Uhamiaji: Mchungezeni mrembo Richa Adhia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhamiaji: Mchungezeni mrembo Richa Adhia

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Malafyale, Mar 19, 2010.

 1. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,209
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Richa Adhia alikuwa mrembo aliyetuwakilisha wa Tanzania kwenye mashindano ya urembo ya dunia mwaka 2007 huko China,na hadi kuna picha nyingi zilionyesha Waziri wa Utamaduni akimkabidhi bendera ya Tanzania akaipeperushe vyema huko China!Kwa kutuwakilisha nje ya Tanzania,nina imani kabisa akina Lundenga walihakiki kama mdada huyu ni Mtanzania!

  Lkn hivi karibuni zimeonyeshwa picha mrembo huyo huyo akiwa na Balozi wa India nchini Tanzania akimuaga tayari kuelekea Africa kusini kwenye mashindano ya Miss India Worldwide na hiyo kama atashinda sasa atakuwa na sifa ingine ambayo ni "Miss India Worldwide"!

  Swali,Je Tanzania tayari imeruhusu 'dual citizenship'?Maana nina amini hadi kupata nafasi ya kwenda kushindania Miss India Worldwide huko Africa Kusini lzm waandaji wake walihakiki kuwa mrembo huyu ni "mwenzao",na pasipo kutia shaka kabisa dada huyu anakwenda huko kushindana kama raia wa India maana haiingii akilini kuwa ataonyesha passport ya Tanzania kwenda kushindania Miss India tena nje ya Tanzania!

  Uhamiaji mchungezeni mrembo huyo maana likely kama ana miliki passport za nchi 2 tofauti jambo ambalo bado sio ruhusa nyumbani Tanzania!Sheria ya Tanzania inasema ukifikia umri wa miaka 18 inabidi uape kuukana au kuukubali uraia wa Tanzania kama itatokea kuna ulazima wa kufanya hivyo!

  Mchungezeni haraka kabla hajaleta madhara kwenye chaguzi zetu,kama ana uraia wa nchi 2 tofauti basi sheria ichukue mkondo wake!
   
 2. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mie hata sijaelewa lile taji walilompa hivi karibuni bado nipo njia panda!
   
 3. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Mitanzania mingine ina wivu wa kijinga sana. Inakuuma kuona huyo mdada ana miliki passport mbili?.
   
 4. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160

  Mhh kuna siku nilisikia rais alisema haiwezekani kuwa na dual na akadai mnataka kula huku na huku???:confused:
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Jamani eeh! yale mashindano ya Miss India Worldwide ni utambuaji wa Wahindi wanaoishi nje ya India. Ndiyo maana balozi wa India alikuwepo kwenye hafla ya Richa. I did not read anything in it more than that.
   
 6. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  JK alisema kuna baadhi ya wasomi pale chuo kikuu Dar ndiyo walikuwa na kauli hiyo ya kula huku na huku, lakini hii issue ya dual inafanyiwa kazi na bila shaka itapita tokana na ukweli kwamba lina faida nyingi kuliko hasara.
   
 7. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,209
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Sio wivu wa kijinga bali ni kinyume cha sheria za Jamhuri ya Tanzania kuwa na passport mbili ukifikisha umri zaidi ya 18.

  By the way,could you present your arguments with respectful manner without to insert any abusive languages?

  Kidatu,unapopinga hoja jaribua kuandika bila kutumia lugha za hovyo hovyo!
   
 8. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,209
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  According to you ,Kwa hiyo Radhia ni Muhindi?Ni kitu gani sasa kinachofanya Radhia atambuliwe kama Mhindi?
   
 9. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Nadhani unaconfuse issues, Indian ni both race and nationality.
  Unaweza kuwa Indian lakini una nationality ya Tanzania. Anyway kuna matatizo makubwa zaidi ya kuchunguza nchi hii.
   
 10. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Jiheshimu kuwa na akili timamu,sio kutoka kwenye mipombe yako ya kienyeji huko unakuja humu kutukana watu.Jibu hoja au mueleweshe aelewe pale ambapo hajaelewa.Unajua mwelevu kumjibu mjinga wewe ndo unakuwa ......kama hujafurahia hii thread si utafute zingine uchangie?
   
 11. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2010
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,650
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Kutoka kwenye tovuti ya Miss India Worldwide tunaweza kusoma:

  http://www.worldwidepageants.com/randrww.htm

  1. WHO CAN PARTICIPATE: Any woman of Indian origin (regardless of her place of birth) between the ages of 17 and 27 inclusive (on December 31st of the year she participates), never married and never having had a child, is eligible to participate. The delegate must be a resident, citizen or born in the country she will be representing. Appropriate documentation regarding the age and residency status of the delegate must be submitted in order to meet the eligibility requirements.

