Uhuru Kenyatta kurudi kama Waziri Mkuu wa Kenya 2022

game over

JF-Expert Member
Jan 1, 2016
10,357
23,149
Serikali ya Jubilii inapanga kupitisha mchakato wa kukusanya Maoni ili kurejesha Nafasi ya Waziri mkuu.

Ikumbukwe kuwa Baada ya Handshakes na BBI sasa ni Wazi Uhuru yupo Karibu na inaonesha wazi kumuunga mkono RAO na yeye atakuwa waziri wake Mkuu.
The Cycle continues, Baada ya hawa sasa itakuwa ni zamu ya kina Muhoho na Gideon

PRESIDENTS.jpg

=======

Rais wa Kenya akataa kufuta uwezekano wa kurudi kama Waziri Mkuu

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekataa kufutilia mbali uwezekano kwamba wadhfa wa waziri mkuu huenda ukabuniwa katika kura ya maoni ijayo kama njia ya kumfanya kuwa na madaraka hata baada ya muda wake wa kikatiba wa mihula miwili kama rais kukamilika.

Bwana Kenyatta anaachilia madaraka 2022. Katika mahojiano na gazeti la Financial Times, rais Uhuru alikataa kuzungumzia kuhusu 'nyadhfa za kisiasa ambazo hazipo'.

Hatahivyo alisema waziwazi kwamba hatosalia kuwa rais baada ya kukamilika kwa mihula yake miwili, akisema kwamba katiba na watu wa Kenya wako wazi kuhusu suala hilo.

''Wakenya wanaelewa kuhusu mihula miwili ya urais tangu 2002, wakati ilipoanza kutekelezwa . Hakuna rais hata mmoja aliyevunja sheria hiyo . Na sina nia kuwa rais wa kwanza kufanya hivyo'', alisema.

Rais amesema kwamba Kenya itaandaa kura ya maoni hivi karibuni, kulingana na yeye ili kubadilisha baadhi ya vifungu vya katiba ukweli ambao pia walioitengeneza wanakubaliana nao.

Pia alizungumzia wasiwasi kuhusu biashara huru inayojadiliwa kati ya Kenya na Marekani , akisema yatakuwa majadiliano ya usawa licha ya tofauti ya kiuchumi na kisiasa ya mataifa hayo mawili.

Mashirika mengi ya wanaharakati , ambayo yanadai kwamba makubaliano hayo ya kibiashara yatakuwa mabaya kwa uchumi wa Kenya , yalituma ujumbe wa kupinga chini ya alama ya reli #NoToKenyaUSFTA.

Bwana Kenyatta pia alikuwa na ujumbe kwa wale wanaoshiriki katika maandamano ya Black Lives Matter nchini Marekani na duniani kwa jumla : All Lives Matter , lakini hakufai kuwa na ukandamizaji wa kundi lolote katika jamii''.

Je, ni nini kinachoendelea kati ya Kenyatta na naibu wake?
Tangu naibu wa rais William Ruto kuanza kampeni za mapema kugombea urais 2022, changamoto kuu ya bwana Kenyatta imekuwa iwapo atamaliza muhula wake wa pili kama kiongozi ambaye alifeli kutimiza ahadi zake kwa Wakenya.

Ili Kutekeleza ajenda yake ya masuala manne makuu serikalini, rais Kenyatta alimtangaza Waziri wa Usalama wa ndani, Dkt Fred Matiangi kama mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji wa maendeleo na mawasiliano katika baraza la mawaziri, hatua inayomzuia naibu wa rais katika kukagua miradi ya serikali.

Lakini la kushangaza ni kwamba uteuzi huo ulimpatia Matiangi uwezo mkubwa wa kusimamia miradi yote ya serikali.

Kwa miezi kadhaa , naibu huyo hajakuwa akihudhuria hafla za rais katika Ikulu ya rais na pia amekosa kushirikishwa katika mikutano ya baraza kuu la usalama ambapo yeye ni mwanachama.

Wakati mmoja naibu huyo wa rais alisikika akisema kwamba kuna njama ya kumzuia kumrithi rais Uhuru Kenyatta na 'mfumo'.

Naibu huyo alinukuliwa mnamo mwezi Machi mwaka huu ,akisema kwamba mfumo huo bila kutoa ushahidi ulikuwa unapanga njama dhidi yake.

