Uhuru na Habari leo yamekuwa magazeti ya udaku?

makoye2009

makoye2009

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
2,644
Likes
499
Points
280
makoye2009

makoye2009

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
2,644 499 280
Leo wakti nasikiliza vichwa vya habari vya magazeti nikasikia Gazeti la Uhuru linasema,"TUNDU LISSU ASHUSHULIWA''. Gazeti la Mwananchi likajinadi kwa kichwa cha habari ''TUNDU LISSU NA MNYIKA WAMPA SPIKA ANNE MAKINDA WAKATI MGUMU''.

Habari inayozungumziwa hapa ni kile kilichotokea jana Bungeni wakti wa mchakato wa kumpata PM mteule na Naibu wa Spika. Kwa mtu makini anayefuatilia kile kinachoendelea Bungeni hawezi kuandika kichwa cha habari cha kipuuzi kama hicho kilichoandikwa na Mhariri wa gazeti la Uhuru. Hapa ndipo mtu unajua ni kwanini gazeti la Mwananchi lilitaka kufungiwa kwa kuandika ukweli ili hawa wanaoandika uongo waendelee kudanganya watu.

Kichwa sahihi cha matukio ya jana ni cha Gazeti la Mwananchi. Kwa hiyo Mhariri wa gazeti la Uhuru anataka kuwadanganya Watanzania hasa wasiokuwa na TV na radio wasioweza kufuatilia kwa karibu. Huu ni uongo ambao hauwezi kukubalika kwa jamii ya Watanzania. Hii imekuwa ni tabia ya Magazeti yote yanayomilikiwa na CCM na Serikali yake kuandika habari zinazopotosha ukweli au uhalisia wa matukio kama yalivyo.

Ndiyo maana mimi sisomi Uhuru,Mzalendo,Habari Leo,Daily Noise(News) maana haya ni sawa na vijigazeti vya UDAKU kama Kasheshe,Ijumaa,Sani n.k.Angalia lugha iliyotumika,KUSHUSHUA, lugha ambazo tunazisikia kwenye vijiwe,kitchen party au send off za kina mama. Uhuru acheni hizo, hebu badilikeni.Kumbukeni mnatumia fedha za walipa kodi kuchapisha hayo magazeti kuna siku tutawauliza kwa kuchapisha magazeti yasiyonunulika kwa kuandika mambo ya Udaku badala ya kuwahabarisha Watanzania.

HIVI BARAZA LA HABARI mnautaratibu gani wa kuwashughulikia watu wanaoandika habari zenye kupotosha umma? Hebu liangalieni hili.
 
BABA JUNJO

BABA JUNJO

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2010
Messages
241
Likes
0
Points
0
BABA JUNJO

BABA JUNJO

JF-Expert Member
Joined Nov 9, 2010
241 0 0
Unajua kuna tatizo la Ushabiki wa vyama wala si uzalendo. Mwandishi wa UHURU ni shabiki wa CCM. Sasa kwa ushabiki huu nchi hatutaijenga kwani mwenye fito atsema zake na mwenye kamba atasema zake na nyumba itasimama kujengwa. Tuache ushabiki jamani tujenge nchi yetu.
 
Kituko

Kituko

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2009
Messages
9,538
Likes
7,407
Points
280
Kituko

Kituko

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2009
9,538 7,407 280
Unajua kuna tatizo la Ushabiki wa vyama wala si uzalendo. Mwandishi wa UHURU ni shabiki wa CCM. Sasa kwa ushabiki huu nchi hatutaijenga kwani mwenye fito atsema zake na mwenye kamba atasema zake na nyumba itasimama kujengwa. Tuache ushabiki jamani tujenge nchi yetu.
hapo sidhani kama kuna Tatizo, hilo ni gazeti la CCM officially kwa hiyo sio raisi hata siku moja ukakuta wakikisifia chama chochote ama mtu yoyote kutoka Chadema, Tatizo lipo kwa magazeti ya serikali na vyombo vingine vya habari ambazo vinapaswa kuwa neutral, lakini uhuru wako sahihi
 
awesome

awesome

Member
Joined
Oct 11, 2010
Messages
37
Likes
0
Points
0
awesome

awesome

Member
Joined Oct 11, 2010
37 0 0
Kitambo sana watu wengi wanatambua hilo kwamba vyombo vya habari vya umma vimekuwa vikiroipoti habari ambazo si za kujenga bali za muchochezi na ushabiki wa vyama, jambo ambalo si jema kwa uandishi au utoaji wa habari kwa umma.

