Uhuru Kenyatta azindua sarafu mpya za Kenya ambazo hazina picha za marais

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
RAIS Uhuru Kenyatta leo Jumanne, Desemba 11, 2018 ameliongoza taifa kuzindua sarafu mpya za Kenya za thamani za Sh 1, Sh 5, Sh 10 na Sh 20, zilizozingatia vigezo vya Katiba ya sasa ya nchi hiyo iliyozinduliwa mwaka 2010, ambazo zimeanza kutumika rasmi leo.

lehe.jpg

Akizungumza wakati wa shughuli hii iliyofanyika katika makao makuu ya Benki Kuu nchini (CBK), jijini Nairobi, Kenyatta amesema sarafu hizo hazitakuwa na picha za marais wa Kenya yaani marehemu Mzee Jomo Kenyatta, Daniel Arap Moi na Mwai Kibaki, bali zitakuwa na nembo ya maliasili na tamaduni zinazoitambulisha Kenya kulingana na katiba.

1-18.jpg

Sarafu ya Sh1 itakuwa na picha ya twiga, Sh5 nembo ya kifaru. Katiba pia inaeleza kwamba sarafu ya Sh10 inapaswa kuwa na picha ya simba na Sh20 ya ndovu, yote yakiwa maliasili ambayo Kenya inavunia kuwa nayo na kuvutia watalii.

Sarafu ya Sh1 itakuwa na uzito wa gramu 5.5 na rangi ya silver, Sh5 itakuwa na gramu 3.75 na kipenyo cha 19.5mm, Sh10 itakuwa na gramu 5, kipenyo cha 23mm na rangi ya njano nje, wakati ndani ikiwa na rangi ya silver. Sh20 itakuwa na gramu 9, kipenyo cha 26mm. Silver nje na njano ndani.

“Huu ni mwanzo wa Kenya kuzaliwa tena na ufanisi wake. Haya yote yanaonesha juhudi tunazojivunia kupitia katiba yetu na malengo ya Ruwaza ya 2030,” amesema Rais wa Kenya.

Kiongozi wa nchi ameeleza kufurahishwa kwake na juhudi za Benki Kuu ya Kenya kuzingatia maoni ya wananchi katika kuzipa sarafu taswira ya raslimali “tunazojivunia kama taifa”.

2-18.jpg

Uchanya

Amesema sarafu hizi mpya mbali na kuzingatia maliasili, zitaweza kutambuliwa na walemavu wakiwemo vipofu.

“CBK imekuwa katika mstari wa mbele kuhakikisha taifa linaafikia Ruwaza ya 2030 pamoja na kulitambulisha duniani,” ameeleza.

Rais aidha, ametumia jukwaa la uzinduzi wa sarafu hizi kuhimiza benki kutumia mifumo mipya ya ubunifu katika kufadhili na kupiga jeki biashara ndogo ndogo na zile za wastani (SMEs). Sekta ya SME, maarufu kama Juakali, imebuni nafasi za kazi kwa zaidi ya asilimia 75 ya Wakenya.

“SMEs mbali na kuchangia serikali ushuru, kupiga jeki benki, imebuni nafasi nyingi za kazi na kutuletea mapato mazuri,” amesema.

Hafla hiyo pia imehudhuriwa na waziri wa Fedha Henry Rotich na Gavana wa CBK Profesa Patrick Njoroge. Rais Kenyatta amepokea hundi ya Sh800 milioni kutoka kwa CBK kwa niaba ya serikali.
 
ACHENI MAJUNGU, TUPAMBANE NA VIWANDA VYETU, KENYA NI LEVEL ENGINE, JAPOKUWA UKWELI UNAUMA
Hamna majungu hapo. Ni taifa lipi lisilojitambua linaweka sanamu za wanyama kwenye sarafu zake badala ya waasisi wa taifa waliojitolea kuwafikisha hapo walipo? Kwanza wakenya nawaona ni zaidi ya wanafiki, ni wendawazimu kabisa. Haiingii pichani wanamweka faru na ndovu kwenye sarafu wakati wameshindwa kuwalinda kila siku wanauliwa na majangiri.
Kenya hawana hata faru kumi kwenye misitu yao, leo watuaminishe wanamthamini faru? Ni kichaa tu atakaefurahia hili.
 
Hahahhaa mkuu nimecheka, ivi kwa hio hakuna hela yetu ata 1 isiyokua NA mnyama?? Tena afadhali zao zinawanyama but zetu zina mpaka wadudu( Nyoka), alaf labda nikuambie tu usibabaishwe na kuwekwa wanyama kwenye hela zao, wao wanajua zaidi ya tunavyojua mm na ww mkuu, ukija kwa upande wa hela yao, hela yao iko juu kuliko yetu ambayo, KWANZA 1.5 YETU IKO WAPI MKUU????
 
Hamna majungu hapo. Ni taifa lipi lisilojitambua linaweka sanamu za wanyama kwenye sarafu zake badala ya waasisi wa taifa waliojitolea kuwafikisha hapo walipo? Kwanza wakenya nawaona ni zaidi ya wanafiki, ni wendawazimu kabisa. Haiingii pichani wanamweka faru na ndovu kwenye sarafu wakati wameshindwa kuwalinda kila siku wanauliwa na majangiri.
Kenya hawana hata faru kumi kwenye misitu yao, leo watuaminishe wanamthamini faru? Ni kichaa tu atakaefurahia hili.
Pamoja na yote mkuu Kenya wanatuzidi mbali mno kiuchumi,kubali yaishe
 
Hamna majungu hapo. Ni taifa lipi lisilojitambua linaweka sanamu za wanyama kwenye sarafu zake badala ya waasisi wa taifa waliojitolea kuwafikisha hapo walipo? Kwanza wakenya nawaona ni zaidi ya wanafiki, ni wendawazimu kabisa. Haiingii pichani wanamweka faru na ndovu kwenye sarafu wakati wameshindwa kuwalinda kila siku wanauliwa na majangiri.
Kenya hawana hata faru kumi kwenye misitu yao, leo watuaminishe wanamthamini faru? Ni kichaa tu atakaefurahia hili.
Ni ufinyu tu wa mawazo. Hata nyie mnaoweka sanamu za wafu ndio kusema watu wenyewe hawauliwi na watu wenzao.

Hao wanyama kama wanauliwa, umesikia eti ni serikali ndio inawaua. Hakuna nchi iliyofika ilipo kwa juhudi ya mtu mmoja. Mambo ya kufanya wengine miungu watu ndio imeifanya bara hili kuwa hapa lilipo na kubaki kuangaika na bakuli kila siku. Bure kabisa.
 
Back
Top Bottom