''Wale walio katika mfumo huo wanajigamba kwamba sitakuwepo hivi karibuni'', naibu huyo aliandika katika mtandao wake wa Twitter.

''Na kwasababu mfumo huo hauwezi kumchagua mtu yeyote, unaweza kuua. lakini kuna Mungu aliye juu mbinguni'', alimaliza.

Vita dhidi ya Ufisadi
Wakati rais Kenyatta alipoanzisha vita dhidi ya ufisadi, bwana Ruto alidaiwa kuwakosoa wachunguzi na kudai kwamba ilikuwa silaha kuwakabili viongozi wanaodaiwa kuwa karibu naye.

Naibu huyo wa rais na washirika wake walisema kwamba Shirika la uchunguzi wa jinai ambalo lilikuwa linaungwa mkono na rais lilikuwa halina uwezo wa kisheria kuchunguza uhalifu wa kiuchumi na kwamba lilikuwa linafanya siasa.

'Handshake'
Msuguano mwengine kati ya rais na naibu wake ni ule ushirikiano wa raila Odinga na Kenyatta wa tarehe 9 mwezi Machi 2017 ambao ulisaidia kuondoa hofu baada ya uchaguzi wa urais wa 2017.

Rais Kenyatta anasema kwamba hatua hiyo ni miongoni mwa ahadi alizowapatia Wakenya.

Wakati huo, taifa lote lilikuwa limezongwa na hali ya wasiwasi baada ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga, kususia uchaguzi wa marudio ulioagizwa na mahakama ya kilele, ambayo ilikuwa imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi yaliompatia ushindi Kenyatta.

Wachanganuzi wa masuala ya kisiasa nchini Kenya wanasema, HandShake ya Uhuru Kenyatta na William Ruto imekuwa chanzo cha mvutano kati ya wandani wa bwana Ruto na wandani wa Raila, ambao wanadai kwamba ni njama ya bwana Kenyatta kufutilia mbali ahadi yake ya kumuunga mkono Ruto atakayewania urais kupitia chama cha Jubilee 2022.

Wanasema kuwa ,rais Kenyatta anategemea handshake na mradi wa BBI uliozinduliwa mwezi Novemba 2019 kama mojawapo ya mipango ya chama tawala cha Jubilee kuunganisha taifa na kumaliza ghasia ambazo zimekuwa zikitokea kila baada ya uchaguzi.

Mikutano ya BBI
Huku rais Uhuru Kenyatta akisema kwamba BBI ni upanuzi wa wazo la Jubilee kufikia taifa lote, anashangaa ni kwa nini linatiliwa siasa.

Wakosoaji hususan kutoka kwa kambi ya naibu wa rais wanasema kwamba ushirikiano wa Kenyatta na Odinga unaweza kuvunja chama cha Jubilee ambacho rais anasema hayuko tayari kuvunja alichonacho.

''Nataka kupanua kile tulichonacho kwa taifa lote na sitasita kufanya hivyo'',alisema rais. Kabla ya mikutano ya BBI kuzuiwa na mlipuko wa virusi vya corona, bwana Ruto alimshutumu Raila Odinga kwa kuyateka mazungumzo hayo na kuigawanya Jubilee.

Wandani wa naibu wa rais akiwemo Kipchumba Murkomen alikuwa wamesema kwamba kwamba mikutano hiyo imekuwa majukwaa ya kumtusi naibu wa rais William Ruto.

Chanzo: BBC Swahili
 
Siku mbili zilizopita... I am not interested in another term or being the Prime Minister- Uhuru Kenyatta.
 
In Africa It always begin this way, at first they seem to be uninterested, then they come out pretending to respect public opinions,(not really public)
M7 ni mfano mzuri, Mark my words, Uhuru is your next Prime minister. We all know Siasa za Kenya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwahahaaa!!yani eti aww mbunge tena
Kweli mko desperate
 
Naona nyani za Mombasa zime enjoy kutawaliwa na kikuyus and kalenjini za bara kweli nyinyi ni bure kabisa
Km vile wewe unavyonengua kutawaliwa na wasukuma..tena hua unanengua km mota vile..
 
