Mkuu tatizo lililopo taaluma ya afya imeingiliwa zaidi na watu au makampuni yanayolenga maslahi binafsi kuliko ustawi au maendeleo ya taaluma yenyewe. You can't imagine makampuni ya madawa yanakimbizana kutengeneza chanjo yapate hati miliki ili yafanye biashara kutengeneza super profit bila kujali maadili na sheria zinazoongoza maswala ya kitafiti. Nafikiri kila mmoja aliona makampuni kutoka nchi tajiri duniani kama marekani, ujeruman, urusi, china, uingereza walivyokuwa yanahaha kuwahi kuja na suluhisho la chanjo, kwa hiyo hapo tayari utanusa ubeberu wa siasa za kimataifa. Huu ubinafsi umefikia hatua tafiti zinafanyika kwa siri bila takwimu za kitafiti kuwekwa wazi kwenye makongamano ya kimataifa na hata kwenye majarida ya kimataifa kama njia ya kuchangia maarifa na watafiti wengine duniani. Ukifuatilia ni kwa kiasi gani data za kitafiti kuhusu teknolojia ya mRNA ya kuzalisha chanjo zimekuwa shared kwa watafiti wengine duniani ili watoe maoni yao au na wenyewe waweze kufanya verification ni kituko, au teknolojia ya nano-particles/nano-molecules kufanya targeted delivery ya chanjo na madawa ndani ya mwili wa binadamu bado utakuta data kama hizo zinafichwa na makampuni kwa kisingizio cha hati miliki....