Uhamiaji YAZINDUKA: Jandu Singh na wenzake 18 kupanda kizimbani!

Wakimaliza hapo waende Lugoba, kwenye "ma-crusher", kule kumejaa wahindi (estim, highland estate, hari singh), wachina(China Geo), badr east africa(wasomali), east african stone crusher(wasomali) na site nyengine nyingi kule wamejazana hawa wageni na wanaishi huko huko "sites". Ukirudi dsm kwenye magodowns na viwanda kama NIDA(Wapakistan), MMI Steel(wahindi), OILCOM, PARADISE HOTEL, Estim construction na makampuni mengine mengi.

Kwa kweli inafika wakati, wengine tunatamani tungeajiriwa immigration, kwakuwa hawa wenzetu waliokabidhiwa dhama hii hawaitendei haki kabisa nchi yetu. Huko migodini ndipo hakushikiki, inauma kwa kweli, inabidi watu wa immigration wawe wazalendo wa kweli.

Mnabadilika sana mkishapewa dhamana..tofauti na wakati mkiwa nje ya madaraka...(experience)

Swala ni kuwepo kwa control mechanism tena ya kudumu (watch dog)

Watu wakipata madaraka wanakuwa tofauti sana ikiwemo wewe
 
Mwanakijiji umefanya la maana ku highlight hii issue ya Jandu.....huyu bwana ndiye aliyejenga lile jengo refu lenye utata pale opposite na ocean road hospital,pale karibu na holiday out wanapokula vyakula wafanyakazi mbalimbali na wanafunzi wa ifm.Kwa wale wenye taarifa na jengo hili (ambalo linataka kufanywa hotel/ au residential) watkumbuka kuwa jengo hili limejengwa kwa makosa kutokana na sheria za nchi......hapatakiwi kujengwa eneo lile karibu na ikulu jengo lenye ghorofa zaidi ya nane lakini jengo hili limejengwa na ghorofa zaidi ya nane na linatazamana na ikulu (yaani liko juu zaidi ya ikulu)jambo ambalo litahatarisha security pale white house.Kwa wasio na taarifa ni kwamba tayari baada ya kelele nyingi serikali wamesema wenye jengo hili wasikodishe zaidi ya ghorofa ya nane.....zile za juu zitakodishwa na serikali......

My take:
  • Huyu mjamaa ni kweli ana uhusiano au network kubwa na vigogo wa serikali
  • Huyu mjamaa ni kati ya wahindi wenye hela noma ambao wamekuja tz kutuibia
  • Huyu mjamaa ana hela chafu si kidogo kwani kampuni yake ni kati ya kampuni kubwa sana hapa tz
  • Tukumbuke watanzania tunavunwa kwa kiasi kikubwa kupitia kwenye sekta ya ujenzi na hawa majamaa kama jandu ndio wenye kutafuna hizi tender za ujenzi..........
  • Hawa majamaa huwa wanakuja tz na mikono mitupu alafu kwa udhaifu wa mifumo yetu ya fedha wanapewa mikopo ya kufa mtu wanapata mitaji mikubwa alafu wanashinda tender za ujenzi wakati wazawa mikopo mikubwa hawapewi na matokeo yake hawashindi tender kubwa za ujenzi/biashara na matokeo tunawaona wageni kama wahindi,waarabu na wachina wakishikilia kila sekta ya ujenzi wa nchi yetu huku wazawa tukilia.Mkitaka kulijua hili nendeni TIB, CRDB, stanbic, standard chatered bank mkaulize nani wateja wakubwa wa mikopo yao.......mtakuta ni hawa kina jandu, manji, paatel, murji,chang, singh etc etc........wazawa hamna.......hata nimeona yule mwarabu wa dowans ....ali adawi ni kati ya wateja wa TIB!!!!!!!!!!yaani mgeni anakuja tz anapewa mkopo wa kuzalisha umeme wakati kuna wazawa kibao!!!!!!!!tena wasomi!!!!!!!leo hii nani mtanzania ataweza kwenda india, au china ua uarabuni akapewa tender kubwa ya ujenzi au biashara tena kwa mkopo wa nchi!!!!!!!!!!!waulizzeni hata watanzania walioko marekani akina willy kama wanaweza kupata mikopo benki za kule na kupata deal kubwa kubwa za kibiashara.....hamna.....kooote ulaya,asia...hamna hii kitu ni kwetu tu tz....kwa waliwao......hii tz inachukiza yaani....hata hawa akina rostam.............fatilieni wao na ndugu zao walikujaje tz???????walikuwa hawana kitu....vyote wamechumia tz........................tena kwa kipindi cha baada ya Nyerere kuondoka....................wahindi waliokuwepo enzi za Nyerere walikuwa waadilifu kwasababu ya system iliyokuwepo............lakin i baadae.....hali ni kama tuliyo nayo
Angalizo: Adui mkubwa number moja wa mtanzania ni mtanzania mwenyewe........tutalia saana lakini tuanze na sisi wenyewe........nani anayewapa deal hawa majamaa???ni mtanzania.......nani anawapa hela....mikopo??ni mtanzania mwenyewe.......nani anachukua 10% zao????ni mtanzania mwenyewe........sasa tunalia nini???????????????????????????
Mkuu sahihisha info yako, mjenzi pale ni ESTIM CONSTRUCTION (vile vile tuhuma hizo zinamhusu)
 
