Uhuni huu unaofanywa na madereva na makondakta wa daladala si wa kuvumilia

Kuna tabia ya madereva wa daladala inapofika muda wa jioni ambapo kunakuwa na abiria wengi kwenye vituo vya daladala hukataa kupakia na kuondoka bila abiria kwa visingizio vingi ikiwemo kupeleka gari gereji n.k,lakini hii ni mbinu tu ya kutoza nauli mbili kwa safari moja.

Juzi nimeshuhudia kadhia hii pale Temeke Sterio ambapo daladala yenye usajili na T956 DTD inayofanya safari zake kati ya Temeke na Kisemvule kufika eneo la pale kituo cha kona ya kuelekea sterio(kwa wale wanaopafahamu) baada ya kushusha abiria na wengine kutaka kupanda dereva na kondakta wake kudai kuwa gari inapelekwa gereji.

Kilichofuata wakaelekea mpaka pale sterio sokoni mwisho ambapo pia kulikuwa na abiria wengi wa Kisemvule wakagoma kuwafungulia abiria mlango wakaondoa gari mpaka Temeke mwisho umbali wa mita kama mia moja hivi wakageuza gari wakaanza kuitia abiria wa kwenda Kisemvule kwa nauli ya Tshs 900/= badala ya 600/= ya Serikali.

Hapa maana yake nini?Wanapakia tena abiria wanarudi tena palepale kituo cha mafuta ambacho kipo "pua na mdomo" wanachukua mia tatu yako halafu wanageuza wanaelekea Kisemvule.

Nimeamua kuandika Uzi huu maana naona tabia hii imeshaota "mizizi" sehemu nyingi.Najua kuna watu wataanza kusema "Acha kupanda daladala nunua gari yako" wengine watatoa majibu yasiyoendana na maada hii,ila nimeandika kuwasaidia "watanzania wenzangu maskini"
Kila mtu anakula kwa urefu wa kamba.
 
Ila abiria na nyie hamna umoja kabisa,mnatakiwa nyote mnapanda ukifika muda wa kulipa mnalipa nauli yenu halali,konda na dereva wake wakizingua mnawachukulia hatua,ama kama wao watalipa iyo mia 900 na wewe unajua nauli halali ni mia 600 unalipa iyoiyo halafu uone konda atachukua hatua gani
 
haya matatizo yanatia hasira sana, Kuna wengine wanasema solution anunue gari, kwani hii kadhia inampata peke yake? au tununue gari nchi nzima?
Ilishafika muda serekali walitakiwa hio huduma waiendeshe wao kwenye miji mikubwa.
 
Back
Top Bottom