi.
 
dos.2020,

..idadi ya viti walivyoshinda ASP inaficha support kubwa na wingi wa kura walizopata.

..ndiyo maana nikakwambia tuletee matokeo ya kura kwa chaguzi zile 3[kama sikosei] kabla ya Mapinduzi uone dhuluma waliyocheza Sultani na vibaraka wake.

..hakuna Mangi anatawala nchi yoyote ile ya Kiarabu, kwanini Sultani atawale nchi ya Waafrika?
.
JOKA na hakuna Muafrika yoyote yule ambaye atakuwa na haki ya kutawala Zanzibar- Isipokuwa Mzanzibari. Sasa Nilikuomba hiyo definition ya Mzanzibari bado hujanipa.
 
Back
Top Bottom