Uhamiaji uwanja wa ndege wa Julius Nyerere "formally dia" wasaidia kupitisha madawa ya kulevya

KHRISHNA POO MIDJA

New Member
Dec 8, 2013
3
0
Katika hali isiyo ya kawaida leo majira ya saa mbili asubuhi nikiwa naelekea kanisani nilibahatika kupanda gari na vijana 2 kiume na 1 wa kike ambao sikuweza kuwafahamu haraka wakiwa na furaha kubwa na kumpongeza mkuu wa kitengo cha uhamiaji ktk uwanja wa kimataifa wa julius nyerere kwa kufanikisha ombi lao la muda mrefu kwake walilompelekea afisa huyo ili kuwazuia maafisa uhamiaji kuingia na simu ofisini.

Wamesema kwa hakika yule bwana anatakiwa kupewa pongezi kubwa maana madili yetu hapa ktkt yalibumba sana. Huku wakitoa kashfa kubwa kwa waziri waliyemtaja kwa jina la mzee wa pama nyeusi kwamba anajifanya kinara wa kuzuia madili yetu, wanasema sasa tumeweza uhamiaji sasa tunaingia polisi ili nao wathibitiwe kuingia na simu ofisini.

Vijana hao walisikika wakisema simu ni noma bwana, mi kuna jamaa tulingia bifu naye sasa aliposikia nasafiri kwnda zangu ng'ambo nahisi aliwapigia jamaa simu na kuwapa details zangu, wacha ile nafika tu pale uwanjani jamaa ananistopisha na kusema tunakuomba toa madawa yako. Bahati nzuri tulipiga dili kubwa sikuwa nimekwenda nayo nilikwenda tu kuchora laketi. Walijaribu kunipekue wakavuna ngedere tu.

Binafsi nahisi kama ni uzushi kama kweli wale jamaa walichokuwa wanakisema ni ukweli kwamba maafisa uhamiaji wamezuiwa kuingia na simu ofisni? Ninacho jua ni kwamba simu kwa afisa usalama yeyote yule ni muhimu sana ili kuwezesha kuwasiliana na wenzake kwa muda muafaka. Kama kweli hawa maafisa wanakataliwa kuingia na simu ofisini hili ni jambo la hatari sana ktk usalama wa taifa letu. Ni sawa na kuzuia kwa makusudi jukumu la usalama wa taifa. Afisa yeyote ktk maeneo nyeti kama hayo anatakiwa hata awezeshwe kuwa na kamera inayoweza kuchukua tukio kwa mbali kabisa ili kuimalisha usalama wa eneo hilo.

Sitaki kuamini kwa haraka kwamba kuna kizuizi kama hicho ktk eneo muhimu kama hilo. Na kama ni kweli basi kwa ushauri wangu tu ni bora mamlaka husika zikachukua hatua mathubuti haraka iwezekanavyo ikiwa ni pamoja ni kuangalia namna ya kuifanya hali hiyo isijirudie tena.

Taifa linaondokana na dhana ya analog na kwenda digital lakini wakati huo huo kiongozi kwa matakwa yake anaamua kuwazuia maafisa kuingia na simu ofisini ili kuzuia mawasiliano kwa makusudi ili kuharalisha vitendo vya kuhujumu utawala wa nchi.

Naomba mamlaka husika ifuatilie suala hili na kuangalia uhalali wake. Lisemwalo lipo na kama halipo basi linakuja.
 

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,817
2,000
Mkuu,
Hivi kazi ya kukagua mizigo ya wasafiri na kukamata madawa kama kuna madawa ya kulevya ni ya Uhamiaji kweli?

Uhamiaji kukataza watu wao kuingia na simu nafikiri ni kwasababu tofauti kabisa. Huko mwanzo pia kulikuwa na madai kwamba
wafanyakazi a uwanja wa ndege wakiwa na simu ndio wanapanga deals zao. Sasa wamekatazwa bado tunalalamika.

Wacha tuwapelekee wahusika ujumbe wako na kama kuna ukweli nafikiri wataufanyia kazi.
 

ilboru1995

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,329
0
Dawa za kulevya hugharamia propaganda za CCM ndiyo maana lukuvi alisema wakianza kutajana hakuna mbunge wa CCM atakae baki mle mjengoni... kuwafanya vijana kuwa mazezeta ni faida kwa CCM maana wakijitambua wataing'oa hata kabla ya uchaguzi mkuu...
 

KHRISHNA POO MIDJA

New Member
Dec 8, 2013
3
0
Mimi kama mutu mupenda tanzania hii nmesema kile nilichokisikia. Ni juu yenu kuendelea kupuzia hali hii. Na ndiyo maana nchi zetu haziendelei. Kila raia ana kazi ya kulinda taifa lake, kila raia ana haki ya kukamata dawa za kulevya maana ni janga la taifa ukisema kazi hiyo siyo ya uhamiaji wewe ni mjinga usiojua amana ya usalama wa taifa lako.

Hoja ya kusema ilisemekana hata wafanyakazi wa uwanja wa ndege walikuwa wanatumia simu kupitisha dawa za kulevya ni ujinga tu huo. Basi hata polisi na vyombo vingine wasiwe wanatumia simu ktk ulinzi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom