Uhamiaji yamba wengine 25; Wapakistani 13, Wabangladesh 9 na Watanzania: Wengine watimka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhamiaji yamba wengine 25; Wapakistani 13, Wabangladesh 9 na Watanzania: Wengine watimka!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 4, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 4, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Idara ya Uhamiaji nchini ikiendeleza wimbi la kukabiliana na uhamiaji haramu leo imewakamata watuhumiwa wengine 25 na kuwafikisha mahakamani ambapo pamoja na kupigwa faini wanaandaliwa utaratibu wa kurudishwa makwao na wale ambao wataweza kuombewa vibali vya kuishi au kufanya kazi Tanzania


  Wahamiaji hao walikamatwa usiku wa kuamkia leo kuanzia saa saba hivi baada ya ya idara hiyo kupokea taarifa za siri za kuwajulisha uwepo wa wa wahamiaji hao haramu. Wahamiaji 13 wa Kipakistani walikamatwa Kariakoo nyumbani kwa Mtanzania mwenye asili ya Pakistani Bw. Mohammed Raza (43). Taarifa ambazo FikraPevu imezipata zinaonesha kuwa hii ni mara ya tatu kwa Bw. Raza kukutwa akiwa anahifadhi wahamiaji haramu.

  Watuhumiwa wengine ni Wabangladesh 9 ambao walikamatwa huko Majohe, Ukonga njia ya kwenda Pugu. Watuhumiwa hao wa Kibangladesh walikamatwa katika nyuma ya mkazi mmoja aitwaye Farid Said Hussein ambaye ni dereva. Bw. Hussein ambaye ni Mtanzania amedai kuwa watu hao wanaletwa kwake na mtu aitwaye Hijaz na kuwa wanalipa Shilingi 6000 kwa siku kwa kichwa.

  SIMULIZI NA PICHA ZAIDI ZA OPERATION FIKRAPEVU.COM
   
 2. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kumbe wanaweza hawa jamaa wakiamua ? Waingie Samora na Bank M na maeneo kibao utawakuta .Je wachina wote wana vibali if I may ask please .
   
 3. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  MM lekebisha taito ili ieleweke vizuri from the begining, btw, good info. Thanks.
   
Loading...