Uhamiaji Badilikeni: Acheni kufanya kazi kwa mazoea

Jamii forum ni sehemu muhimu ya kutolea kero za kijamii ambazo huwa zimeshindikana, huko uhamiaji huwezi kusikilizwa hata ulalamike vipi ndiyo maana mleta mada akaamua kuja JF akiamini hata viongozi wa Uhamiaji watapita humu na kuona malalamiko yote kisha kuyafanyia kazi.
Sawa kabisa kwenye mkutano wa kujadili tatizo la malaria, huwezi kumualika mbu naye kuwa mjumbe
 
Niamini sifanyi kazi Uhamiaji wala Serikalini Mimi ni mpambanaji ila nimewakubali sana, tatizo lipo kwetu sisi hatujipangi na tumeshazoea short cut amini ndugu.
Wewe utakuwa ni mfanyakazi au Mtumishi wa uhamiaji umeamua kuwatetea kijanja lakini utambue kuwa unalea Ugonjwa mbaya wa kuendeleza usumbufu usio na Tija unaolikosesha Taifa mapato

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale jamaa huwa wanashirikiana na vishoka wao kwenye stationeries kadhaa mitaa hii ya uhamiaji na kota za bandari
 
Yani mi mwenyewe nimesoma maelezo yake nimeshangaa, yani yeye watu kusumbuliwa ndio anaona ni namna ya kudhibitisha uraia, sasa hao NiDA wanatoa national IDs za nini kama wanashndwa kudhibitisha uraia wa MTU, tayari ushasema kupata passport uwe na kitambulisho cha taifa, tayari ninacho, unataka kudhibitisha nini tena? Jamaa umemjibu vizuri , hawa ndio wale wanaopenda kusumbua watanzania wenzao kisa wamekalia ofisi za umma.
Nyinyi ndo mnakaa nyuma ya viti na kusumbua watz wenzenu kwa kisingizio cha kukwepa kusajili wakimbizi

yaani wewe umesomea mambo ya uhamiaji halafu huwezi kubaini nani raia na nani ni haramu hadi usumbue kila anayekuja mbele yako!?

duuh maajabu hayataisha tz hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi sioni kama uhamiaji kuna tatizo ila naamini sisi ndio tuna matatizo, kama kweli wewe ni Mtanzania na una vigezo kwanini usiwe na documents ambazo zitadhibisha na kuona kweli unastahili kupata Passport!!?

Nilienda uhamiaji mida ya saa Saba mchana nimejipanga haswaa hasa katika swala la documents, yule Brother alie nishughulikia alisema unastahili na huna sababu ya kuto kupewa Passport.

Nikapewa tarehe kweli nikaenda kuchukua wizara ya mambo ya ndani, yani faster tu hata Wife alinishangaa akasema eti Mimi kijukuu cha Mtume ila ukweli nilijipanga kwa vigezo na sikutoa hata rushwa mia.

Serikali naipongeza kwa hatua zake maana hapa Bongo kambi za wakimbizi ni nyingi na asilimia kubwa wakimbizi wana ongea kiswahili kizuri.. Binafsi nawapongeza sana Uhamiaji na nampongeza JPM kwa hatua za kumpa heshima Mtanzania na Passport mpya.

Wengi wenu mlipata Passport za zamani kimaghumashi mkubali mkatae, kwa taratibu za sasa lazima mrudishwe kwasababu mlizoea kutoa rushwa Passport zinawafata majumbani sasa hivi ngumu.

Asante Mh Rais na Uhamiaji kwa kuleta heshima ya Mtanzania tutaelewana tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi nikuulize wewe kanyela mumo, assuming you have that brain to reason things out, hivi kitambulisho cha NIDA ni cha nini ? Navyojua mimi mtu yeyote mwenyewe kile kitambulisho amethibitishwa bila shaka ni mtanzania 100%, ndio maana ikaundwa NIDA ili kudhibisha hilo, sio uhamiaji, uhamiaji wanataka niwe na National ID tayari ninayo, wanataka nini tena? Mbona unakuwa na ubongo wa size ya walnut? Huo usumbufu ni wa "KISHAMBA" na kutaka rushwa kwa nguvu.
 
Uhamiaji wanahitaji Elimu kubwa watumishi wao wengi bado hawajui wajibu wao usumbufu kwa waomba passport umezidi sana, ni mara mia wangetangaza utaratibu mpya kwa wale wenye passport za zamani wasiwe wanasumbuliwa kujaza form kibao maswali mengi ya kijinga jinga, waandae mfumo bora kwao ili mtu akifika wanatumia data za awali analipia Ada anapewa passport anaondoka huku Serikali ikiingiza mapato, lakini sasa usumbufu wao unaikosesha Serikali mapato na kuishia kujinufaisha wao binafsi.
 
Yani mi mwenyewe nimesoma maelezo yake nimeshangaa, yani yeye watu kusumbuliwa ndio anaona ni namna ya kudhibitisha uraia, sasa hao NiDA wanatoa national IDs za nini kama wanashndwa kudhibitisha uraia wa MTU, tayari ushasema kupata passport uwe na kitambulisho cha taifa, tayari ninacho, unataka kudhibitisha nini tena? Jamaa umemjibu vizuri , hawa ndio wale wanaopenda kusumbua watanzania wenzao kisa wamekalia ofisi za umma.

Uhamiaji ndipo kuna maswali ya kijinga jinga kuliko idara zote kwa Tanzania hawataki hata kubadilika waende na wakati bado wamekomaa na usumbufu wa tokea miaka ilee
 
Usipadharau JF na kama unaona siyo sehemu sahihi ya kutolea kero ambayo wewe binafsi haijakutana nazo ni vyema uache wenye kero wapate kutema nyongo zao ili viongozi wa uhamiaji wapate kujirekebisha
Kuja kutema nyongo huku kabla hujafanya jitihada za kupata majawabu hukohuko naiona kama kutengeneza lawama zisizokuwepo. Pengine kuna issue mahususi alielekezwa aitekeleze, Ila yeye ili ionekane kanyanyaswa anakimbilia JF. Tungeambiwa na jitihada za kuipata/kuidai haki take ziliishia wapi angalau tungepata mwanga. JF hakupatikani pasipoti
 
Jamii forum ni sehemu muhimu ya kutolea kero za kijamii ambazo huwa zimeshindikana, huko uhamiaji huwezi kusikilizwa hata ulalamike vipi ndiyo maana mleta mada akaamua kuja JF akiamini hata viongozi wa Uhamiaji watapita humu na kuona malalamiko yote kisha kuyafanyia kazi.
Zilizoshindikana. Safi kabisa. Tatizo la mdau limeshindikana? Alijaribu vipi kulitatua pale likashindikana?!
 
Back
Top Bottom