Ndio nikakuuliza awe mbunge tena
Manake waziri mkuu bbi inasema lazima awe mbunge alafu tena afanye kuchaguliwa..
Uhuru huyo sasa

Wewe subiri marekebisho ya sheria yapitishwe ndio utajua atakuwa mbunge tena au atakuwa nani...

Hiyo ni nchi yake bado hajatosheka kuitafuna.
 
Bwahaha!!sasa wewe unajua sana hata kuliko BBI na wakenya..
Hemu nendeni mkamuongezee miaka 20 jiwe
 
Serikali ya Jubilii inapanga kupitisha mchakato wa kukusanya Maoni ili kurejesha Nafasi ya Waziri mkuu.

Ikumbukwe kuwa Baada ya Handshakes na BBI sasa ni Wazi Uhuru yupo Karibu na inaonesha wazi kumuunga mkono RAO na yeye atakuwa waziri wake Mkuu.
The Cycle continues, Baada ya hawa sasa itakuwa ni zamu ya kina Muhoho na Gideon

View attachment 1484220

=======

Rais wa Kenya akataa kufuta uwezekano wa kurudi kama Waziri Mkuu

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekataa kufutilia mbali uwezekano kwamba wadhfa wa waziri mkuu huenda ukabuniwa katika kura ya maoni ijayo kama njia ya kumfanya kuwa na madaraka hata baada ya muda wake wa kikatiba wa mihula miwili kama rais kukamilika.

Bwana Kenyatta anaachilia madaraka 2022. Katika mahojiano na gazeti la Financial Times, rais Uhuru alikataa kuzungumzia kuhusu 'nyadhfa za kisiasa ambazo hazipo'.

Hatahivyo alisema waziwazi kwamba hatosalia kuwa rais baada ya kukamilika kwa mihula yake miwili, akisema kwamba katiba na watu wa Kenya wako wazi kuhusu suala hilo.

''Wakenya wanaelewa kuhusu mihula miwili ya urais tangu 2002, wakati ilipoanza kutekelezwa . Hakuna rais hata mmoja aliyevunja sheria hiyo . Na sina nia kuwa rais wa kwanza kufanya hivyo'', alisema.

Rais amesema kwamba Kenya itaandaa kura ya maoni hivi karibuni, kulingana na yeye ili kubadilisha baadhi ya vifungu vya katiba ukweli ambao pia walioitengeneza wanakubaliana nao.

Pia alizungumzia wasiwasi kuhusu biashara huru inayojadiliwa kati ya Kenya na Marekani , akisema yatakuwa majadiliano ya usawa licha ya tofauti ya kiuchumi na kisiasa ya mataifa hayo mawili.

Mashirika mengi ya wanaharakati , ambayo yanadai kwamba makubaliano hayo ya kibiashara yatakuwa mabaya kwa uchumi wa Kenya , yalituma ujumbe wa kupinga chini ya alama ya reli #NoToKenyaUSFTA.

Bwana Kenyatta pia alikuwa na ujumbe kwa wale wanaoshiriki katika maandamano ya Black Lives Matter nchini Marekani na duniani kwa jumla : All Lives Matter , lakini hakufai kuwa na ukandamizaji wa kundi lolote katika jamii''.

Je, ni nini kinachoendelea kati ya Kenyatta na naibu wake?
Tangu naibu wa rais William Ruto kuanza kampeni za mapema kugombea urais 2022, changamoto kuu ya bwana Kenyatta imekuwa iwapo atamaliza muhula wake wa pili kama kiongozi ambaye alifeli kutimiza ahadi zake kwa Wakenya.

Ili Kutekeleza ajenda yake ya masuala manne makuu serikalini, rais Kenyatta alimtangaza Waziri wa Usalama wa ndani, Dkt Fred Matiangi kama mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji wa maendeleo na mawasiliano katika baraza la mawaziri, hatua inayomzuia naibu wa rais katika kukagua miradi ya serikali.

Lakini la kushangaza ni kwamba uteuzi huo ulimpatia Matiangi uwezo mkubwa wa kusimamia miradi yote ya serikali.

Kwa miezi kadhaa , naibu huyo hajakuwa akihudhuria hafla za rais katika Ikulu ya rais na pia amekosa kushirikishwa katika mikutano ya baraza kuu la usalama ambapo yeye ni mwanachama.

Wakati mmoja naibu huyo wa rais alisikika akisema kwamba kuna njama ya kumzuia kumrithi rais Uhuru Kenyatta na 'mfumo'.

