Uhamiaji Kigoma walalamikiwa kuwabambikizia kesi za uraia wananchi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
uhamiaji%20kigoma.jpg

Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma ujiji mkoani Kigoma wamelalamikia vitendo vya baadhi ya maafisa wa idara ya uhamiaji mkoani Kigoma kufanya vitendo vya uonevu kwa kuwakamata na kuwabambikia makosa ya uraia wananchi ambao ni raia halali wa Tanzania huku wakiwaacha watu wasio raia ambao wamekuwa wakiishi bila kuzingatia sheria.

Madiwani hao wamesema maafisa wa idara ya uhamiaji wamekuwa wakiwakamata watanzania na kuwalundika pamoja bila kuzingatia misingi ya utu pamoja na kuwashusha abiria kwenye mabasi bila kutenda haki licha ya kuwa raia, huku wakiwaacha wahamiaji ambao wanaishi na kufanya shughuli zisizo halali katika maeneo ya kumbi za starehe na maeneo mengine ya kibiashara.

Akitoa ufafanuzi kuhusu sintofahamu hiyo Afisa kutoka idara ya uhamiaji mkoa wa Kigoma, Dominic Kibuga, amesema idara hiyo imekuwa ikipokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi kuhusu kusumbuliwa na maafisa wa idara hiyo, na kwamba hatua zimekuwa zikichukuliwa pamoja na kuhakikisha hakuna usumbufu unaojitokeza katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya usafiri.
 
Serikali kali dhwalimu hubambikiza kesi, hufadhili wizi, hulinda wezi, kupoteza watu (Ole type) ,nk.

Mama hataki kurithi hayo tokea #5.

Kudos mama Samia kwa kuukemea hadharani udwalimu.
 
Kuoneana tu mtu mweusi kwake ni africa tu, iwe kigoma, burundi, mwanza kenya uganda senegal nigeria, Ethiopia na kwingineko maadamu ni africa basi ni raia tu coz africa ni moja tu, sasa ulaya tufukuzwe na africa pia
 
Back
Top Bottom