Uhalisia wa Zuio la Bomoabomoa Dhidi ya Serikali

UHALISIA WA ZUIO LA BOMOABOMOA DHIDI YA SERIKALI

Hivi karibuni baadhi ya maeneo katika jiji la Dar es Salaam (hasa maeneo ya Kimara) kumekuwa na ubomoaji unaofanywa na serikali kupitia wakala wa barabara TANROADS dhidi ya makazi ya wananchi na kuibua manung’uniko na lawama za hapa na pale, wengine wakidai kuwa kuna kesi mahakamani na mahakama ilikwishatoa amri ya kuzuia ubomoaji huo. Kumeibuka kauli mbalimbali, wengine wakisema kuwa serikali imeingilia uhuru wa mahakama na kukiuka amri iliyotolewa na mahakama. Ifuatayo ni makala fupi kuhusiana na ni nini hasa inapaswa kutambulika kuwa amri yamahakama kuzui bomoabomoa mahali popote pale.

Wapo wanaodai kuna zuio na walioonesha karatazi zilizoandikwa Stop Order wakisema kuwa ndio amri halali ya Mahakama. Nitatoa ufafanuzi wa hivi vitu viweli, Stop Order na Amri ya Zuio.

Stop Order

Mwandishi Bryan A. Garner Katika kamusi ya misamiati ya kisheria Black’ law Dictionary, 8th edition anatoa maana ya neno Stop order:

“Order that suspends a registration statement containing false, incomplete, or misleading information…. A bank customer’s order instructing the bank not to honor one of the customers’ checks – also termed stop payment order. …An order to buy or sell when the security’s price reaches a specified level (the stop price) on the market…”

Msamiati Stop order umetajwa katika baadhi ya sheria za Tanzania. Msamiati huu unajitokeza katika sura na. 323 ya sheria za Tanzania (The Forest Act) na hauhusiani vyovyote na kesi za madai na ubomoaji kupisha miradi ya serikali. Pia msamiati Stop Order unajitokeza katika by-laws za sura ya 269 za sheria za Tanzania (The Archtects and Quantity Surveryors (Registration) Act By-Laws). Hii inajitokeza katika kanuni ya 113 na haihusiani na masuala ya bomoabomoa au amri za mahakama.

Msamiati huu pia upo katika sura ya 322 ya sheria za Tanzania (The Police Force and Auxiliary Serivices Act) katika kifungu namba 43. Zaidi msamiati huu unapatikana katika sura ya 258 ya sheria za Tanzania (The Political Parties Act) kifungu cha 11. Sura Na 394 ya sheria za Tanzania (the Insurance Act) pia ina msamiati Stop Order, katiaka kifungu na. 101.

Zaidi ya hapo msamiati huu hauonekani katika sheria zingine Tanzania ikiwemo ile inayotoa msingi wa Kuzia tendo fulani lisifanyike au kushinikiza kufanyika kwa jambo fulani (injunction) ambayo ni sura ya 33 ya sheria za Tanzania. Sheria hii ndiyo inayotoa Amri ya zuio ambayo ndio ingefaa kuzuia bomoabomoa inayolalamikiwa.

Stop Order inaweza tolewa kwa mtu binafsi au taasisi binafsi kama vile kampuni pale tu itakabodhihirika kuwa mtu huyo au taasisi hiyo haina mamlaka kisheria kufanya shugghuli pale au kuhodhi eneo lile. (The Town Director v Daniel Sekao 1988 TLR 22 (HC))

Amri ya Zuio (Temporary Injunction)

Amri ya zuio ama injuction ni zao la litokanalo na taratibu zilizoanzia uingereza, na Kesi iliyoweka misingi wa zuio hili ni kesi ya American Cyanamid Co. v Ethicon Ltd ([1975] AC 396; [1975] 1 ALL ER 504). Katika kutoa zuio hili, mahakama huangalia vigezo vitatu muhimu (baadhi ya kesi huongeza kingine na kuwa vinne). Kwa Tanzania amri hii hutolewa chini ya kifungu cha 68 na O. XXXVII ya sura ya 33 ya sheria za Tanzania (the Civil Procedure Code).