Naibu huyo alinukuliwa mnamo mwezi Machi mwaka huu ,akisema kwamba mfumo huo bila kutoa ushahidi ulikuwa unapanga njama dhidi yake.

''Wale walio katika mfumo huo wanajigamba kwamba sitakuwepo hivi karibuni'', naibu huyo aliandika katika mtandao wake wa Twitter.

''Na kwasababu mfumo huo hauwezi kumchagua mtu yeyote, unaweza kuua. lakini kuna Mungu aliye juu mbinguni'', alimaliza.

Vita dhidi ya Ufisadi
Wakati rais Kenyatta alipoanzisha vita dhidi ya ufisadi, bwana Ruto alidaiwa kuwakosoa wachunguzi na kudai kwamba ilikuwa silaha kuwakabili viongozi wanaodaiwa kuwa karibu naye.

Naibu huyo wa rais na washirika wake walisema kwamba Shirika la uchunguzi wa jinai ambalo lilikuwa linaungwa mkono na rais lilikuwa halina uwezo wa kisheria kuchunguza uhalifu wa kiuchumi na kwamba lilikuwa linafanya siasa.

'Handshake'
Msuguano mwengine kati ya rais na naibu wake ni ule ushirikiano wa raila Odinga na Kenyatta wa tarehe 9 mwezi Machi 2017 ambao ulisaidia kuondoa hofu baada ya uchaguzi wa urais wa 2017.

Rais Kenyatta anasema kwamba hatua hiyo ni miongoni mwa ahadi alizowapatia Wakenya.

Wakati huo, taifa lote lilikuwa limezongwa na hali ya wasiwasi baada ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga, kususia uchaguzi wa marudio ulioagizwa na mahakama ya kilele, ambayo ilikuwa imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi yaliompatia ushindi Kenyatta.

Wachanganuzi wa masuala ya kisiasa nchini Kenya wanasema, HandShake ya Uhuru Kenyatta na William Ruto imekuwa chanzo cha mvutano kati ya wandani wa bwana Ruto na wandani wa Raila, ambao wanadai kwamba ni njama ya bwana Kenyatta kufutilia mbali ahadi yake ya kumuunga mkono Ruto atakayewania urais kupitia chama cha Jubilee 2022.

Wanasema kuwa ,rais Kenyatta anategemea handshake na mradi wa BBI uliozinduliwa mwezi Novemba 2019 kama mojawapo ya mipango ya chama tawala cha Jubilee kuunganisha taifa na kumaliza ghasia ambazo zimekuwa zikitokea kila baada ya uchaguzi.

Mikutano ya BBI
Huku rais Uhuru Kenyatta akisema kwamba BBI ni upanuzi wa wazo la Jubilee kufikia taifa lote, anashangaa ni kwa nini linatiliwa siasa.

Wakosoaji hususan kutoka kwa kambi ya naibu wa rais wanasema kwamba ushirikiano wa Kenyatta na Odinga unaweza kuvunja chama cha Jubilee ambacho rais anasema hayuko tayari kuvunja alichonacho.

''Nataka kupanua kile tulichonacho kwa taifa lote na sitasita kufanya hivyo'',alisema rais. Kabla ya mikutano ya BBI kuzuiwa na mlipuko wa virusi vya corona, bwana Ruto alimshutumu Raila Odinga kwa kuyateka mazungumzo hayo na kuigawanya Jubilee.

Wandani wa naibu wa rais akiwemo Kipchumba Murkomen alikuwa wamesema kwamba kwamba mikutano hiyo imekuwa majukwaa ya kumtusi naibu wa rais William Ruto.

Chanzo: BBC Swahili
1592688322556.png

Punguza jazba jomba, kunwa maji kwanza umeze hilo povu lisije lika kukaba koo..
Miaka mitano tu tayari mshaitwa wapiga dili
Sasa ni rasmi wakenya mmepata sababu ya kutokutawaza baada ya maji kuadimika Kenya nimeona video ya mama akichapa mtoto viboko baada ya kutumia maji chooni ,mama analalama ni maji ya kunywa tehtehteeeee
Slums za Kenya vs kambi za wakimbizi ,jiandae kwa huo Uzi
 
Slums ndio level yenu
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom