Uhamiaji rushwa nje nje: Nimeumia sana sicho kitu nilichotarajia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhamiaji rushwa nje nje: Nimeumia sana sicho kitu nilichotarajia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Profesa, Nov 11, 2011.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Nimetoka kubadili hati yangu ya kusafiria, hali niliyoikuta Uhamiaji siyo ile nilioiacha miaka saba liyopita ambapo tofauti na zamani, wafanyakazi wa uhamiaji wanakusaidia kujaza fomu na kukutengenezea nyaraka zoooote bila hata wewe kusogeza mguu hapo ulipo, ila tu ni kiasi gani ulichonacho. Nimeachana na mmoja aliyenitajia 250,000, nikaenda kwa mwingine nafuu kidogo 150,000 ah mwisho baada ya kuwakwepa wote nikaishia dirishani na shilingi 20,000 zaidi ya ile 50,000 ya kawaida ambayo unailipia bank. Passport au hati ya kusafiria inaweza kutoka ndani ya masaaa, ndivyo nilivyoambiwa! Siamini ninachokiona! Serikali ya awamu iliyopita ilikuwa imeshaweka sawa matatizo haya wakati inaondoka. Jamani basi tu sina hata point za kuongea maana nadhani kila mtu anajua inamaanisha nini kwa usalama na hali halisi ya nchi yetu kwa siku za hivi karibuni ...
   
 2. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Pole sana Prof. yalishanikuta hayo. Yani huko ni kunanuka...........................
   
 3. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  jamaa yangu aliondoka bongo wakati wa mzee ruksa, akaenda zake ughaibuni kutafuta riziki alirudi wakati wa mzee ben akaenda uhamiaji ku renew passport yake. Aliporudi alinisimulia kwa mshangao alivyo hudumiwa vizuri bila ubabaishaji, tofauti kabisa na hali iliyokuwepo wakati anaondoka kwenda ughaibuni. Mkuu ina maana tumerudi tena kule kule!
   
 4. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Huko ulikokuwa kwa miaka saba, kwa nini wasikupe hati ya kusafiria ya kwao?
   
 5. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wewe umetoka wapi? Haukujua toka Miaka Ile Uhamiaji ni Rushwa?

  Haya ngoja nikufundishe, chukua Gazeti la Uhuru angalia makala ya Uraia Uone Maraia kibao eti wanatafuta mtu anayeupinga uraia wake hapa Bongo

  Ni Michezo kama dau - Ma TX wote wakienda bongo wanabaki bongo kwanini?
   
 6. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  pole sana kaka ndiyo maana ikaitwa bongo. hata ndani ya nusu saa tu unapata passport yako safi unaondoka. uhamiaji sasa hivi kunakuwa na foleni sana hivyo wanatumia udhaifu huohuo kukuumiza. Hata documents zenyewe siyo ishu muhimu ni picha na kuchukua finger prints basi. nchi imebinafsishwa kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake. Passport za tanzania haziaminiki sana nchi za wenzetu maana wanasema ndiyo nchi inayoongoza kwa kutoa passport zake kwa wageni. mtu akitoka kongo na fedha zake ndani ya saa amepata passport ya tz anaomba visa mfano UK safi kabisa anaondoka kama raia wa Tanzania.
   
 7. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Siyo Uhamiaji tu! Idara nyingi za serikali ndani ya miaka 5 zimepanda chati kwa kula rushwa. Ulishaona wapi mkuu wa nchi anasema "Ukitaka kula kubali kuliwa kidogo". Viongozi wakuu wote wanakashfa za rushwa unategemea nini kwa wafanyakazi wanaopata mshahara usiokidhi mahitaji yao kwa mwezi?

  Matatizo mengi kwenye jamii yeyote husababishwa na viongozi! kama kiongozi nimtenda madhambi lazima jamii husika itakuwa ndani ya matatizo.
   
 8. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Ndugu naona ulikutana na vishoka, uhamiaji ni kati ya idara chache wanaotoa huduma nzuri iwapo hutajaribu short-cut. Siku nyingine fuata utaratibu uliowekwa na hakuna atakayekuomba rushwa.
   
 9. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #9
  Nov 30, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Hakika rushwa ipo kila mahali....na hao uhamiaji wanakula rushwa! Uhakika ni kuwa rushwa hatutaimaliza kama sisi wenyewe hatutaki kufuata utaratibu. Ukitaka shortcut unatengeneza rushwa. Usimlaumu unayempa, jilaumu unayependa kushorten everything. Mimi nimeenda kutafuta pasipoti uhamiaji - kweli niliona usumbufu. Wanahitaji vingi muno! MARA, CHETI CHA KUZALIWA, KIAPO CHA MZAZI, BARUA YA MWALIKO, MARA NIKASHUHUDIWE ETI KWA WAKILI, SIJUI STEMPU DUTY...NK. Nilihangaika ila nilipokamilisha vyote nimeipata pasipoti yangu kwa kulipa 50,000/= tu, tena benki. Ukiweka lugha za nisaidie kurekebisha mambo mengine unaiita RUSHWA!
   
 10. B

  Bi Mashavu Member

  #10
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani tuwe wakweli tu, hatutaki kufuata taratibu zilizoweka na hiyo ndo gharama yake! Katika idara za Serikali ya JMT zinazofanya kazi vizuri tena bila bugudha kwa wateja wake basi Uhamiaji ni moja kati ya idara hizo (mimi kama raia wa kawaida nimehudumiwa mara kadhaa kwa mujibu wa taratibu sijaona kikwazo chochote). Hakuna kucheleweshwa wala kuombwa rushwa! Sasa wewe unakwenda leo na unataka hati yako leo leo wakupe bure! Fuata taratibu unazoambiwa tafadhali.
   