Hii ni matunda ya siasa ya ushindani iliyopo kwa sasa!, kidumu CDM, kidumu CCM. watafanya kazi tu!, hata kwenye madini watazinduka muda si mrefu!
 
Kwa upande mwingine tofauti na matatizo yaliyopo ndani ya Idara hii ya Uhamiaji hasa kwa maafisa wao na utendaji wao,Napenda kutoa pongezi kwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa Dar(RIO) simfahamu kwa jina ila alitokea Mkoa wa Kilimanjaro huyu jamaa yuko makini na kazi yake na tangu amefika mabadiriko yameonekana Huyu jamaa haendeshwi na Viongozi iwe wakisiasa ama Makamisha wa Makao makuu, hii ndio inapelekea ufanisi huu na mengi yaliyo pita kama yalivyo ripotiwa na gazeti la Nipashe:Komaa kamanda na wenzako wa Mikoa mingine kama Mwanza ,Tanga,Arusha na mipakani wapate somo la kuto pelekeshwa na Manyang'au wa Makao Makuu wanakalia kupiga simu na kuwa dhalilisha maafisa wenye vyeo vidogo pindi wanapo tekeleza Majukumu yao halali,Kwa hapa Dar umewaweza kamanda wakiskia ni kutoka Mkoani wanaufyata.Nimwanzo mzuri na ninatumai mtashinda na kuturudishia heshima ya Mkoa wetu na Taifa kwa ujumla.
 
[h=2]Watiwa hatiani kwa uhamiaji haramu[/h] Thursday, 03 November 2011 18:53 newsroom

MAFUNDI bomba 18 raia wa India na Pakistan, wamefikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya kuishi nchini bila kibali. Washitakiwa hao na mkandarasi wa Kampuni ya Jandu, Ndegrjit Jandu (61), walipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mustafa Siyani. Washitakiwa hao ni raia wa India, Surji Singh (36), Chandresh Jesarani (26), Pravin Bhudiya (26), Harmandeep Cheema (20), Dilio Singh (23), Manji Parbat (23), Barindel Sharma (25) na Suresh Kumar (26).
Kartikuma Patel (29), Dahyabhai Patel (30), Vindo Pindoriya (25), Mukesh Kerai (25), Prafulbahi Patel (35), Jatinder Singh (25), Kishor Patel (24), Rajesh Ramdhiai (26) na Hareshkuma Samji (44). Raia wa Pakistan ni
Shahzad Munawar (33).
Wakili Patrick Ngayomela kutoka Idara ya Uhamiaji, alidai shitaka la kwanza linamkabili mkandarasi huyo, raia wa Tanzania mwenye asili ya Kiasia, anayedaiwa Novemba 2, mwaka huu, katika kampuni hiyo iliyopo Buguruni, aliwaajiri raia wa kigeni wasio na vibali vya kufanya kazi nchini.
Mkandarasi huyo pamoja na washitakiwa wenzake, katika shitaka la pili wanadaiwa siku hiyo walikamatwa bila ya kuwa na kibali kinachowaruhusu kuishi nchini.
Ngayomela katika shitaka la tatu alidai washitakiwa walijihusisha na ajira bila ya kuwa na vibali.
Washitakiwa walikiri makosa, ambapo walisomewa maelezo ya awali, ambayo pia waliyakiri.
Hakimu Siyani aliwatia hatiani washitakiwa na kuwahukumu kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya sh. 50,000 kwa kila shitaka. Hata hivyo, alisema adhabu hizo zitatumikiwa kwa pamoja.
Hadi jana mchana walikuwa hawajakamilisha taratibu za kulipa faini hiyo.