Hili ni zuio ambalo hutolewa na mahakama kuzuia upande wa pili wa wadaawa kufanya jambo au kulazimisha kufanya jambo kwa kipindi kesi ya msingi ikiendelea au hadi pale mahakama itakavyoamua vinginevyo. Amri hii ya zuio ni nusu ya hukumu na inafanya kazi kama vile hukumu ya kesi ya msingi ilishatolewa, hadi pale mahakama itakapotoa amri nyingine tofauti. Mwandishi msomi Sohoni katika kitabu chake SOHONI'S LAW OF INJUNTIONS, 2nd Edition ukurasa 67 anaandika:

“As such, an injunction is in its operation, somewhat like judgment and execution before trial, it is only to be resorted to from a pressing necessity, to avoid injurious consequences which cannot be repaired under any standard of compensation…. an application for an Injunction is an appeal to the Court, and the plaintiff is bound to make out a case showing a clear necessary for its exercise, it being the duty of the courts rather to protect acknowledged rights than to establish new and doubtful cases. Moreover, a temporary injunction is a restrictive or prohibitory process designed to compel the party against whom it is granted to maintain his Status merely, until the matter in dispute shall by due process of the courts be determined.”

Amri ya Zuio haitolewi na haifanyi kazi kwa mtu au taasisi isiyokuwa moja ya wadaawa katika kesi ya msingi (National Bank of Commerce v Dar es Salaam Education and Office Stationery 1995 TLR 272 (CA)).

Tofauti kati ya Stop Order na Injunction (Amri ya Zuio)

Kwa hiyo basi, Stop order na Amri ya Zuio ni vitu viwili tofauti vitokanavyo na misingi tofauti ya kisheria. Wakati stop order ni zao la sheria Huru (substantive law) Amri ya zuio ni zao la sheria za kiutaratibu (Procedural Law). Stop Order inaweza kutolewa na mtu yeyote au mamlaka yeyote lakini amri ya Zuio inatolewa na Mahakama Pekee. Wakati Stop order ina asili ya kushinikiza utii wa kanuni zilizopo kwa mujibu wa sheria, Amri ya zuio in asili ya hukumu itokayo kabla ya kesi ya msingi haijasikilizwa, huku ikizingatia usumbufu na haki kufurahia mali baina ya wadaawa. Stop order haizingatii uwiano wa manufaa (balance of convenience) lakini Amri ya Zuio siku zote huzingatia uwiano wa manufaa baina ya wadaawa. Pia Stop Order inaweza tolewa baina ya watu au taasisi zisizo na mahusiano ya kimkataba au kiutendaji, wakati Amri ya zuio hutolewa baina ya pande zilizo katika mgogoro pekee. Stop orders hutolewa pasopo taratibu za kusikilizwa katika misingi ya kesi za madai (on preponderance of evidence) wakati Amri ya zuio usikilizwaji lazima ufanyike. Vilevile Stop Order inatoa wasaa kwa mhusika kukata rufaa dhidi ya order hiyo, wakati Amri ya Zuio haitoi wasaa wa kukatiwa rufaa (Hardmore Productions Ltd. and Others v. Hammilton And Another, [1983] 1 A.C 191, - Diplock, L.J., angalia pia Gazelle Tracker Limited v Tanzania Petroleum Development Corporation Civil Application no. 15 of 2006 (CAT, unreported)).

Hatua za kufuatwa katika Amri ya Zuio

Baada mmoja wa wadawa kuomba amri ya Zuio katika mahakama yenye mamlaka, ombi hilo husikilizwa (ikumbukwe kuwa maombi haya huwekwa mbele ya mahakama pale ambapo kesi ya msingi ilishafunguliwa). Mahakama ikishajiridisha kwa kuzingatia vigezo vinne vikuu, hutoa amri ya kuzui kutendeka kwa jambo fulani (prohibitive/restrictive injuction) au kulazimisha kufanya jambo fulani (mandatory injunction). Amri hii ikishatolewa (interim decree) hutolewa kwa mfumo wa drawn orders na wadaawa wote hupewa service ya hizi orders.

Amri za Zuio hazitakiwi kuwekwa kwenye mbao za matangazo au eneo husika ili kuzuia kitendo fulani kisifanyike. Hii si dhamira ya Amri hizi. Dhamira ya amri hizi ni kushinikiza ukaziaji wa “hukumu” iliyotolewa kabla ya uamuzi wa mwisho wa kesi ya msingi (ndio maana ya kuitwa temporary injunction). Kwa hiyo kama mmoja wa wadaawa hakuwepo siku amri hizi zinatolewa na mahakama upande ulioomba amri hizi unalazimika kumtafuta mdaawa aliyelengwa na amri hizi na kumpatia (serve).

Ukweli kuhusu kitu kinachotolewa kwa jina la Stop Order

Mahakama ina maafisa wa ngazi mbalimbali, ukianzia na makarani, mahakimu, mawakili, wasajili na majaji. Mahakama inapota amri (katika hukumu yake) hutoa kitu kinachoitwa decree (extracted decree or drawn orders). Hakimu au jaji mara nyingi hajihusishi na kuandika (extract) decree hizi. Makarani na wasajili hufanya hii kazi na hakimu au jaji ataweka saini yake baada ya kuandikwa kwa decree.

