Uhamiaji kwa kufukuta,rais atakiwa kumuondoa mgonja na kuteuwa makamishna kujaza nafa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhamiaji kwa kufukuta,rais atakiwa kumuondoa mgonja na kuteuwa makamishna kujaza nafa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by rungulugujo, Dec 26, 2010.

 1. r

  rungulugujo New Member

  #1
  Dec 26, 2010
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuteuliwa kwa kamishna Mkuu NDG Ulungi kulitegemewa na Wengi na watumishi wanamwamini na wanampongeza rais Jk kwa uteuzi huo ulungi siyo fisadi na ni mtu wa kufuata sheria asiye na majungu.Hata hivyo IKULU baado inalaumiwa kwa chombo kikubwa kama hiki cha ulinzi na usalama kushindwa kuwateuwa Makamishan wengine ambao nafasi baado ziko wazi hali imepelekea Idara sasa kuongozwa na mtu mmoja tu kamishna wa utawala na Fedha ambaye anaipeleka Idara pabaya kwani amekuwa akiifanya Idara hii ni mali yake na kujifanyia maamuzi kivyake bila ha ta kuwashirikisha viongozi wenzake,kamishana huyu MGONJA kwanza aliinigia kwenye nafasi hii muhimu kwa kubebwa na kamishna mkuu Mstaafu ndg KIHOMANO ili kulinda maslahi yake ya kifisadi kwani hana taalauma ya utawala na Fedha na aliyeshinda nafasi hiyo wakati huo ni ndg MBUYA ingawa KIHOMANO kwa kutumia ushrika wake wa karibu ndg LUMBANGA alishinikiza nafasi hiyo apewe MGONJA,Dhambi hii ndiyo inayoitafuna Idara na Watumishi wamezamilia sasa kuanika Uozo wote anaoufanya wa UFISADI,UKABILA,MAJUNGU anayoyafanya idarani.
  NDG MGONJA ameendekeza ukabila kwa kuwateuwa Wachagga na wapale kushika sehemu mbalimbali zenye maslahi nayeye kama vile Uteuzi wa RIO kwa mikoa yenye Neema kama ARUSHA,mipakani wamejaa wenzake,Viwanja Vya Ndege usiseme.mfano tarehe 01/04/2010 dada mmoja aitwaye SHARIFA alihamishiwa wilaya ya TEMEKE lakini kwa mshangao yeye tu hakuchukua hata mwezi akahamishiwa JNIA je yeye ana sifa gani muhimu za kupekwa huko?
  PIA ukienda kitengo cha Pasipoti utakuta kuna watu wanazeekea pale hawahami kama vile mleka,lilian malekos,mwansasu,na wengine lakini kuna watu hata mwaka wanahamishwa kwa kusingiziwa makosa.Kitengo cha hati ndiyo usiseme kwani wamepanga safu zao anzia SHAYO NYANGE,MAGADULA huyu ananyota Mbili lakini cha ajabu DCI,SACI,ACI n.k wanalipoti kwake kwanini ??kama siyo mtandao''''''.Angalia kule TIC watu walihamishwa lakini walichanga Fedha na kutoa kwa wakubwa na uhamisho kufutwa licha ya Aliyekuwa akikaimu nafasi Ya kamishna mkuu kuelekeza nafasi hizo kuwa za mzunguko.Nenda uraia watu wanajichuulia fedha za malipo ya uraia bure kwani hakuna AUDITING inayofanywa kuonyesha uwiano wa vyeti vinavyotolewa na fedha inayokusanywa.
  LAKINI pia MGONJA analalamikiwa kuwa na watu wake anaowabeba wakiwemo wanawake wa kipale na hawara zake ambao hawa hawahamishwi licha ya kukaa muda mrefu angalia kitengo cha Sheria,Utumishi n.k watumishi pia wanaul;iza kuna sheria ambayo zamani ilikuwa inatumika kuwa kwa VYEO fulani kama huna mke hurusiwi kuteuliwa mbona huyu hana mke na karibia anastafu sheria hiyo iko wapi?
  MGONJA ananlalamikiwa kuwa mtu wa majungu bila hata kufanya upembuzi matokeo yake amekuwa akifanya maamuzi yanagusa vibaya maisha ya wafanyakazi.
  RAIS mwondoe katika nafasi hiyo ukitaka Idara hii pamoja na kamishna mkuu mpya afanye kazi kwa mafanikio.
  PIa ULUNGI azifanyie mabadiliko ikiwemo kuomba maafisa UTUMISHI raia na Kumuondoa baadhi ya maafisa mipango ambao hawana tija kwa idara.
  UPANDISHAJI vyeo nao ni UFISADI kwani kuna watu walipanda mwaka jana lakini wamepanda tena safari hii huu ni UHUNI????
  mATUMIZI mabaya ya kulipana POSHO tu makao makuu kwa safari na vikao hewa visivyokuwa na Safari report ziangaliwe na ulipaji wa posho bila kaangalia vyeo rate viangaliwe
  KATIBU MKUU,WAZIRI PAMOJA NA DAP IANGALIENI SANA IDARA HII
   
 2. M

  Mpwa Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 54
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Umejitahidi kuichambua Hii Idara ya kifisadi Ila tatizo wengi hawaijui Uhamiaji hata hao viongozi; Naskia kuna Afisa kajiua sababu ya huyo Mgonja kutomlipa fedha zake za uhamisho wa sehemu zote alizo muhamisha; sasa sijui hatma ya maafisa 14 walio hamishwa Arusha kwa zengwe:
   
 3. October

  October JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  ??????????
   
