Elections 2015 Uhamiaji kuchunguza uraia wa Zitto

Habari zilizoripotiwa kwenye vyombo vya habari juu ya Idara ya Uhamiaji kuanza kuchunguza Uraia wa ndugu Zitto Kabwe zinapaswa kuhojiwa kwa kuwa zinazua maswali mengi ya kuudhi

Ni kitu gani hasa kilichoisukuma idara hiyo leo kuanza kufuatilia Uraia wa Zitto?

Turejee historia kwa ufupi:

Mwaka 2010 Mgombea wa Upinzani jimbo la Nyamagana Ezekiel Wenje alitangazwa kuwa si Raia.

Mwaka huo huot Mgombea wa CCM jimbo la Nzega Hussein Bashe aliyekua kinyume na kambi ya mwenyekiti taifa ambae ni Rais alitangazwa si Raia wa Tanzania

-Baada ya Rais Mkapa kuingia madarakani,alipokosolewa vikali Mwanasiasa na mwanaharakati nguli Jenerali Ulimwengu alitangazwa kuwa si Raia

Je,Hili la ndugu Zitto halina unasaba na siasa za majitaka?

Ni nani mwenyehatimiliki ya nchi kiasi kwamba anaweza kuitumia idara nyeti ya umma kuchokonoa,kutishia haki ya msingi ya mtu kwa sababu za kisiasa?

Zitto amekua Mbunge kwa zaidi ya miaka 10 na Amekua Mwenyekiti wa PAC na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambazo ni nafasi nyeti.

Je,Uhamiaji wanataka kutangaza kuwa Idara ya Usalama wa Taifa hawafanyi kazi yao ipasavyo hadi kumuachia mtu ambae hajulikani alipotoka kuwa na access ya nyaraka nyeti za nchi baada ya kuongoza taasisi muhimu?

Niliwahi kuandika kuwa ukitaka kuthibitisha kama wewe ni raia wa nchi hii basi ikosoe serikali ya Tanzania,gombea ubunge au urais halafu uwabane vilivyo watawala.Kama umezaliwa maeneo ya mipakani au kama rangi yako ya ngozi ni ya asili ya nje ya mipaka yetu utakiona

Hii tabia haipaswi kufumbiwa macho hata kidogo. Ni lazima Idara ya Uhamiaji ieleze msingi wa uchunguzi huo unatokana na nini. Tabia ya kuviziana na kutumia dola ikiachwa iendelee hakuna atakaebaki salama

Cha ajabu watu wenye rekodi ya kupambana na ufisadi na kuonyesha uzalendo kwa nchi ndio wanaokua wa kwanza kutiliwa mashaka juu ya Uraia wao.Inachekesha sana


Kama tunafika Mahali Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania anamuomba Mkongomani orodha ya walioficha fedha za Tanzania nchini Uswisi basi Mkongomani huyo uzalendo wake ni zaidi ya ule wa viongozi wakuu wa vyombo vya Dola na hata Rais wa nchi.

Usishangae kukuta kuwa suala hili linaibuka kumnusuru Mgombea wa CCM huko Kigoma mjini.Yaani ili kuzua hisia hasi dhidi yake kutoka kwa wapiga kura tu.

Maslahi ya kisiasa yametamalaki kama yalivyotamalaki katikat mradi wa unyanyasaji aliofanyiwa Jenerali Ulimwengu,Hussein Bashe na Ezekiah Wenje mwaka 2010 na hapo kabla

By the way, Katika Kitabu kilichopigwa marufuku cha "The Dark Side of Julius Nyerere " cha Ludovick Mwijage kulikua na tuhuma ambazo hazikuwahi kujibiwa kuhusu uraia wa Mwalimu Nyerere.Au jibu la Serikali ndio kukifungia kitabu kile?

Mch.Christopher Mtikila aliwahi kuibua tuhuma kuhusu Uraia wa Rais Mkapa kuwa sio Mtanzania .Hazijawahi kujibiwa kiufasaha

Ipo siku wanamuziki Alli Kiba,Mwasiti na Wengineo kutoka Kigoma au Mipakani watakapotumia nyimbo zao kuelimisha jamii na kugusa maslahi ya watawala wataanza kuonekana kuwa sio watanzania. Tusikubaliane na ujinga huu

Tuhoji ,Tukosoe na kulaani jaribio lolote la kutumia idara nyeti za nchi kutisha sauti kinzani dhidi ya watawala au watu wachache kwa maslahi yao binafsi.

Tanzania ni yetu sote,Hakuna mwenyehatimiliki ya nchi hii

Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Afrika...

Aluta Contimua,Victory Ascerta....

Ben Saanane
 
Na ccm wanamgombea ana uraia wa Marekani..lakini uhamiaji 'hawajui' na 'hawataki kujua'
 
Akizungumza kwenye moja ya mikutano ya kampeni Kigoma, mgombea urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho Anna Mghwira amesema, anawashangaa Uhamiaji leo kuanza kuchunguza uraia wa Zitto wakati ameshawahi kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Habari zaidi soma gazeti la Majira la leo.
Mbona Jenerali ulimwengu alichunguzwa akakutwa sio raia na alikuwa ameisha kuwa mbunge, mkuu wa wilaya etc? Hata huyu achunguzwe, usijekuta ni mhutu huyu
 
kwa hiyo na Dr.Ben mkapa ni wa msumbiji kwa kuwa kwao masasi karibu na msumbij? aaaah siyo kweli ni utaratibu tuu wa kazi.
 