Iwapo mahakama imetoa amri yake ya zuio kutokana na sura ya 33 ya sheria za nchi (O. XXXVII) hakuna kitu kinachotakiwa kutolewa kinaitwa Stop order, hata kama chini yake itajitokeza saini ya jaji au hakimu. Watumishi wa Mahakama hasa makarani wamekuwa si wajuzi wa taratibu za kisheria kwa hiyo kwa namna moja au nyingine wanaweza kuandaa kitu kimeandikwa stop order na mamlaka husika ikaweka saini yake kwa kupitiwa. Kama kitu hiki kinajitokeza basi nyaraka hii inakuwa ni batili katika misingi ya sheria.

Baadhi ya mawakili, ama kwa kutojua au kwa kuhadaa wateja wao mamekuwa na mtindo wa kuandika vitu kama hivi pia wakinuia kutoa zuio linalotolewa na kisheria kwa mujibu wa sura ya 33 ya sheria za nchi. Kitu kama hiki ni batili pia.

Amri ya zuio na inayotumika kuzuia mtu, taasisi au serikali ni ile ambayo msingi wake unaanzia kwenye kesi yenyewe iliyoko mahakamani. Waathirika au wadaawa walalamikaji wanaweka maombi ya zuio mbele ya mahakama kwa kutumia fomu maalumu (chamber summons) na mahakama hupanga siku ya kusikiliza maombi hayo. Maombi lazima yasikilizwe na mahakama itoe uamuzi juu ya maombi hayo.

UHURU WA MAHAKAMA HAUJAINGILIWA

Kufuatana na hali hii ni wazi kuwa mahakama haijatoa Amri yoyote kuzuia bomoabomoa. Pia serikali au mamlaka yeyote ya serikali haikuvunja amri halali ya mahakama. Kwa hali hiyo basi uhuru wa mahakama umebaki imara kwa mujibu wa Ibara ya 107B ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

NINI KIFANYIKE

Elimu mahsusi itolewe kwa umma kuhusiana na uhuru wa mahakama na namna unavyokuwa. Wananchi waelimishwe ni kwa jinsi gani na misingi ipi mahakama inatoa Amri ya Zuio. Mawakili wawe wakweli kwa wateja wao na wasaidiane na serikali kutoa elimu husiaka. Maofisa wa mahakama hasa makarani wapewe elimu juu ya amri hizi, ikiwemo namna ya kuziandaa na mipaka iwekwe katika mamlaka inayotakiwa kutoa amri hizi. Pia umma ueleweshwe kubainisha order zinazotolewa na mahakama ikiwa katika muendelezo wa usikilizwaji kesi (mfano maintenance of status quo) na amri za stop/stay of execution.

Kilichotolewa katika bomoa bomia ya Kimara hadi Kiluvya ni "all parties to maintain status quo pendind determination of main suit", Kwa Kiswahili mahakama iliagiza kuwa hali ilivyo siku ya kutolewa hilo zuio ibaki hivyo hivyo kati ya walalamikaji (wananchi) Na walalamikiwa (serikali kwa maana ya mwanasheria mkuu anayeiwakilisha wizara ya ujenzi Na Tanroads) hadi pale mahakama itakapotoa maamuzi yake kuhusiana Na shauri lililo mbele yake. Ikumbukwe kuwa shauri lililo mbele ya mahakama ni wananchi kupunga kubomolewa kwa Nyumba zao Na kuporwa Ardhi yao.

Kilichotokea ni serikali (Tanroads) kuendelea Na ubomoaji wa nyumba zs walalamikaji hata baada ya mahakama kutoa amri ya "Status Quo".Walalamikaji walijitahidi kuwaonyesha Tanroads nyaraka za amri ya Status Quo iliyotolewa na mahakama, Tanroads kwa jeuri wakawa pia wanawatolea nakala zao za amri husika na jeuri na kiburi kuwajibu wana maagizo kutoka juu kuwa zoezi la ubomoaji liendelee tuu. Kitendo cha Tanroads kuws nakala ya amri husika ni ushahidi kuwa walalamikaji waliwaserve Tanroads amri ya mahakama ya zuio.

Je kwa maini yako matendo haya ya serikali (executive) sio uvunjwaji wa Katiba ya nchi kifungu 107 b kama ulivyoainisha?
 
As long as Mahakama imesema "Usibomoe" mpaka kesi ya msingi itakapoisha maana yake serikali anatakiwa iache hiyo activity mpaka kesi ya msingi itakapokwisha.

