Uhitaji wa katiba Mpya

HigherGround

Senior Member
May 14, 2015
108
94
Habarini wakuu,

Nikiangalia namna ambavyo raisi Maghufuli anavyoteua teua viongozi kwenye nyazifa mbali mbali, inadhihirisha namna katiba yetu ilivyo na mapungufu. Yaani nyazifa nyingi na zote nyeti kwa katiba tulio nayo sasa zimewekwa chini ya maamuzi ya mtu mmoja, nadhani hii ni hatari kubwa sana.

Hata kama ni mzuri kiasi gani, mwanadamu siku zote ana mapungufu yake, akipewa wigo mpana mwishowe huelemewa na sifa na kusahau utaratibu na kuanza kutumia mtazamo wake.

hili wadau ninyi mnalionaje?
 
Habarini wakuu,
Nikiangalia namna ambavyo raisi Maghufuli anavyoteua teua viongozi kwenye nyazifa mbali mbali, inadhihirisha namna katiba yetu ilivyo na mapungufu. Yaani nyazifa nyingi na zote nyeti kwa katiba tulio nayo sasa zimewekwa chini ya maamuzi ya mtu mmoja, nadhani hii ni hatari kubwa sana. Hata kama ni mzuri kiasi gani, mwanadamu siku zote ana mapungufu yake, akipewa wigo mpana mwishowe huelemewa na sifa na kusahau utaratibu na kuanza kutumia mtazamo wake.
hili wadau ninyi mnalionaje?

Una mifano? nani kateuliwa unamuona hafai? Unaposema hivyo ukumbuke pia kwamba Magufuli alichaguliwa kwa kura ya Wananchi kuwa Kiongozi wao. Hivyo vyombo unavyotaka wewe vifanye uteuzi vina msingi gani, vimechaguliwa na nani, vinathibitiwa na nani? Usisagau pia kuwa watu tuko milioni 50, wengi sana, lazima tutumie uwakilishi. Wawakilishi wetu ni Wabunge tuliwachagua sisi. Bunge likiamua limeamua, na hadi leo Bunge halina matatizo na teuzi za rais. Wewe ni nani? Unamuwakilisha nani?
 
Back
Top Bottom