UHURU
 
Watiwa hatiani kwa uhamiaji haramu

Thursday, 03 November 2011 18:53 newsroom

Yaani ka-faini ka TZS 50,000 kwa kila kosa!! KWani wana makosa mangapi!!! Hata kuwafukuza nchini hakuna!! Yarbi Toba!!
 
Mbwembwe tu hizo hakuna kitakachoendelea keshokutwa utasikia ushahidi umekosekana.

Hilo changa la macho.
 
By Ntambaswala Nilishasema kuna ajira zaidi ya 300,000 ambazo zimeshikwa na wageni, ajira hizo ni za kada ya kati- graduates wa VETA, diploma na hata shahada wengeweza kuzifanya. Nilivyosikia rais anatangaza ajira mpya 1,000,000 nilijua ataanza na hizi 300,000

Wako wengi hawa. kuna wachina, wahindi, nk

Sio siri hii ni biashara kubwa ya Watu wa uhamiaji wakishirikiana na idara ya kazi na kituo cha uwekezaji....waliio wengi kati ya hawa wanapatiwa vibali vya kufanyia kazi nnchini.....Jambo baya kabisa na la aibu wengi wao hawana qualifications...na hasa wahindi...na mbaya zaidi hawa ambao hawana qualification yoyote wanalipwa mishahara mikubwa kuliko wenye nnchi yao!!!!!!.... Watu wa uahamiaji wankula vichwa sio mchezo kwa hizi work permit...kwahiyo wao wenyewe uhamiaji wanwajua wahamiaji wote ambao hawastahili kufanya kazi nnchin...
 
Mkuu sahihisha info yako, mjenzi pale ni ESTIM CONSTRUCTION (vile vile tuhuma hizo zinamhusu)

Uko sahihi kidogo si mjenzi mkuu (Main-Contractor) hata jengo la Uhamiaji makao makuu si mjenzi mkuu ila ni mmoja wa wajenzi (sub-contarctor).
 
Mnabadilika sana mkishapewa dhamana..tofauti na wakati mkiwa nje ya madaraka...(experience)

Swala ni kuwepo kwa control mechanism tena ya kudumu (watch dog)

Watu wakipata madaraka wanakuwa tofauti sana ikiwemo wewe

Mbona unakurupuka Topical,

Kama experience yako ni watu kubadilika, bila shaka ni kutoka kwakmo mwenyewe ama wengine wa aina yako.

Kwani unafahamu mimi nafanya kazi gani na wapi?? kwamba unaweza kuthibitisha kwamba na mimi nitabadilika? haya ni mawazo ya kipuuzi tu ambayo hayawezi kutusaidia. Nchi hii kuna watu tuna nia na moyo wa kuisaidia na kwa nafasi zetu tunafanya hivyo. Sasa kama unaona watu fulani wanaboronga lazima uwe na hasira na kutamani upewe hayo majukumu kwa nia njema ya kulisaidia taifa, kama wewe umeishiwa uzalendo, usidhani kwamba wote tumekuwa kama wewe. Sitoshangaa kama hilo ndio somo ulilojifunza kwa MS, na kwahiyo kila kitu unakitazama kwa jicho hilo!
 
Mtakaporuhusu URAIA wa NCHI mbili mauzauza haya yataongezeka zaidi. Subirini.
 
wasiishie JANDU tu waje huku ESTIM Construction waone kituko maana wakiachiwa hivi hata walinzi watakuwa wahindi na wafilipino
 
Back
Top Bottom