Wakili wa Serikali alijua maana yake nini kusema "Usibomoe" sasa wewe unayesme Serikali INA haki ya kubomoa wakati Mahakama imetoa order rasmi Usibomoe,basi huko serikalini Hamna wanasheria na kama mbao ni Makanjanja wa Sheria.

Serikali Haina cha kujitetea hapo,alisikia Rais alisema endeleeni kubomoa msisikilize MTU yeyote,inaonyesha Rais yupo juu ya Sheria na since Mahakama haina Kiongozi Rasmi Haina nguvu.

In short hatuna Mahakama tuna mfano wa majengo ya Mahakama. Hatuna Mahakimu tunamfano wa watu wanaovaa magwanda ya Mahakama,lakini Mahakimu hakuna kama wapi basi wawili au watatu
 
Kilichotolewa Kimara had I Kiluvya ni "all parties to maintain status quo pendind determination of main suit", Kwa Kiswahili hali ilivyo siku ya kutolewa hilo zuio ibaki hivyo hivyo kati ya walalamikaji (wananchi) Na walalamikiwa (serikali kwa maana ya mwanasheria mkuu anayeiwakilisha wizara ya ujenzi Na Tanroads) had I pale mahakama itakapotoa maamuzi take kuhusiana Na shauri lililo mbele yake.

Na shauri lililo mbele ya mahakama ni serikali kutaka kubomoa Nyumba za walalamikaji
.
Kilichotokea ni serikali (Tanroads) kuendelea Na ubomoaji wa nyumba xa walalamikaji hata baada ya mahakama kutoa amri ya "Status Quo". Walalamikaji walijitahidi kuwaonyesha Tanroads nyaraka za amri ya mahakama, Tanroads kwa jeuri wakawa pia wanawatolea nakala zao za amri husika na jeuri na kiburi kukujibu wana maagizo kutoka juu kuwa zoezi la ubomoaji liendelee tuu. Je matendo haya ya serikali (executive) sio uvunjwaji wa Katiba ya nchi kifungu 107 b kama ulivyoainisha?

Siyo hiyo tu hata Rais akiwa Ikulu alisikika alisema wasiogope wala kusikiliza MTU yeyote wabomoe na hajaona kama wamebomoa.

Amri toka.juu ndiyo hiyo ya Rais. Na amefanya hivyo sababu maeneo hayo wapinzani ndiyo wengi.Kuwaumiza au kuwakomoa wapinzani ndiyo maana makada wa CCM hawaoni ubaya wake.
 
Wewe ni mwanasheria wa serikali!!???
Maana huko ndio kunamabashite wa sheria
 
huna hoja

Napenda nikupongoze bila kujikita moja kwa moja kwenye content ya bandiko lako namba moja, kwa kuleta ufafanuzi wa stop order na zuio la mahakama. Wangalau leo nimekubali ulichotolea ufafanuzi wa hayo mambo mawili kwa kina, hivyo hapo wangalau wenye uelewa mpana hasa wa sheria ndio wanaweza kukupinga kwani panahitaji majibazano ya hoja kisheria zaidi. Nakupongeza kwa ufafanuzi huu.
 
Ndugu kwenye andiko hilo kuna neno dikteta? Ok, mimi ni mnufaika wa serikali, je, inabadili ukweli uliopo?
Wabongo ndio maana ujinga haututoki, mwenzenu ameleta hoja ameziainisha vizuri, badala ya kujibu kipengele kwa kipengele mijitu inaishia kutoa povu na kuleta siasa bila kuja na majibu kwa mtoa hoja. Yale yale ya tunaibiwa mchanga wa dhahabu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna jipya na pengine hatujafikia maamuzi magumu ya watawala wa awamu zilizopita, mathalani katika kushughulikia wala rushwa na watumizi vibaya wa madaraka 1995 Mkapa kupitia mahakama alimfunga jela kigogo aliyekuwa waziri wa ujenzi bwana Nalaila Kiula, awamu ya nne Kikwete aliwafunga jela vigogo Mramba na Mgonja. Awamu hii bado sana hatujaona Kigogo akitupwa jela kwa hiyo hakuna jipya kihivyo katika kushughulikia walaghai katika nchi hii.
 
