Halafu sijui kama bado ipo,ila polisi pia kuna wakati walikuwa wanakamata watu hovo hovyo tu,eti mzururaji,na ukweli hizo kazi hazipo,basi tu unyanyasaji,halafu pia inajulikana kabisa kuingia polisi ni bure,lakini kutoka ni pesa,sasa sijui wanategemea mzururraji atoe wapi hiyo pesa?Wakuu Mkienda pale Blue Pearl Hotel ubungo
Ndio mtashangaa wapo wahindi zaidi ya 11 ambao wanafanya kazi wanalala hapohapo hotelini hawana vibali vya kuishi nchini
achilia mbali kufanya kazi. tumepeleka taarifa mara kibao uhamiaji hakuna hatua. Ukienda pale diamond motors hivyo hivyo.
Hawa wa blue pearl wako active usiku zaid kuliko mchana. Ukitaka info zaidi wasiliana na wafanya kazi wa pale. napendekeza kama
kweli uhamiaji wanataka kumaliza huu uozo wa wageni wasio na sifa za kufanya kazi nchini tupo tayari kushirikiana nao kuwapatia majina, simu number zao, wanaishi wapi wanafanya kazi saa ngapi ili wawakamate.
Mtanzania asilia.
Safi sana
Jandu Singh
Katika kile kinachoaminika kuwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Shamsi Vuai Nahonda la kuwataka maafisa uhamiaji kuonesha ndani ya wiki tatu wamefanya nini kudhibiti uhamiaji haramu mmiliki wa kampuni ya Jandu Construction & Plumbing, Indertit Sigh Jandu, amekamatwa na Uhamiaji kwa tuhuma za kuwahifadhi na kuwatumikisha wahamiaji haramu 18.
Jandu ambaye ameshiriki kujenga jengo la Uhamiaji Kurasini, alionyesha jeuri akidai kuwa na mahusiano na vigogo Uhamiaji, serikalini na wanasiasa lakini sasa yuko mahabusu. Walikamatiwa eneo la kampuni hiyo Buguruni Dar es Salaam Jumatatu usiku. Kumi na saba (17) ni raia wa India na mmoja wa Pakistan.
Jandu aliamua kutafuta njia ya kuzima sakata hilo kwa ‘wakubwa' kwa kwenda makao makuu ya Uhamiaji lakini akakwaa kisiki.
Wafanyabiashara wenye asili ya Kiasia wamekua wakifanya biashara ya watu kwa kuingiza wahamiaji wengi na kuwatumikisha katika kampuni zao, baadhi wakiwa katika maandalizi ya kwenda kufanya kazi Afrika Kusini
HABARI ZAIDI HAPA
Mkuu hakuna uvivu ni namna organisation behaviour inavyojengwa!! Tuadhibiwe kwa kutoku perform na si kwa kukosa nafasi sababu ya wageni! Hatuwezi kujiadhibu na kugeuza nchi shamba la bibi kisa eti sisi wavivu! Tuna matatizo yaliyochangiwa na historia na utamaduni wetu lakini haya hayatufanyi vilema!! Hii ni nchi yetu mgeni yeyote lazima afate sheria zetu.hatuwezi kuwafundisha watu wetu kwa njia hii pasco! Lakini pia kujituma kwa hawa wageni si bure,ukifuatilia walikotoka,namna walivyopenya nchini na masharti wanayopewa na hao wanaowaleta ingekuwa hata watz wangekuwa hivyo! Hawatuzidi ubinadamu wowote!! Tuna madhaifu yetu lakini pia tuna nchi yetu na sheria zetu Pasco!!Asante Mzee Mwanakijiji kwa hili.
Pamoja na hili naomba ifike wakati sisi Watanzania wenyewe tujitathmini utendaji wetu wa kazi.
Tangu enzi za ujenzi wa reli ya kati, leba force ilitoka India na ndio wakapata fedha wakajenga hayo maghorofa uhindini.
