Uhamiaji: Paspoti zinazotolewa siyo vitambulisho ndani ya nchi

Kamishina mbn kaeleweka jaman, kwa sasa nchi ina kitambulisho rasmi cha taifa almaarufu kitambulisho cha NIDA.. Passport inabaki tu km hati ya kusafiria. ugumu wa kuelewa upo wapi watanzania wenzangu!?
 
Huu ni upuuzi,hakuna kitambulisho kinachomtambulisha mtu vema kama pasport,hii inakuwa na guarantee kubwa kuliko vitambulisho vingine ambavyo ni rahisi kufoji!
Ijulikane ili kupata passport ni lazima uwe umepeleka cheti chako cha kuzaliwa,cha form 4,form 6 kama kipo,vyeti vya wazazi vya kuzalwa,barua kutoka mtendaji wa eneo unaloishi,picha zako na pia unaacha finger prints!

Ni kitambukisho gani kingine ambacho walau hupatikana kwa kutoa information nusu ya passport????

Kinachofuata kwa mbali sana ni leseni ya udereva!!!!
So ni uchizi kusema passpirt isitumike kama utambulisho nchini!!!
Mama MTU Mzima kazaliwa 1945. Hana birth certificate. Hajafika seko, hajasoma. Anataka kusafiri nje ya nchi. Hatapata hiyo pasi ya kusafiria? Barua ya VEO au WEO zinatosha?
 
Kwa kuwa Tanzania, tulio wengi hatuna IDs,tunatumia docs zifuatazo kama utambulisho.
1: Vote cards
2: Driving License
3: Bank Cards
4: Political parties cards
5: Passports
6: Health insurance cards
7: Schools/ College certificate.
Lengo kurahisisha utambuxi.
 
NIDA wanatumia passport kama kitamburisho cha kupata kitamburisho cha uraia, kwa vile wanaamini kwamba uhamiaji walikufanyia interview. ila wamesahau kama kuna wengine wamepata passport wakiwa nyumbani, walienda uhamiaji kwa ajili ya fingerprint kila kitu shortcut. tujisahihishe tusonge mbele
Sio kweli. NIDA wanahitaji kupata taarifa nyingi iwezekanavyo za RAIA wake.
Ndio maana wanaomba hadi vyeti vya shule, TIN number, card ya Mifuko ya jamii, Post codes, mtaa, ulipozaliwa,jina lako maarufu (aka). Hiyo ni full details.
 
d7fa29a82f92ece55b233eca493955c4.jpg

Hatutumii majina feki kijana sisi,
Nenda kachukue kitambulisho cha Taifa..!!
Huna passport wewe!Unalopoka tu mambo usiyojua!Ndio tatizo la watu kujifanya wachangiaji kwa kila jambo!Nenda na hivyo vitu ulivyotaja kama utapata hiyo passport!!!!
 
Ukitaka kukipata leo hicho cha NIDA utakipata?Halafu hicho cha NIDA kina require less information kuliko passport!
Waziri Kivuli usitulishe tango pori. NID kina much requirements than any ID in Tz. Mpaka post codes or zip codes are needed.
Acha bwana. Don't be too much knows but know nothing.
 
Huu ni unaa na roho mbaya tu. Imekuwa kama vile kila mwenye cheo anapaswa kufanya ukuda fulani hivi kwa wananchi ili aonekane anafanya kazi.

Sasa subiri huyu dogo atapandishwa cheo kwa huu unyambirisi aliofanya. Baada ya hapo utasikia TRA nayo ikikatazia driving license kuwa kitambulisho, na tume ya uchaguzi ikikatalia vitambulisjo vya mpiga kura. Sii ajabu NIDA nao watasema vitambulisho vya utaifa havihusiani na kumtambulisha mwanachi isipokuwa kwenye sijui utaahira gani.

Mwisho wa siku itatamkwa kuwa kila mtu aende kwenye idara fulani ya kizembe akajiandikishe katika muda wa siku saba na baada ya hapo ni faini au kufutiwa uraia.
 
