Uhuru Hospital Mwanza, mmiliki ni kijana chini ya miaka 40. Tupe ujanja ulifikaje huko?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Kwa mara ya kwanza nilimsikia kwenye semina za fursa za clouds. Anaitwa Dr. Derrick.

Kwa jinsi anavyoongea, ni kama kwamba ni kwa vile ana uwezo mkubwa wa kuona fursa na kuchukua hatua na kwa akili na maarifa aliyo nayo, ameweza kufika hapo.

Pia nilimsikia akisema zipo fursa za wadau walio tayari kutoa mitaji kufadhili miradi iliyobuniwa, lakini watu wenyewe, ndio hawapo wanaobuni miradi.

Napenda kujua mwekezaji huyu alianzaje hadi kufika hapo?

Najiuliza mimi mtoto wa mkulima nimalize kozi ya udaktari na kwa miaka isiyozidi sita naweza kuwa na mtaji wa kuanzisha Hospitali?
 
Kwa umri huo kama amepata kihalali hongera.

Sasa ule uzio ambao una nyumba mbele yake angezibomoa tu ili pale na nafasi
 
Uhuru hospital..... Hospitali bomba sana hii..... Sio kubwa ila huduma bora kabisa..... Hata ambulance yao nzuri....safi sana
 
Uwekezaji mwingine ni mitaji ya wakubwa watu wanasafisha pesa zao kupitia miradi kama hiyo, huyo ni chambo tu, asikudanganye mtu bila kushikwa mkono hawezi kupata pesa hizo kwa biashara halali, hata USA matajiri wanashikwa mkono na serikali au wakikuona unakitu unataka kugundua lazima wakusaidie ufanikiwe na wao wafaidike.
 
Haya maisha haya, yaache kama yalivyo.

Mwingine ana skills na knowledge na well informed juu ya jambo (fursa) fulani, mwingine ana capital ila hana hivyo alivyonavyo mwenziwe, kwa hiyo wakati mwingine wakiungana ( combination) hapo lazima mafanikio yaonekana na sie watu baki unabaki kushangaa.

Yaani kwa ufupi siri ya mafanikio ya mtu, anayeijua ni yeye mwenyewe na hakuna atakayekueleza ABCDs zote za mafanikio ya maisha yake. Sahau.

NI MTAZAMO WANGU TU WANA JF
 
Back
Top Bottom