Ukienda hoteli nyingi za kitalii, leba force kubwa ni Wakenya kwa hoja kuwa Watanzania ni wavivu, na wanaongoza kwa absentisim kwa visingizio kibao.
Naunga mkono hoja zozote za empowerment kwa Watanzania ila pia naunga mkono let foreign labor force itake place for doing dirty jobs Watanzania hawawezi kuzifanya.
Maeneo ninakoishi mimi, asilimia 80% ya mashamba boy ni Wamalawi. Wakowapi hao mashamba boy wa Kitanzania?.
Angalieni makampuni ya ujenzi na gereji za Wachina. Kazi ni usiku na mchana, hakuna Jumapili wala sikukuu. Nyumba ya kuishi unakabidhiwa within one month. Ukipeleka gari almost write off, inakuwa restored within a week!. Jee Watanzania tunaweza au kazi kulalamika.
Juzi nimepita pale Doha, kuanzia wahudumu wa vyooni mpaka wahudumu hotelini wote ni Wahindi. Zamani dada zetu angalau walitamba japo kwa kale kabiashara, sasa wachina, wafilipino na warusi wamewapiku!. Watanzania tunaweza nini zaidi ya majungu na kulalamika kwa sana!.
Kwa wapitaji wa Bagamoyo Rd, yale Maghorofa marefu karibu yote ni ya wawekezaji wa Kisomali hebu tembeleeni vitegauchumi vyao, wafanyakazi wote mpaka wafagiaji ni Wasomali, Kiswahili hawajui, Kiingereza hawajui ila utahudumiwa kila utakacho kwa sign language!. Watanzania tuko wapi?.
Shoprite walipokuja walifingua masuper market lukuki, JM Mall, My Fair Plaza, Lumumba, etc, waliajiri wabongo, wamewaibia mpaka maduka yamefilisika sasa yamefungwa!. Mtu akileta Wahindi kwa sababu ni waaminifu ni makosa?,
Jandu Singh
Katika kile kinachoaminika kuwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Shamsi Vuai Nahonda la kuwataka maafisa uhamiaji kuonesha ndani ya wiki tatu wamefanya nini kudhibiti uhamiaji haramu mmiliki wa kampuni ya Jandu Construction & Plumbing, Indertit Sigh Jandu, amekamatwa na Uhamiaji kwa tuhuma za kuwahifadhi na kuwatumikisha wahamiaji haramu 18.
Jandu ambaye ameshiriki kujenga jengo la Uhamiaji Kurasini, alionyesha jeuri akidai kuwa na mahusiano na vigogo Uhamiaji, serikalini na wanasiasa lakini sasa yuko mahabusu. Walikamatiwa eneo la kampuni hiyo Buguruni Dar es Salaam Jumatatu usiku. Kumi na saba (17) ni raia wa India na mmoja wa Pakistan.
Jandu aliamua kutafuta njia ya kuzima sakata hilo kwa wakubwa kwa kwenda makao makuu ya Uhamiaji lakini akakwaa kisiki.
Wafanyabiashara wenye asili ya Kiasia wamekua wakifanya biashara ya watu kwa kuingiza wahamiaji wengi na kuwatumikisha katika kampuni zao, baadhi wakiwa katika maandalizi ya kwenda kufanya kazi Afrika Kusini
HABARI ZAIDI HAPA
...Pasco, unataka kusema kwamba kufungwa kwa Shoprite pale JM Mall, Lumumba, Mayfair Plaza na Slipway ilitokana na wizi wa waswahili? Mbona maduka ya wahindi mjini ndio yanayoibiwa sana kuliko hata hao. Kumbuka kuwa si kila eneo unalofungua biashara linakuwa na mzunguko wa wateja kutosha kukurudishia mtaji, gharama na kukupatia faida.Shoprite walipokuja walifingua masuper market lukuki, JM Mall, My Fair Plaza, Lumumba, etc, waliajiri wabongo, wamewaibia mpaka maduka yamefilisika sasa yamefungwa!. Mtu akileta Wahindi kwa sababu ni waaminifu ni makosa?,