Kilichotolewa katika bomoa bomia ya Kimara hadi Kiluvya ni "all parties to maintain status quo pendind determination of main suit", Kwa Kiswahili mahakama iliagiza kuwa hali ilivyo siku ya kutolewa hilo zuio ibaki hivyo hivyo kati ya walalamikaji (wananchi) Na walalamikiwa (serikali kwa maana ya mwanasheria mkuu anayeiwakilisha wizara ya ujenzi Na Tanroads) hadi pale mahakama itakapotoa maamuzi yake kuhusiana Na shauri lililo mbele yake. Ikumbukwe kuwa shauri lililo mbele ya mahakama ni wananchi kupunga kubomolewa kwa Nyumba zao Na kuporwa Ardhi yao.

Kilichotokea ni serikali (Tanroads) kuendelea Na ubomoaji wa nyumba zs walalamikaji hata baada ya mahakama kutoa amri ya "Status Quo".Walalamikaji walijitahidi kuwaonyesha Tanroads nyaraka za amri ya Status Quo iliyotolewa na mahakama, Tanroads kwa jeuri wakawa pia wanawatolea nakala zao za amri husika na jeuri na kiburi kuwajibu wana maagizo kutoka juu kuwa zoezi la ubomoaji liendelee tuu. Kitendo cha Tanroads kuws nakala ya amri husika ni ushahidi kuwa walalamikaji waliwaserve Tanroads amri ya mahakama ya zuio.

Je kwa maini yako matendo haya ya serikali (executive) sio uvunjwaji wa Katiba ya nchi kifungu 107 b kama ulivyoainisha?
Mkuu, bila shaka hili suala la status quo nimeliweka mwishoni kabisa mwa bandiko. kwa maelezo mengine status quo sio order ya kuzuia bomoabomoa wakati kuna application husika iliyo mbele ya mahakama.
 
Je Humanitarian ground haipo kwenye bomoabomoa hiyo ?
Humanitarian ground huwepo pale ambapo misingi ya sheria haikufuatwa. Sheria haina kitu kuoneana aibu kama sheria yenyewe haitoi mwongozo wa kuona aibu.
Humanitarian reason zinakuweko kama mahakama iatijiridhisha (on balance of convenience) na kutoa amri ya zuio. Mahakama huangalia vigezo mbalimbali ikiwemo sababau za kuitu katika kutaoa amri ya zuio.
 
Umeandika mavi kabisa wewe mbumbumbu wa sheria. Hukumu ya mahakama ipo halafu wewe kenge unaleta kitita cha notes kuelezea stop order badala ya kurejea hukumu ya mahakama kuhusu uhalali wa zile nyumba. Wewe kama Una degree ya sheria basi Ni degree ya chupi

Kwanza pole. "Nemo dat quod non habet " kumbe mavi ndo wewe tena Original. Mheshimiwa katuelimisha hakuna mahali alipohukumu. So kwa lugha yako mwenyewe let us serve you "kabla hujatawaza na kuflash kinyesi chako usije Jf
 
Mkuu, bila shaka hili suala la status quo nimeliweka mwishoni kabisa mwa bandiko. kwa maelezo mengine status quo sio order ya kuzuia bomoabomoa wakati kuna application husika iliyo mbele ya mahakama.
Kimsingi hauko sahihi. Lengo lako ni ovu kupotosha umma ili kuitetea serikali. Ndio maana umekwepa kufafanua mini maana ya "Status Quo" kkatika mazingira ya hoja iliyopo mbele yetu ya serikali kuendelea kubomoa nyumba za wananchu licha ya mahakama kutoa amri ya zuio ulivyofanya kwa neno Stop Order Amri ya zuio
 
Asante kwa kuleta tofauti ya kisheria katika hizo terms mbili. Hakika nimekuelewa mkuu vilaza ndio watakaokuja ku diss maana hawataelewa kitu!

Sie pia tuna case kama hio ya kimara...tulienda mahakamani tukiwakilishwa na uncle wangu ni lawyer nguli akaenda kutuwekea court injuction dhidi ya bomoa bomoa ya makusudi kupisha ujenzi wa barabara ya highway. Hawakuvunja na mradi ukasimama maana hela ilitakiwa itoke world bank utekelezaji uanze pesa haikutoka, huwa hawafadhili kama eneo lina kesi inayoendelea.

Ishu ilikuwa kulingana na allocations za ramani ya mipango miji barabara ya highway ilitengewa sehemu yake maalum ambapo panajulikana na pako wazi. Haikutakiwa ku meander mtaani tena katikati ya nyumba za watu kama Engineer uchwara alivyotaka kufosi ili avunje apige hela za fidia.

Tofauti ya mtaa wetu na kimara ni kuwa kuna wazee wasomi wengi tu na wanaijua sheria sio rahisi kuburuzwa kizembe. Hata huyo anaejiita toka juu akija lazma ale za uso kisutu!
 
Back
Top Bottom