Nakumbuka maneno ya Wassira ..... CCM walijua uzi mgumu unaowaunganisha Mbowe na Slaa ukatikie wapi na muda gani ...... CCM wametuweza kweli ..... kazi ipo kupanga upya upinzani ..... leo mameneja wengine wa kampeni za upinzani hata kadi hawana na tumewaamini kabisa ......ngoja tupishe hii mihemuko uchaguzi upite ndio akili zitawarudia ....

Waombe Mungu Lowasa apite, akipigwa chini duuuh....
 
Mbona Kinana ni msomali na hatujawahi kusikia idara ya uhamiaji kuhoji uraia wake,ni nani mtanzania halisi athibitishe kama hutokuta mgogo wa Sukamahela peke yake ndo mtanzania halisi
 
Baaada ya jana kuisimamisha Dar leo mafuriko yanaingia mji kasoro bahari na saa hii yuko Ruaha.
Lowassa ni noma, anadokoa huku anaacha, anaenda huku anashindilia anaacha, anaamia sehemu nyingine anakandamiza! ccm wanatamani muda wa kampeni uishe
 
Asante mkuu Ben Nilikuwa najiuliza haya yamekujaje? Kumbe ni habari ya Jimbo la Kigoma mjini manake nasikia hilo JIMBO wt waliopitishwa wananguvu sasa CCM wanahisi Zitto anaweza kuwa naushawishi zaidi akalichukua asee CCM wataleta VITA kwenye Nchi hii Kwakweli niupuuzi majitu yametawala miaka mingi lkn bado inadhani inahatimiliki ya kuongoza milele.....nawachukia sana hawa wagu
 
Last edited by a moderator:
Interesting......Slaa anaibomoa CHADEMA Zitto anachunguzwa uraia....
CCM wanaendelea na kampeni....Lipumba ka quit....

Whoever is behind all this ni 'genius' wa mikakati...

sawasawa! em fikiria alichosema slaa kua ilikua ikijulikana tangu zamani hata kabla ya dr slaa kujotoa katika siasa kwamba Lowasa angekuja chadema na watu wake na wote waliafikiana, sasa naona kumbe dah... cc tunaona kachukua maamuz magum, eti Lowasa wamemkata kweny cham chake mara cjui hajarudisha kadi ya chama cha mapinduzi. YOTE HII NI MIPANGO, VIONGOZI MTALIPWA CKU YA MWISHO, WANANCHI WANAUWANA KISA USHABIKI WA VYAMA..

HAKUNA CHA UKAWA, CCM WALA ACT. WOTE NI WALE WALE... NACHUKIA SIASA YA TZ, ISHAALLAH MOLA ATAWALIPA
 
kazaliwa tanzania.zito kazali wa tanzania. tueleze taratibu za kuwa raia hapa tz...
Kuzaliwa Tanzania sio guarantee ya kuwa raia kama wazazi wako wahamiaji na hawakuomba uraia wa Tanzania. ...tumechoka kuwa na viongozi wahamiaji toka yule mwenye kifimbo cha kuchezea
 
Nchi hii ina kingmaker na sijui lini tutamjua.
Wee acha tu....
Sasa waSwaha (TZds) wanagongana na kukashifiana kati yao " WHO is WHO" ndani ya nchi hii..... Acha sasa SULTANI arudi kuchukuwa klichobaki !!!!
Wandaguu hebu simameni imara tujenge TAIFA !! acheni umbeya !!
 
Kuna kiongozi mkubwa wa jeshi la Tanzania alitorokea Rwanda baada ya kugundulika si raia. Kutenda kosa kwa muda mrefu bila kugundulika hakuhalalishi kosa.

Hakuwahi kutoroka yule...suala la kutoroka lilitengenezwa tu, ukweli ni kuwa kaburi lake halijulikani lilipo.
 
sawasawa! em fikiria alichosema slaa kua ilikua ikijulikana tangu zamani hata kabla ya dr slaa kujotoa katika siasa kwamba Lowasa angekuja chadema na watu wake na wote waliafikiana, sasa naona kumbe dah... cc tunaona kachukua maamuz magum, eti Lowasa wamemkata kweny cham chake mara cjui hajarudisha kadi ya chama cha mapinduzi. YOTE HII NI MIPANGO, VIONGOZI MTALIPWA CKU YA MWISHO, WANANCHI WANAUWANA KISA USHABIKI WA VYAMA..

HAKUNA CHA UKAWA, CCM WALA ACT. WOTE NI WALE WALE... NACHUKIA SIASA YA TZ, ISHAALLAH MOLA ATAWALIPA

Ndio maana la muhimu sana ni lawasa kutoa ahadi ya lini atatupatia katiba mpya. Ahadi zingine zote hazina maana kama ukawa hawataleta katiba mpya.
 
Back
Top Bottom