 4. z

  zamlock JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  mgonja ni nani kwenye maisha ya watanzania? Tena damu ya huyo aliyejiua itamlilia siku zote za maisha yake na familia iliyokuwa inamtegemea itamlilia mgonja mpaka mwisho wa maisha yake na atakosa amani siku zote za maisha yake
   
 5. K

  Kufakunoga Member

  #5
  Dec 30, 2010
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  labda niwape historia fupi wana JF kuhusu huyu mgonja aka mgonjwa,huyu alikuwa ni afisa sheria wa idara ya uhamiaji,ni mwanasheria by proffessional,lakini kuna tetesi kwamba alikuwa ni chakula cha mkurugenzi wa uhamiaji aliyemaliza muda wake bw.kihomano,na hizi tetesi uenda ni za kweli kwasababu alimpigania mpaka akampa nafasi ya kamishna wa utawala na fedha wakati hana sifa za nafasi hiyo is just a mere lawyer by professional watu wenye sifa walinyimwa nafasi hiyo na kupewa yeye kwa kulipa fadhila.kinachoshangaza ni kwamba bwana mgonja umri wake ni almost miaka 54 lakini hana mke wala mtoto wa kusingizia,muda wote huo amekuwa bwabwa la kihomano.jamaha ana roho mbaya mambo ya utawala awezi kabisa,mawazo yote ni rushwa,kama upo kwenye nafasi nzuri lazima akusumbue sana kwa kukuuliza kwanini upeleki returns kwake,ukikosa jibu anakupiga uhamisho,alishawahi kusimamishwa kazi kwa ajili ya rushwa,jamaa ana roho ya kifisadi vibaya mno.hatujui pesa anapeleka wapi kuna tetesi kwamba uwaonga vijana ili wamshughulikie kikamilifu,na inawezekana kwasababu kamishna wa utawala na fedha kuishi bila familia inashangaza sana
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,132
  Likes Received: 5,571
  Trophy Points: 280
  huku ampati msaada

  njooni ufufuo na uzima mkatolewe mizimu ya misukule ya kukataliwa baadae mnamisha hyo gonja sijui mbonja kwenye ulimwengu wa kiroho bila wasi wasi
  karibuni usiogope sadaka ni hiari ila muhm kumtolea bwana mungu
  apokeae bure amelaaniwa unalijua hili??
   
 7. L

  Leornado JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hii inasound kama bosi wangu katili jaluo moja baya sana i wish lirudi kwao. sorry kwa kwenda nnje ya mada.
   
 8. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Du namjua huyo Kijana aliejiua anaitwa Giriki......alikuwa kijana safi sana wa Kondoa huko....ila JK ana kazi kubwa sana kusafisha uozooo sehemu tele wizara ya mambo ndani!!!!magereza nako hakufaiii.....polisi nao wanaliaa JK anazunguka nafikiri anajuta kuongeza term ya pili.....mambo hayaendiiii
   
 9. b

  ba mdogo Member

  #9
  Dec 30, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :target: mini nimesikia kuwa kwa ushirikina ndiyo kabisaa kabobea. may be ni moja ya sababu zinazowafanya wakubwa wasimguse. JK ana kazi kubwa. huyo kijana aliyejiua nakmbuka kuwahi kumkuta katika moja ya ofisi mkoani shinyanga na kwamba hata kuhama kwake kuliwasononesha wengi. Nawapa pole wana familia. ila akina mgoja mbona ni wengi na hasa katika vyombo vya ulinzi na usalalama?
   
 10. W

  Watchman Member

  #10
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa ndg yangu umeanza kutubore,maana inaonesha mna personal conflict na boss wako,sasa hizo issue zenu kutuletea kwenye hii BLOG cc hazituhusu,wewe zungumza issue za kijamii zinazotugusa watu wote bila ya kujali ni kutoka katika Org hipi.
   
 11. M

  Mwipulika Member

  #11
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakin mimi ninapata was was na hawa maafisa uhamiaji,kwa sababu hata ukisoma huo waraka uliotumwa kwenye blog hii,inaonekana kuna vituo vina neema na vingine havina neema. Sasa does this mean kwamba maafisa uhamiaj wananeemeka kwa rushwa? Maanake vituo vilivyotajwa kwamba ni vya neema, vyote ni vya either mipakan au sehem wanazoingia na ku toka
  kwa wingi kama airport
   
 12. P

  Paul S.S Verified User

  #12
  Jan 3, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu kuwa mkuu wa mkoa wa dsm si sawa kuwa na mkuu wa mkoa wa lindi.
  kuwa polisi wa malindo si sawa na trafiki.
  kuwa waziri wa jinsia si sawa na wa fedha.
  Nadhani umenisoma
   
