Uhuni unaoendelea Uwanja Wa Taifa Jamal Malinzi Uko wapi?

Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
7,022
9,285
Mod Haya ni malalamiko ya wananchi usitoe huu uzi.

Nimefika hapa uwanja wa Taifa kushuhudia mechi kati ya Yanga na JKU,
Cha ajabu watu wamefika kwa wingi tiketi watu wamenunua kupitia Selcom lakini cha ajabu mitambo haifanyi kazi na watu wanaekekea kudhulumiwa pesa zao.
Kinachosikitisha na kuonyesha uhuni wa hali ya juu ni kwamba, mtu akilipia hii mechi kupitia mtandao wa Simu mechi iliyooorodheshwa ni Yanga vs JKT Ruvu wakati mechi inayochezwa ni Yanga na JKU, hii ni ajabu sana kuwadanganya watu na hii inatia wasiwasi kuwa huu ni mpango wa makusudi wa kuwaibia Watu.
Mimi Binafsi nimelipia Kiingilio kwa kulipia VIP lakini cha ajabu hakuna lango lolote ambapo watu wa VIP wanapita leo.
Machine zote za kuingilia getini zimezimwa na hazifanyi kazi kabisa.
Ndugu Malinzi, Je ni kwa nini malalamiko ya wananchi juu ya Kuingia mpirani hamyatatui?. Je mnafanya hivi makusudi ili kuionyesha serikali kuwa Tiketi za kielectronic hazifai ili turudi mfumo uleule wa Zamani ambapo wajanna wachache walikuwa wanapiga hela?
Ninaona kwa Wazi kabisa kuwa watu wanajaribu Kumhujumu Waziri Mkuu kwa kuweka vigingi vingi ili zoezi la tiketi za kielectronic zifeli.
Kwa haya yaliyotokea katila mechi hii ya Yanga na JKU ni ubabaishaji, dhulma na uonevu wa hali ya juu kwa wananchi ambao wamenunua tiketi zao kielectronic halafu washindwe kuingia ndani.
Naiomba serikali kupitia wizara ya michezo ichunguze jambo hili, na iwawajibishe wahuni wote waliosababisha sintofahamu katika mechi hii
 
wewe sema tatizo hapo ni umeibiwa JKU nani angekuja / mbona hutumii akili ? na kuhujumiwa kwa MP kunatokea wapi ? acha unafiki na uzandiki kaa kimya
 
Mechi hii TFF aiwahusu na uwanja ni mall ya wizara tuangalie lawama zingine tupunguze tusiwe watu wa kukariri kila kitu TFF
 
Yanga kapigwa 2.Hamna cha mkata umeme wala mkata maji.Mpira mbovu kazi sifa za magazeti.
 
Back
Top Bottom