shikulaushinye
JF-Expert Member
- Aug 29, 2014
- 828
- 456
Wanatnzania wenzangu inashangaza na kusikitisha kuona kila kitu kinachoyanyika ktk awamu hii ni kipya, kama vile nchi haikuwahi kuwa na dola wala utawala. Kwa muda mrefu kila taasisi za dola zinazoifanya serikali kufanya kazi zilipata kiharusi.
Kwa leo naomba nizungumzie uzoefu wangu kuhusu utendaji wa jeshi la POLISI.
Kuna ndugu yangu ambaye ni POLISI, kwa kipindi cha miaka 7 ya nyuma alikuwa kitika kituo cha wazo, alinipa uzoefu wa kazi yake mpaka nikashanga sana, alinipa mbinu mbalimbali wanazotumia kujipatia pesa, kwa kifupi walikuwa na mtandao wa kuchukua pesa kwa bidhaa zinazoingia nchini kutoka Zanzibar kupitia bandari bubu ya MBWENI, waliweka vijana wa kuwapa taarifa za mizigo yote ya magendo na kulikuwa na network na wafanya biashara wa Kipemba.
Mzigo hufika kwa usafiri wa majahazi na boti ndogo usiku wa manane kisha kupakuliwa na kupakiwa kwenye magari aina ya FUSO, magari hayo hupata ulinzi au ESCORT ya polisi wakati mwingine gari la POLISI mpaka nyumbani au store za wapemba kama mbagara, Temeke na nk. kwa kuwa utaratibu huu unafahamika hata gari likikamatwa huwa wanapeana taarifa na kuliachia mara moja. Biashara hii inafanyika sana katika maeneo yote ya fukwe hasa MBWENI, BAGAMOYO NA TANGA.
Ukitaka kufanya utafiti mdogo; magari yote ya mizigo yanayotoka njia ya Bagamoyo lazima POLISI wayakamate lkn muda si mrefu hamalizana na wahusika na kuachiwa kuendelea kushusha mzigo. Wakati fulani hata askari wa usalama barabarani pale mwenge akiliona FUSO kutokea uelekeo wa BAGAMOYO huacha kuongoza magari na kulikimbilia kwaani ni dili zuri.
Gari la POLISI la kikosi maalumu cha kupambana ujambazi aina ya Toyota Landa Cruiser Pick up yenye bomba mara nyingi huwa lina namba za bandia utalikuta linafuatilia magari haya kutoka bagamoyo hasa FUSO. hufuata gari na mwisho huweka mtego pale karibu na daraja la JKT Mlalakua, then hukamata gari husika lkn kwa kuwa ni mtandao na wahusika huwa wana budget ya kazi hiyo gari halichukui round huwa linaachiwa mara moja.
USHAURI:
Serikali isitegemee POLISI peke yake katika vita hii ya biashara haramu, kwaani ni hatari siku zitaiingizwa siraha na milipuko na kutumaliza watanzania, kwa kifupi mikapa yetu ya majini haina ulinzi wa kutosha. Fukwe zote ziko wazi usiku na mchana. JWTZ wamejikita kulinda maji marefu.
Hakuna kitu kigeni ambacho jeshi la POLISI halijui, labda POLSI wote wa DAR wahamishwe au kiundwe kikosi maalumu ndani ya jeshi la POLISI maalumu kulinda mipaka ya bahari na ikitokea kukamatwa kwa bidhaa za magendo au siraha au madawa ya kulevya basi wawajibike.
Aksanteni.