Elvis Legacy
JF-Expert Member
- Aug 10, 2017
- 3,379
- 4,703
Siku hizi mfumo wa uhamiaji umerahisisha upatikanaji wa passport. Unafanya application on-line.
Document za muhimu ni;
1.Kitambulisho cha NIDA au namba na online copy.
2.Cheti chako cha kuzaliwa.
3.Taarifa za wazazi (Baba na Mama)
3.Cheti cha kuzaliwa Mama (Au kiapo)
4.Barua ya utambulisho serikali ya mtaa au mtendaji kata.
5. Picha moja ya passport size photo (soft copy)
Hakikisha una-scan vyote hivyo.
Una-apply online. Mfumo ni rahisi na rafiki sana. Ukifanikisha utalipia Tsh.20,000.
Kisha uta-download fomu yenye taarifa zote baada ya kulipia.
Kuna sehemu ya wadhamini wawili, utatafuta wakujazie. Kuna sehemu ya mwanasheria na muhuri. Utatafuta akusainie. Au nenda pale ofisini zao wapo, watakusaidia.
Kisha ambatanisha na hard copy ya vielelezo vyote hapo juu isipokuwa picha ya passport size photo.
NB: Kama kuna ushahidi wa safari kama mwaliko, barua au ticket ambatanisha pia. Kama ni kwa ajili ya biashara ambatanisha TIN number na leseni ya biashara. Hapa inategemea na maombi yako ya passport.
Ukifika ofisi za uhamiaji (HQ), Utakutana na maafisa uhamiaji watajiridhisha na taarifa zako. Wanaweza kukuuliza maswali kadhaa kijiridhisha. Viambatanisho zaidi vitahitajika kama maelezo yako hayajitoshelezi au kama fomu yako ina taarifa hazipo sawa.
Kama kila kitu kipo sawa. Utapewa control number, kisha utalipia 130,000.
Baada ya ku-approve malipo. Utaenda kitengo cha kupiga picha na kusaini kwa alama za vidole. Kisha utapewa tarehe ya kufata passport yako wizara ya mambo ya ndani.
Passport inapatikana ndani ya wiki mbili kama taratibu zote hapo juu umekamilisha.
Vinginevyo utabaki unalaumu tu kuwa kuna ubabaishaji, wakati wewe mwenyewe ndio tatizo.
Sent using Jamii Forums mobile app