Kuna watu kadhaa kama Marin Hassan wa TBC1, mhariri wa gazeti la The Daily News na wengine wengi hawapaswi kufanya kazi katika vyombo vya umma bali wakatangaze au kuandika magazeti ya udaku ya kitaa.
 
NewDawnTz

NewDawnTz

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Messages
1,675
Likes
6
Points
0
NewDawnTz

NewDawnTz

JF-Expert Member
Joined Nov 15, 2010
1,675 6 0
Mimi wala sina tatizo na uhuru maana ni gazeti la walewale wenye upeo wa kufikiria kama kunguni. Ila hili habari leo ambalo ni la serikali ndo linanipa mamoto hasa ninapogundua mapuuuzi haya yanaishi kwa kodi yangu ninayofyekwa kwenye mshahara wngu kila mwezi. Yananipa hasira kweli na nilishaamua kutokuyasoma toka long-time ago nilipogundua yanakula kodi zangu na kuandika upuuzi wenye kulibeba kundi fulani.

Nadhani habari leo na Daily News waondoke huko na warudi kwenye mstari kuwasemea wananchi wanaowalipa kwa kodi zao
 
W

We can

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2010
Messages
681
Likes
5
Points
35
W

We can

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2010
681 5 35
Uhuru wako sahihi! Sema jina la Gazeti lao ndo limekaa vibaya!
 
K

KERENG'ENDE

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2010
Messages
398
Likes
2
Points
35
K

KERENG'ENDE

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2010
398 2 35
Habari leo and daily news you don't need to be bias, political biasness will distort our national unit. Please leave such unbalanced information to Uhuru news paper
 
M

Mkorosai

Member
Joined
Nov 17, 2010
Messages
65
Likes
0
Points
0
M

Mkorosai

Member
Joined Nov 17, 2010
65 0 0
Uhuru wako sahihi! Sema jina la Gazeti lao ndo limekaa vibaya!
Hawako sahihi hata chembe. Uhuru linatakiwa kubaki kuwa gazeti tena la kuaminika hata kama limeegemea upande wa cCM. Hivi kama wangelipoti habari ile kwa usahihi, CCM au Spika wangeku wamepungukiwa nini?

Nawashauri waache kudanganya na kupotosha kila kitu maana siku moja watapotosha kitu kitakacho athiri nchi yetu halafu waje wajutie
habari zao.
 
M

mchakachuaji1

Senior Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
122
Likes
4
Points
35
M

mchakachuaji1

Senior Member
Joined Nov 4, 2010
122 4 35
Leo wakti nasikiliza vichwa vya habari vya magazeti nikasikia Gazeti la Uhuru linasema,"TUNDU LISSU ASHUSHULIWA''. Gazeti la Mwananchi likajinadi kwa kichwa cha habari ''TUNDU LISSU NA MNYIKA WAMPA SPIKA ANNE MAKINDA WAKATI MGUMU''.

Habari inayozungumziwa hapa ni kile kilichotokea jana Bungeni wakti wa mchakato wa kumpata PM mteule na Naibu wa Spika. Kwa mtu makini anayefuatilia kile kinachoendelea Bungeni hawezi kuandika kichwa cha habari cha kipuuzi kama hicho kilichoandikwa na Mhariri wa gazeti la Uhuru. Hapa ndipo mtu unajua ni kwanini gazeti la Mwananchi lilitaka kufungiwa kwa kuandika ukweli ili hawa wanaoandika uongo waendelee kudanganya watu.

