Uhasama kati ya Waisrael na Wapalestina: Ninahitaji kujua the history behind

Jack Beur

JF-Expert Member
Feb 26, 2010
222
246
Huu uhasama wa Waisrael na Wapalestina unaelezwa kwamba mnamo mwaka 1948 waisrael walivamia ardhi ya wapalestina na kuikalia kwa mabavu, inaelezwa pia waisrael walikuwa utumwani huko ulaya mashariki, Poland, Germany, na kwingneko, inaelezwa kwamba huko

Ujerumani mtawala wa kipindi hicho Adolf Hitler aliwatesa sana kwenye gas chamber na concentrated camps, inaelezwa hili kovu halitakaa lisahaulike katika vizazi vya waisrael.

Ninachotaka kufahamu, hao waisrael walifka huko ulaya mashariki wakitokea wapi, ( ancestor land), walipelekwa huko kama watumwa au kwa minajili gani, maake kusema waisrael walikuja baadae kuwanyang'anya ardhi wapalestina bila kujua walikuwa wakiishi wapi kabla inakuwa ni ngumu kujua mtiririko wa tukio zima.

Naomba wajuzi wa historia wanisaidie kulielewa hili, pia naomba hao wataalamu wa hii history wajikite zaidi kwenye actual story, story ya kwenye Biblia ninaifahamu tangu nikiwa mdogo.

Ahsanteni sana.
 
Hakuna story ya ziada zaidi ya uliyosoma kwenye bibilia yako. Mengine ni yale ya Trump kuutambua ule mji mkuu.
 
Huu uhasama wa Waisrael na Wapalestina unaelezwa kwamba mnamo mwaka 1948 waisrael walivamia ardhi ya wapalestina na kuikalia kwa mabavu, inaelezwa pia waisrael walikuwa utumwani huko ulaya mashariki, Poland, Germany, na kwingneko, inaelezwa kwamba huko

Ujerumani mtawala wa kipindi hicho Adolf Hitler aliwatesa sana kwenye gas chamber na concentrated camps, inaelezwa hili kovu halitakaa lisahaulike katika vizazi vya waisrael.

Ninachotaka kufahamu, hao waisrael walifka huko ulaya mashariki wakitokea wapi, ( ancestor land), walipelekwa huko kama watumwa au kwa minajili gani, maake kusema waisrael walikuja baadae kuwanyang'anya ardhi wapalestina bila kujua walikuwa wakiishi wapi kabla inakuwa ni ngumu kujua mtiririko wa tukio zima.

Naomba wajuzi wa historia wanisaidie kulielewa hili, pia naomba hao wataalamu wa hii history wajikite zaidi kwenye actual story, story ya kwenye Biblia ninaifahamu tangu nikiwa mdogo.

Ahsanteni sana.
Ninachofahamu ni kwamba,baada ya mwenye enzi MUNGU kuumba ulimwengu ikalazimika lazima ulimwengu upate mwogozo,na mwongozo wa sheria za walianza kuupata waislaeli.

Nachotaka kusema ni kwamba,hapo zamani utawala ulikuwa unadhibitiwa na manabii na mitume,na hao waislaeli walitawanywa kwa vita vilivyotokea miaka hiyo kama kwao ni adhabu kwao..na kwenye vitabu vya kihistoria unaweza kuona kukaa kwao pamoja kulizuia dini isikuwe kwa kuwa hawakuitaka dini hata kidogo,kwani walimuuwa nabii zakalia,walimuudhi Nabii Musa na hata kumvunjia heshima MUNGU kwa kudai hawataendelea kumuabudu mpaka wamuone na walivyoenda ukawatokea mlipuko huko kisha wakajuta,pia walimuuwa nabii issa na mbaya zaidi kubadilisha maneno kwenye vitabu vyao vya dini..

Kwaiyo ili kuwaadhibu wakaadhibiwa kwa vita vilivyotokea kipindi hicho na kufutwa kabisa hilo kabila la kiyahudi ili lisiwepo na wakatawanywa yaani walifutwa wasiwepo kwenye hiyo ardhi na hiyo ilikuwa azma yake MUNGU ili kufanya eneo liwe salama. na wengine wakawa wako misri na maeneo mengine.

Huko misri wakatumiwa na firauni kama watumwa na ardhi ikabaki mikononi mwa Palestine kwa kuwa Israel ni kabila tu la watu wachache.

