UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UHALISIA: Kilichomtokea Dr. Ulimboka mwanzo-mwisho...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbaga Michael, Jul 1, 2012.

 1. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #1
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,914
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  "NI saa 12:45 asubuhi, bado kiza kimetanda katika eneo hili la Msitu wa Mabwepande. Mbele yangu namwona mtu akiwa amekaa chini, pembeni ya barabara akiwa amelowa damu mwili mzima.

  "Ninapomkaribia nasikia sauti ya mtu huyo ikisema kwa taabu; naomba msaada jamani… naomba msaada jamani", hivi ndivyo anavyoanza kusimulia Juma Mgaza Abdallah, mtu wa kwanza kumwona Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka baada ya kutekwa, kupigwa na kutupwa katika Msitu wa Mabwepande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

  Abdallah, anasema mara baada kumwona daktari huyo akiwa katika hali hiyo, alijaribu kumkokota kumtoa eneo hilo, lakini alishindwa kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo.

  Baada ya hapo, aliamua kusubiri mtu mwingine apite eneo hilo ili amwombe wasaidiane kumpeleka Kituo cha Polisi Bunju.

  Anasema muda mfupi baadaye aliona gari likija mbele yao, akalinyooshea mkono kulisimamisha. Liliposimama, akamweleza dereva hali aliyokuwa nayo Dk Ulimboka na kwamba anahitaji msaada wa haraka.

  Abdallah ambaye hadi wakati huo alikuwa hamfahamu mtu ambaye alikuwa akimsadia kuwa ni kiongozi wa madaktari kutokana na sura yake kuvimba, anasema walimwingiza katika gari hilo na kumpeleka Kituo Kidogo cha Polisi Bunju.

  Anasema, