UHAURI: Wezi wa fedha za Serikali wafilisiwe ili mali zao ziwe za Serikali

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
1,183
1,817
Wateule wa Rais wamekuwa vinara wa kuiba fedha za serikali.

Wakati umefika sasa wa serikali kukamata mali zao bila kujali zilipatikana kwa fedha gani zitaifishwe na kuwa mali za serikali ili kufidia fedha zilizoibiwa.

Ni aibu kwa mteule wa Rais kuwa mwizi kwani kunamshushia hadhi aliyemteua.
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
49,910
86,082
Huyo rais mwenyewe ni muadilifu mpaka useme ni aibu kwa mteule wake kuwa mwizi? Hao wateule wa rais ndio husimamia michakato ya wizi wa kura na kunajisi uchaguzi ili rais apatikane. Sasa katika mazingira hayo ya mifumo michafu unamuwajibisha nani?
 
Nunio

Senior Member
Sep 17, 2013
194
477
Mwamba alikuwa anapita nazo kimya kimya, ukiona umeonewa, lete vithibitisho halali vya upatikanani halali wa ukwasi wako.....unakimbilia kuomba huruma ya jamii ya walafi wenzako mitandaoni, ye hana habari....anaenda kumpa mama mwenye dhiki anayedaiwa matibabu na tayari keshapoteza mtu pale Muhimbili, mara kaagiza ndege kwa cash....sio vichwa na mabehewa used kwanza kisha ndo mapya(ulambaji asali huu)

Ni ujinga kuthibitisha kuwa mtumishi amekwapua billions of shillings, kisha kumuacha POLISI, TAKUKURU na MAHAKAMA watende kazi ya kumfunga tu huyu ilihali wao wote wananunulika, si wanalipwa milioni milioni kama mishahara, hili JIZI likitoa hata 10m kwa kila kigingi, likabakiwa na 5bn ana hasara gani?

FILISI, PIGA SHABA
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
56,184
131,525
Nyie endeleeni kupigwa tu mpaka mtakapo amua kufuata nyayo za Sri Lanka, Wateule walafi ni reflection ya Raisi mlafi!

Aliekuwa anazirudisha hizo mali kwa mlango wa nyuma mlimwita dikteta mshamba anayechukia matajiri. Huyo tajiri kakwepa kodi si chini ya miaka 2O kufika hapo aliko.
 
Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,457
9,899
Huyo rais mwenyewe ni muadilifu mpaka useme ni aibu kwa mteule wake kuwa mwizi? Hao wateule wa rais ndio husimamia michakato ya wizi wa kura na kunajisi uchaguzi ili rais apatikane. Sasa katika mazingira hayo ya mifumo michafu unamuwajibisha nani?
Hajui kuwa wanajua vizuri humo ndani na pengine raisi nae anapata mgao wake?
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
38,833
92,452
🐒🐒🐒
16504564148361.jpg
 
maiyanga1

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
1,177
1,538
Ukisikia mtumishi wa serikali anafungwa kwa wizi wa fedha ya serikali jua kuna mawili:
1. Aliwapiga wakubwa katika mgao au
2. Amenyandua mzigo wa boss
Tazama matumizi ya mawaziri, manaibu, makatibu wakuu, wakurugenzi jinsi wanavyotumia tofauti na vipato vyao.
Tume ya maadili imeshawahi kuchukua hatua gani kwa viongozi waliojipatia mali kinyume na utaratibu?
 
Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
65,242
69,305
Wateule wa Rais wamekuwa vinara wa kuiba fedha za serikali.

Wakati umefika sasa wa serikali kukamata mali zao bila kujali zilipatikana kwa fedha gani zitaifishwe na kuwa mali za serikali ili kufidia fedha zilizoibiwa.

Ni aibu kwa mteule wa rais kuwa mwizi kwani kunamshushia hadhi aliyemteua.
Waanze naye yeye mwenyewe
 
Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
65,242
69,305
Ukisikia mtumishi wa serikali anafungwa kwa wizi wa fedha ya serikali jua kuna mawili:
1. Aliwapiga wakubwa katika mgao au
2. Amenyandua mzigo wa boss
Tazama matumizi ya mawaziri, manaibu, makatibu wakuu, wakurugenzi jinsi wanavyotumia tofauti na vipato vyao.
Tume ya maadili imeshawahi kuchukua hatua gani kwa viongozi waliojipatia mali kinyume na utaratibu?
Kweli tupu
 
Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
65,242
69,305
Utafilisi nchi nzima?
Hakuna muadulifu tusijidanganye Ndio maana utasikia tu Takukuru mpo?
Mchukueni huyo mkurugenzi na anapewa lift tu anasepa

Hautakuja kusikia huyo kafungwa miaka 30 kwa wizi wa Billion kadhaa ila utasikia kafungwa miaka 30 kwa wizi wa Ng’ombe
Jamaa kabla ya kuiba wanakaa na wanasheria wazuri
 
Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
65,242
69,305
Nyie endeleeni kupigwa tu mpaka mtakapo amua kufuata nyayo za Sri Lanka, Wateule walafi ni reflection ya Raisi mlafi!

Aliekuwa anazirudisha hizo mali kwa mlango wa nyuma mlimwita dikteta mshamba anayechukia matajiri. Huyo tajiri kakwepa kodi si chini ya miaka 2O kufika hapo aliko.
Shida ya nchi yetu wizi unaanzia juu kushuka chini
 
5 Reactions
Reply
Top Bottom