  Kwa vigezo hivi, Richa Adhia siyo lazima awe raia wa India ili aweze kuiwakilisha Tanzania kwenye Miss India Worldwide.
   
 12. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ........Radhia ni mtanzania mwenye asili ya kihindi, na hili shindano linawahusu miss wa nchi yoyote duniani mwenye asili ya kihindi.Hivyo ni halali yake kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya miss wa kihindi duniani.
  Mie sioni tatizo lolote hapa, zaidi watu tumezidi kulalamika, na huyu binti anatumia passport moja ya Tanzania. Hongera zako Radhia na nakutakia kila la kheri ushinde huko ili urudi na ushindi wako hapa nyumbani.
   
 13. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #13
  Mar 19, 2010
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,209
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Unahisi kwenye mashindano haya ya SA wasifu mkuu wa kuwa mshiriki na hata kushinda Miss India Worldwide ni rangi ya mshiriki?
   
 14. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #14
  Mar 19, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  (a) Huyo aliyeweka hiyo post inaelekea kuwa hakujua kuwa dada huyo alikuwa anashiriki mashindano ya watu wote duniani wenye asili ya kihindi bila kuangalia uraia wao. Zamani watu wenye asili ya kiafarika nao walikuwa na kitu kinaitwa FESTAC, lakini sijui kiliishia wapi. Dada huyo ni mtazania ila ana asili ya kihindi hivyo anaruhusiwa kushiriki mashindano yale.


  (b) Pamoja na huyu jamaa aliyepost kutokujua hilo hapo juu, jibu lako ndugu Kidatu ni mediocre sana. Mentality hii inachangia sana kutufanya tusiendelee kwani tunakaa kimya badala ya kuchukua hatua za kieshria tunapoona mtu anaiba mali ya umma kwa kuamaini kuwa kufanya hivyo ni wivu wa kijinga. Kuna waliojua kuwa Chenge kaiba lakini hawakusema kwa kudai huo ni wivu wa kijinga. Tutafika lini kama hatuwezi hata kutetea sheria zetu?
   
 15. M

  MLEKWA Senior Member

  #15
  Mar 19, 2010
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [UJINGA WETU WENYEWE WATANZANIA .
  Nani atakataa tukisema tuna waTanzania intelligence unit yetu imejaa Wahutu na Warundi ?
  Kuna ajabu gani kuona tuna mbunge muhutu m waziri mtusi wakati hatuna system ya kuulinda utanzania wetu vyeti vya kuzaliwa vinauzwa sokoni kariakoo nusu saa tu untolew cheti cha kuzalia nani asiejua kuna maelfu ya Wazimbabwe wameningia Marekani kwa kutumia uraia wa Bongo kial mmoja ukimuuliza ulipataje passsport wanakuambia tuliuziwa Arusha ?
  Ilikua nchi pekee kwa sisi kupata passport kama papai ni aibu kuona watanzania tuko uchi ?
  Miaka mingapi imepitishwa sheria ya ID kila mtanzania kuwa na ID nini kimeshindikana , nilisikia tenda ya ID ilitolewa na Mkapa na leo Kikwete utawala wake unamalizia kipindi cha mwanzo bado Mtanzania under CCM rule National ID ni ndoto ya mchana .

  Tusipige kelele kuwa na Wazambia , wamalawi wanatuongoza kwa vile hatuuthamini utanzania wetu tunachothamini ni ile picha ye Nyerere na Karume kuchanganya Udongo nyuma ya pazia ila ukweli Watanzania hatuelezwi , imekuaje Tanzania tunaambiwa ni nchi moja ila Wazanzibari wana Zanzibar NAtional ID uko wapi ule udongo ulio changanywa na Mchonga na Karume ?
  Acheni kuwabagua raia wasiokua weusi lazima tukubali kama wenzetu taifa kubwa duaniani USA wanapokiri kuwa immigration system is bad as Tanzanian I will call our system terrible , any one can land in Tanzania next day can fly to any where with bongo Passport.
  We need to have one office which control birth certificates and National ID as well passports ili kupunguza usumbufu kwa wazawa wa nchi hii.
  We need to reduce cost by implementing this sytem with today technology.
  Inakuaje leo Zanzibar ikiwa huna ID huwezi kujiandikisha kupiga kura ila Ukiwa Mbeya unaweza kujiandikisha na kuwahonga raia wachache wa Zambia kujiandikisha kupiga kura hii ndio siri ya CCM inatumia raia wa kigeni miaka mingi walioko mipakani kupiga kura na kujitangazia ushindi mnono ukweli wanaoiweka CCM madarakani sio watanzania bali ni wageni wanaoletwa kutoka kwenye mipaka yetu , Congo ,Uganda na waburundi kupiga kura kule Kigoma.
  Hiii ndio Siri ya CCM kuogopa kuwapa watanzania National ID kwani wanajua kuwa watkosa maelfu ya wapiga kura na pia wanhofia kuwapa uraia wageni hawa kwani hwana uhakika kuwa hapo baadae watawapigia kura kwani sasa hivi wanapiga kura kwa kuhongwa mamilioni ya pesa.
  Watanzania amkeni nchi yenu inamalizwa na wageni.
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Mar 19, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Haya, tusema ni Mtanzania mwenye asili ya Kihindi. Does that make it better for you?
   