Wakajuta na kutubia makosa yao na kutamani kurudi kwenye ardhi yao ya zamani na hapo wakala kiapo kuwa yale mambo yao hawatarudia tena na ndipo akatumwa MUSA aende kuwafuata ili wahifadhiwe tu hapo na walikubaliana kuwa watakifika watakuwa watiifu na watakuwa pia ni wenye kufuata amri zake bila kubagua..

Cha ajabu sasa,hilo kabila likakua na wakarudia yaleyale ambayo waliokatazwa na sambamba na hilo kuna mataifa na watawala wanasaidia wale watu warudi kama taifa"kwa sababu lile ni kabila tu la wayahudi kizazi cha islaeli ambae ni mtawala mchungaji wa zamani.

Na sasa kabila limefanywa kuwa nchi na haitoshi wanawafukuza wale ambao wamewakuta ambao walibaki kama watu wema baada ya wao kufutwa kama kabila dhalimu.

Kimsingi haya ni matatizo ya kidini zaidi.

Na sio ya kisiasa.
Na kwenye vitabu vya dini hao waislaeli walikuwa wanapendwa mno mpaka wakawa wanadhani hawawezi kukasirikiwa na MUNGU na.

Na mwishowe MUNGU amewalaani zaidi kwa kumdhalilisha yesu ambae alitumwa aje awafundishe ustaarabu na dini na pia kubadilibadili maneno kwenye taurati na injili.

Taifa la MUNGU au la kiungwana haliwezi kuwa na vitendo vya kuuwa mitume na baadhi ya wachamungu.

Ili kufichua haya MUNGU akabadili mpango wake na akachagua katika waarabu ambao hawakuwa na Muonyaji au nabii kwa kipindi chote hicho na kumpa Qurani na hapo ndipo chuki zilipozidi...

Kwa kuwa wao kitu mitume au nabii hawakutaka kabisa.

Cha ajabu sasa:
Wao wanasema,jibril au wao humwita malaika Gabriel'alifanya hiyana kupeleka Quran Makkah na alitakiwa aipeleke kwao,yaani malaika Gabriel anachuki na hao waislaeli kitu ambacho MUNGU anasema yeye ni malaika mwaminifu mno na ni mtiifu na kama wao wanafanya ushindani na hilo wasubili waone..

KABILA LIMEZAA KUWA NCHI.
WANAITWA WAHARIBIFU.

MUNGU anajua zaidi.
 
Mgogoro wa Palestina na Israel chanzo chake ni Waraka wa Balfour au Balfour Declaration. Kiufupi Uengereza waliwaahidi Wayahudi kuwapa nchi katika ardhi ya Palestina. Sasa kilichofanyika Wayahudi hawa walitumia mabavu na kufanya mauaji ya kutisha ya Wapalestina zaidi ya elfu 10 na kupelekea wengine zaidi ya laki 7 kuyakimbia makaazi yao na kuwafanya kuwa wakimbizi.

Sasa Wapelestina kitu hichi wanakiita Nakba au catastrophe . Na ndio chanzo cha wao kuupinga utawala dhalimu wa Israel. Hata haya maandamano ya sasa yanapinga jambo hili. Kuna baadhi ya wapelestina mpaka leo wanazo funguo za nyumba zao.

Lakini uovu wa Israel haukuishia hapo. UN waliigawa Palestina na ndo ikapatikana Israel. Lakini ile Ardhi iliyoamriwa ibakie kuwa ni Palestina bado Israel wanaendelea kuipora na kuikalia kimabavu. Wapalestina wakipinga ndo wanaonekana kuwa ni wakorofi. Lakini mateso na ubaguzi wanaoupata Wapalestina katika ardhi yao ni mkubwa na wa kutisha kwa kiasi ambacho mauti kwao wanaona ni bora kuliko kuwa hai.

Mfano katika ukanda wa gaza hakuna maji safi na salama, watoto wanakosa lishe, umeme ni masaa manne kwa siku pia idadi kubwa hawana ajira.

Wakati Israel anapokea mabilioni ya misaada ya fedha na kijeshi kutoka Marekani, hakuna msaada wowote wanaoruhusiwa kupokea Wapalestina bila idhini ya Israel.

Mpalestina anaweza kufungwa kwa kumpiga kibao mwanajeshi wa Israel lakini Myahudi anaweza kuua familia nzima ya Wapalestina na akawa huru.

Sheria za Israel haziangalii umri wala jinsia. Watoto wengi wa kipalestina wako magerezani Israel kwa makosa ya kurusha mawe tu.

Waisrael hawachagui pa kushambulia wala aina ya silaha. Wanashambulia shule hospitali sehemu za ibada makaazi ya raia n.k
 
Back
Top Bottom