 13. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2011
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,215
  Likes Received: 2,077
  Trophy Points: 280

  Ndugu, punguza jazba. JF si blog, ni forum, hapa kila mtu analonga kwa uhuru
   
 14. s

  siyenda Member

  #14
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  LO!mmenikuna vilivyo na hii mada kuhusu uhamiaji.Pia kuna maafisa ninaowafahamu huku Kigoma wamekaa kituo kimoja miaka 7 mpaka 13 bila kuhamishwa,ikiwa wengine hufika na kuhamishwa hata baada ya mwaka mmoja.na wengine hata wakipata uhamisho wa ndani ya mkoa mlipo yao ya uhamisho huchukua mwaka au wasilipwe kabisa.night ndio hakuna kabisa hata usafiri kikazi unabaki kutumia fedha yako huku wakidai watarejesha lkn pesa hiyo wala hairejeshwi.
   
 15. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Tatizo la idara ya Uhamiaji ni kama ifuatavyo:-

  • Mfumo wa idara ya Uhamiaji ni wa kibabaishaji sana, kuanzia uongozi hadi wakati mwingine wafanyakazi! Hebu fikiria idara inakuwa na Deputy Commissioner of Immagration (DCI) zaidi ya 100 inatia mashaka kabisa. Chukulia jeshi la polisi kuna DCP wasiozidi 10 hali kadhalika Magereza ina DCP wasiozidi 5 lakini wao wamezidi 100 na hivi vyeo vinaendana na idadi ya watumishi. Kimsingi Magereza wamewazidi Uhamiaji, Magereza nao wamezidiwa na Polisi hali kadhalika Polisi nao wamezidiwa na TPDF. Huu ndiyo pyramid ya uongozi, sasa kama wao wapo wachache kisha maDCI wanazidi 100 ni ubabaishaji kabisa. Kosa kubwa ni serikali kutoitupia macho hii idara ambayo saizi watu ndiyo wanaamka na kutaka kujua utendaji wake kiundani baada ya matukio kadhaa yaliowaweka wazi zaidi.
  • Idara hii ndiyo imeanza kukua hivyi inashindwa kuendana na mabadiliko haya hususani viongozi ambao wanafanya mambo yao mengi kwa mazoea sana. Hivi karibuni walifanya mabadiliko katika vyeo vyao lakini hii siyo tatizo sana tatizo ni utendaji wake umejaa rushwa sana. Uhamisho mtu anaweza kuuzima kirahisi tu kwa sababu ya rushwa tena rushwa uchwara.
  • Mwisho ni serikali kutoiangalia idara kwa makini kwani idara ilikuwa haina chuo lakini saizi wanacho kipo Moshi, idara haina nyumba za wafanyakazi hata kama ni mbavu za mbwa lakini hazipo hivyo kulazimika kupanga bila kuwa na fedha ya pango katika mshahara. unafikiri nini kitaendelea hapo kama si kukimbizana na wahindi, wazungu, wasomali na kuchukua rushwa kisha kuidhalilisha nchi yetu kuuwa ukitaka kuishi nchi Tz utaishi bila shida hata kama siyo raia tena bila bughudha.
  • Yaani nifikiriapo Uhamiaji naona image ya ubabaishaji tu. Ayaaaaa bwana.
   
 16. czar

  czar JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tatizo sana miuteuzi m ingi mpaka Ikulu, this is not good for us at all. Katiba ibadilishwe, rais apunguziwe majukumu unaweza kuta kasahau.
   
 17. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #17
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Hivi hizi nafasi zinawafanya watu waone wataishi milele sio????Mbona hivi lakini?Haiwezekani JK asiwe msafi amteue mtu msafi wala asafishe uozo uliopo,tufanyeje?Labda kweli tuende kwenye maombi Ufufuo na Uzima.
   
 18. M

  Mwipulika Member

  #18
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nionavyo mimi mkuu,maafisa uhamiaji wameshakua na mazoea ya kuneemeka kwa rushwa ndio maana hawana muda wa ku deal na wahamiaj haramu ambao ni choka mbaya. Namaanisha wakimkamata mtu ambae ni mhamiaj haramu na hana hela ya maana,bas watamfungulia mashtaka,ila kama ana hela watapokea rushwa kisha wanamuachia
   
 19. M

  Mwipulika Member

  #19
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lakin mkuu..sawa hii ni sehem ya mtu ku express freely mawazo yake,ila kuna maneno mengine hayafai kuyaweka hadharan,jarib kupunguza ukali wa maneno..ingelikua wewe ndio huyo mgonja na umeandikwa hivyo,ungejiskiaje?..au ndio unajiona kua wewe ndio Mr. freedom of expression?
   
 20. M

  Mwipulika Member

  #20
  Jan 16, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Narudia tena..nimemind sana jins ulivyoporomosha matus,wee unadirik kumuandika mtu hadharan eti yeye ni bwabwa!..et kwa kua hana mke..acha hizo,hiyo ni life style yake aliyojiamulia..ila kwa point zingine ulizotoa,nazikubali japo sina uhakika nazo..acha jazba
   
Loading...