Uhitaji wa ajira na tenda isiwe chanzo cha utapeli na kuingizana gharama zisizokuwa na msingi

Mnyuke Jr

JF-Expert Member
Jul 3, 2021
4,471
6,370
Wasalaaaam wakuu,

Nina imani ninyi wote ni wazima wa afya, bila kupoteza muda niende kwenye mada tajwa hapo kama inavyojieleza, katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wengi wakiume na kike katika nchi yetu la kutafuta ajira na tenda mbalimbali na hili linasababishwa na ukosefu wa ajira ambalo limekuwa janga kubwa sana.

Hivyo hii imepelekea hii imepelekea kupitia jukwaa hili la ajira na tenda, vijana wengi na mimi pia nikiwemo kuja kuanzisha uzi kwa ajili ya kupata msaada wa kupata kazi, ajira au Tenda yeyote ile cha msingi ile ni halali tu katika nchi yetu, na kupitia hili ninyi ndugu zangu mmekuwa shahidi katika hili, nyuzi za kuomba kazi Zimekuwa nyingi sana.

Katika jambo la kushangaza hii imekuwa tofauti kwa watu wengine humu jukwaani wamekuwa wakitumia nafasi ya watu kuhitaji ajira na tenda kwa lengo la kuwatapeli na wengine kukupa ahadi ya kukusaidia na mnapeana mawasiliano kabisa, na pia anaweza hata kukutumia nauli uende sehemu alipo ili akakupe tenda katika biashara zake au ajira katika kampuni n.k.

Cha kushangaza unafika katika katika mji ule na unampigia simu kumtaarifu kuwa umefika aje kukupokea, ila hapokei simu zako na kufikia hatua za ku Block laini yako kabisa katika hili mm nimekuwa muhanga na sio mara moja ni zaidi kabisa, pia katika kutapeliwa wengine wanafikia hatua ya kukushawishi uweze kutoa kiasi cha pesa ili aweze kukusaidia ila baada ya kumpatia hicho kiasi ana kublock kabisa, Jamani nimekuja hapa kuwaomba maBoss wa humu jukwaani, tafadharini sana msitumie nafasi zenu kutuumiza vijana wenu katika hili, imefikia hatua wengine tumeanza kuogopa kutafuta connection kupitia jukwaa hili.

Ila bila kukata tamaa tutaendelea kutafuta connection hapa jamiiforum naamini mafanikio ya vijana humu jukwaani yapo kupitia wakuu waliopo humu. Mwisho kabisa kwa mwenye ajira, tenda, kibarua chochote kile ambacho ni halali, kijana wenu ninahitaji msaada wenu katika hili mimi nipo Dar es Salaam-Mbagala zakhiem, mawasiliano yangu ni 0766626491 na 0629026431

Naomba kuwasilisha
 
Mkuu unataka msaada ila wewe hutaki kusaidia?

Be matured. Saidia ili usaidiwe. No free lunch in Africa. When you eat someone's bread you have to pay for it.
 
Mkuu unataka msaada ila wewe hutaki kusaidia?

Be matured. Saidia ili usaidiwe. No free lunch in Africa. When you eat someone's bread you have to pay for it.
Shida sio kusaidia mkuu, wengine sisi ni wepesi wa kutoa chochote ili tuweze kupata tunacho kihitaji, ila tatizo linakuja pale ambapo uliye mpa chochote anakata kila aina ya mawasiliano na ushiriano na wewe.
 
Back
Top Bottom