Kichwa sahihi cha matukio ya jana ni cha Gazeti la Mwananchi. Kwa hiyo Mhariri wa gazeti la Uhuru anataka kuwadanganya Watanzania hasa wasiokuwa na TV na radio wasioweza kufuatilia kwa karibu. Huu ni uongo ambao hauwezi kukubalika kwa jamii ya Watanzania. Hii imekuwa ni tabia ya Magazeti yote yanayomilikiwa na CCM na Serikali yake kuandika habari zinazopotosha ukweli au uhalisia wa matukio kama yalivyo.

Ndiyo maana mimi sisomi Uhuru,Mzalendo,Habari Leo,Daily Noise(News) maana haya ni sawa na vijigazeti vya UDAKU kama Kasheshe,Ijumaa,Sani n.k.Angalia lugha iliyotumika,KUSHUSHUA, lugha ambazo tunazisikia kwenye vijiwe,kitchen party au send off za kina mama. Uhuru acheni hizo, hebu badilikeni.Kumbukeni mnatumia fedha za walipa kodi kuchapisha hayo magazeti kuna siku tutawauliza kwa kuchapisha magazeti yasiyonunulika kwa kuandika mambo ya Udaku badala ya kuwahabarisha Watanzania.

HIVI BARAZA LA HABARI mnautaratibu gani wa kuwashughulikia watu wanaoandika habari zenye kupotosha umma? Hebu liangalieni hili.
Ndugu acha kupoteza muda kuangalia heading za magazeti ya kipumbavu, endelea kutafuta habari za ukweli na uhakika kutoka magazeti ya ukweli yanayozingatia maadili ya uandishi. Hao wapumbavu watakutia ghadhabu kila siku urudi home una hasira mkuu.
 
emmathy

emmathy

Senior Member
Joined
Sep 22, 2010
Messages
147
Likes
11
Points
35
emmathy

emmathy

Senior Member
Joined Sep 22, 2010
147 11 35
Kwa mtazamo wangu magazeti yote yangetangaza interest ( yako upande gani wa chama / serikali) ili wale wananchi wenzetu kule kijijini taratibu waanze kuelewa kila gazeti linapoandika linalenga nini..Wengine hawaelewi wanasema serilkali imesema kupitia gazeti wakati inawezekana kwa interest ya wachache na wala si serkali iliyosema matokeo yake watu wanaamini kitu ambacho si cha kweli...
Je tundu lisu ameshushuliwa au amefafanuliwa vifungu vinasema nini au amebaniwa kama mwanzo wa ishara zakuzima moto utakao washwa?
 
Limbani

Limbani

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Messages
1,440
Likes
101
Points
160
Limbani

Limbani

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2008
1,440 101 160
Kila siku asubuhi Makamba anaamka na kusoma UHURU na HABARI LEO!! Siku moja nilimsikia mhariri mtendaji wa gazeti la UHURU ni dada mmoja mrembo na ameenda shule lakn nilimuonea huruma maana inabidi taaluma yake aiweke pembeni ili awapendeze akina Makamba na John Komba!!

Ukiacha waandishi uchwara wagangia tumbo kama kina Mkumbwa Ally (sijui kwa nn hajiungi Uhuru na Mzalendo) na kina dada kama dada yangu mmoja alikuwa anaitwa Janeth chakula cha wazee wapo waandishi ambao kwa kweli hawana jinsi na hasa kwenye Habari Leo (Nawajua wengi ambao inabidi waandike tu anavyotaka Mhariri).

Ni sawa gazeti liwe na mwelekeo wa kichama au kiitikadi lakini sio kupotosha habari!! wangekuwa wastaarabu na wangeheshimika zaidi kama wasingeandika habari ya Tundu Lissu bungeni KULIKO KUIANDIKA KATIKA MWELEKEO TOFAUTI WAKATI KARIBU YA WASOMAJI WOTE WA MAGAZETI WALIKUWA KWENYE RUNINGA JANA NA KUONA NI NINI KILICHOTOKEA.

SHAME ON YOU HABARI LEO AND DAILY NEWS EDITORS!!!!
 
VoiceOfReason

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
5,234
Likes
59
Points
0
VoiceOfReason

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
5,234 59 0
hizi gazeti hata hazifai kufungia maandazi:A S angry:
 
Forum statistics

Threads 1,238,833
Members 476,196
Posts 29,333,230