 17. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #17
  Mar 19, 2010
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Hahaaaaaa,Malafyale bwana...Sasa si ni bora ungejituma hata kuingia kwenye hiyo website ya hao jamaa wa Miss India Worldwide kabla ya kuja hapa na kuwataka Uhamiaji wamchunguze Richa...Soma post ya Ndjabu hapo juu,ni fupi lakini inaeleweka:

  1. WHO CAN PARTICIPATE: Any woman of Indian origin (regardless of her place of birth) between the ages of 17 and 27 inclusive (on December 31st of the year she participates), never married and never having had a child, is eligible to participate. The delegate must be a resident, citizen or born in the country she will be representing. Appropriate documentation regarding the age and residency status of the delegate must be submitted in order to meet the eligibility requirements.

  Ni vizuri tukafanya utafiti japo kidogo kabla hatujaja JF na tuhuma za aina hii

   
 18. M

  Mwano Member

  #18
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  rangi si tatizo, umejuaje kama ana p/port 2?
   
 19. M

  Mwano Member

  #19
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ukabila unavunja maendeleo!
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Tatizo yawezekana ni Uhindi wake na siyo suala lake la Uraia. Siku za karibuni kuna kitu nimeanza kunotice tabia ya kuwa bash Wahindi kwa kile mtu anafikiria anaonesha uzalendo. Malafyale sijaona kwenye mada yake ya kwanza akitaja "uhindi" wa Radhia ila alikuwa anoji "Uraia".

  Bila ya shaka aliamini (kwa makosa kama ilivyooneshwa) kuwa wagombea wa Miss India Worldwide ni lazima wawe "raia wa India". Bahati nzuri kama ilivyo Tanzania India haitambui Uraia wa nchi mbili kikatiba. Inatambua kile kinachoitwa " Overseas Citizenship".

  Lakini tukiachana na hilo (kwani limeoneshwa pasipo shaka kuwa Richa anaweza kugombea) ni lazima tuanze kuangalia hoja ambayo imeanza kuota mizizi kuwa Utanzania ni sawasawa na "Weusi". Wapo wanaotaka tuamini kabisa kuwa Mtanzania ni "mtu mweusi tu" na mwingine yeyote hata kama anatimiza masharti yote ya kisheria ya kuwa raia wa nchi yetu basi "si mtanzania kamili".

  Hata hivyo utaona kuwa tatizo kubwa katika hili haliko kwa Wamarekani (weupe) waliochukua uraia wa Tanzania, Wajapani waliochukua uraia wa Tanzania au hata Waingereza waliochukua uraia wa Tanzania. Hawa wataonekana ni Watanzania hata kama rangi zao si nyeusi. Inapokua Wahindi tunajikuta tunachanganya mambo mengi kiasi kwamba tunafikia kuwalundika Wahindi wote kuwa si Watanzania.

  Tukikubaliana na dhana hii utaona kuwa tuko tayari tuongozwe na fisadi mweusi au kiongozi mbovu mweusi kwa sababu tu ni mweusi lakini tumkatae kiongozi mwadilifu ambaye ni Mhindi! Lakini watu hawa hawa wanaweza kuwa wanaona furaha kwa Obama kuwa Rais wa Marekani na wanakubali jinsi gani Marekani imeanza kuingia kipindi cha "post racial" kwa kumchagua mtu wa minority kuwa Rais wao lakini wakija Tanzania kumchagua mtu wa minority group inakuwa ni vurugu.

  Binafsi ningependa kuona:

  Mojawapo ya nafasi za juu katika Tanzania inaenda kwa minority Group.. Mwanasheria Mkuu, Jaji Mkuu, Mkuu wa Majeshi, Mkuu wa Polisi, Spika n.k Wakati wa Mwalimu hili halikuwa shida sana kwani alikuwa anataka kuonesha ukweli kuwa Tanzania ni moja na binadamu wote ni sawa. Leo hii hili haliwezekani tena. Kikwete hana ujasiri wa kufanya hivyo na tunaanza kurudi pole pole kujificha kwenye gamba letu!

  Yale ya msingi ambayo yaliifanya Tanzania kuwa Tanzania tunaanza kuyakana pole pole huku tukifikiria ni Uzalendo!
   
Loading...