Huu ni upuuzi,hakuna kitambulisho kinachomtambulisha mtu vema kama pasport,hii inakuwa na guarantee kubwa kuliko vitambulisho vingine ambavyo ni rahisi kufoji!
Ijulikane ili kupata passport ni lazima uwe umepeleka cheti chako cha kuzaliwa,cha form 4,form 6 kama kipo,vyeti vya wazazi vya kuzalwa,barua kutoka mtendaji wa eneo unaloishi,picha zako na pia unaacha finger prints!

Ni kitambukisho gani kingine ambacho walau hupatikana kwa kutoa information nusu ya passport????

Kinachofuata kwa mbali sana ni leseni ya udereva!!!!
So ni uchizi kusema passpirt isitumike kama utambulisho nchini!!!
nasubiri na tra waseme driving licence sio ID isitumike
 
Sio kweli. NIDA wanahitaji kupata taarifa nyingi iwezekanavyo za RAIA wake.
Ndio maana wanaomba hadi vyeti vya shule, TIN number, card ya Mifuko ya jamii, Post codes, mtaa, ulipozaliwa,jina lako maarufu (aka). Hiyo ni full details.
 
Passport=hati ya kusafiria
ID=kitamburisho cha uraia
Tuache mazoea, tuangalie wenzetu wanaishi vipi, dunia imekuwa kijiji tuangalie vijiji vya wenzetu wanaishi vipi.
Hao wenzenu wanoishi vipi ni akina nani? Passport is a valid identinty and can be used to identify a person if need arise anytime, anywhere because it is linked to ones personal information and finger prints. So can be used as an ID, and is being used as an ID worldwide.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IDARA ya Uhamiaji nchini imewataka wananchi kutambua kuwa paspoti siyo kitambulisho ndani ya nchi na kwamba kisitumike kwa matumizi hayo kwa sababu siyo utaratibu uliopangwa kisheria ndani ya mipaka ya nchi.

Pia amesema kuwa ikibainika kuwa mtu amepoteza paspoti hiyo kizembe hatopewa nyingine. Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Uhamiaji- Pasi na Uraia, Gerald Kihinga wakati alipofanya mahojiano maalumu na gazeti hili, na kuwaomba wananchi kutambua kuwa paspoti zinazotolewa zinapaswa kutunzwa na kutumika kwa lengo lililokusudiwa la kusafiria nje ya nchi.

Kihinga alisema kumekuwa na maombi ya kutengenezewa paspoti baada ya kupotezwa, lakini wengi wamekuwa wakitoa sababu ambazo zinatilia shaka umakini wa mtu kwenye utunzaji wake. “Naomba mfahamu kuwa paspoti pia zinazotolewa siyo vitambulisho ndani ya nchi hivyo visitumike kama vitambulisho na tena si vizuri kutembea nayo kila mahali kama huna safari ya nje ya nchi.

Paspoti au hati ya kusafiria zinatumika kama kitambulisho pale unapokuwa nje ya nchi, lakini matumizi yake rasmi ni ya kukusaidia kuingia na kutoka nchini,” alisema. Alisisitiza kuwa kitambulisho rasmi cha Mtanzania anachotakiwa kutembea nacho ni kile kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Aidha, kamishna huyo pia ametaka wananchi raia wa Tanzania kutambua kuwa wanaweza kupata paspoti wakiwa popote Tanzania na kwa muda mfupi.

Chanzo: Habarileo
Mtu kasafiri miaka 10 iliopita lakini passport haikauki mifukoni,kisa umaarufu kuwa yeye huwa anatokaga,kwa mtindo huo zitaacha kupotea...

Sony Z3
 
Unajua kama kitambulisho cha Taifa unapeleka cheti cha kuzaliwa mama&baba shule walizosoma n.k ?
Au hujawahi kuchukua kitambulisho cha Taiga..!?
Passport unapeleka cheti cha darasa la saba,form four,form six au
Kwa hiyo ni uchizi kufananisha passport na kitambulisho cha Taifa....!!
Nafikiria hujawahi kuchukua passport wala hujui passport ni nini ni bora unyamazee.
 
Back
Top Bottom