 11. clet 8

  clet 8 JF-Expert Member

  #11
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 1,065
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Unapoona hali kama hizo katika ofisi za serikali na idara zake tumepungukiwa na uadilifu na ktk mwenendo kama huo usitegemee maendeleo. Tutabaki kuwa shamba la bib milele.
   
 12. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #12
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  JAMANI MIE NILIOMBWA SHILINGI LAKI MOJA NA NUSU ILI NISHUGHULIKIWE PASSPORT YANGU.
  LAKINI FOMU YENYEWE IMEANDIKWA SH. ELFU HAMSINI TU. NA HUYO BWANA ANANIAMBIOA HAYO PASIPO AIBU WALA HAYA.

  jamaaani UHAMIAJI kumeoooza, kunanuka, kazi haziendi bila RUSHWA.

  Nahodha, Pinda na Rais Kikwete Tafadhali geukieni UHAMIAJI hali ni mbaya sana, SAIDIENI WANANCHI WENU.
  MUNGU TUSAIDIE.
   
 13. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #13
  Nov 30, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,495
  Likes Received: 2,739
  Trophy Points: 280

  Hivi unajua hati ya kusafiria inayozungumziwa hapa au?? Ni passport !!!!!! Sasasijui unataka professor abadilishe uraia wake ama?? Tungekuelewa kama ungeuliza kwa nini hakuombea ubalozini huko huko aliko?? Lakini pia jibu ni sio kila mahali tuna balozi halafu inachukua muda mrefu kuipata ukiombea ughaibuni!!!
   
 14. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #14
  Nov 30, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ndio maana tunataka kuliachia li-nchi lao. Upumbavu kila kona...
   
 15. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #15
  Nov 30, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Sipingi suala la rushwa uhamiaji hilo lipo tena lipo sana sana, kwa ujumla kila mtendaji wa serikali anatafuta mbinu ya kunufaika pale alipo, mbinu hizo ni pamoja na kukuchelewesha makusudi, kuficha file na kila ukijuacho.

  Kitu ninachopinga ni kusema serikali ya awamu iliyopita iliyaweka sawa haya hapo nakukatalia labla useme serikali hii iliyaweka sawa haya katika muhula uliopita. Wakati wa Mkapa Uhamiaji ilikuwa balaa sana, kupata document yako ilikuwa ni shida sana. Katika miaka ya mwanzo ya JK wakati wa Kinemo Kihomano alijitahidi kufuta uoza aliotoka nao kwa Mkapa ili alinde nafasi yake na kujaribu kupunguza bughudha za ucheleweshwaji wa Pass japo rushwa haikuisha. Kwa ujumla ni kwamba Rushwa ni sehemu ya utendaji kazi serikali katika kila kona kila idara. Hakuna wa kumshughulikia mwenzake ni kama vile wewe na mkeo mnakutana guest, hakuna wa kumuuliza mwenzake umefuata nini huku.

  Wakati wa Kikwete Rushwa imezidi sana tu ila kilichoongezea ni utandawazi ambao unaiweka wazi rushwa kitu ambacho kilikosena wakati wa mkapa na watu kuishia kusemea chinichini.

  Kosa lako kubwa wewe ni kukubali kutoa rushwa ili mambo yako yafanikiwe, ungeamua kutotoa rushwa na pengine kuweka mitego kwa ksuhirikiana na TAKUKURU ungekuwa umelisaidia taifa kwa nafasi yako. Ila kama unaogopa revenge inabidi ule jiwe tu, maana ukikubali kuwa mwana ndoa basi ukubali na kulala...
   
 16. Ngararimu

  Ngararimu Senior Member

  #16
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Acha upumbavu inawezekana wewe ni mmoja kati ya wala rushwa wanaotesa jamii ya walala hoi wa tanzania huyu mwananchi inawezekana anasafiri sana na pass yake imejaa mihuri anatakiwa apewe nyengine au imeisha muda wake. Hivi ulitaka nchi gani impe pass wakati yeye ni mtanzania?? Kweli siku sheria kunyoga wala rushwa na mahakama pamoja na mnyongaji wakawa hawali rushwa 90% ya wafanyakazi wa serikali ya TZ watanyongwa.
   
 17. Ngararimu

  Ngararimu Senior Member

  #17
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 30, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Kosa lako kubwa wewe ni kukubali kutoa rushwa ili mambo yako yafanikiwe, ungeamua kutotoa rushwa na pengine kuweka mitego kwa ksuhirikiana na TAKUKURU ungekuwa umelisaidia taifa kwa nafasi yako. Ila kama unaogopa revenge inabidi ule jiwe tu, maana ukikubali kuwa mwana ndoa basi ukubali na kulala...

  Hili la kuwahusisha takukuru lingemgarimu pesa nyingi zaidi kwani hawa wanaongoza kwa rushwa kuliko uhamiaji. kesi ya ngedere unampelekea nyani? wewe unaishi bongo kweli?
   
 18. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #18
  Nov 30, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  watu tusiandike tu kiushabiki. Sitaki hata kukumbuka jinsi nilivyonyanyasika pale uhamiaji kipindi cha mkapa wakati na shughulikia passport yangu. Narudia, tusiandike tu kiushabiki kwa sababu ya chuki. Binafsi yalinikuta.
   
Loading...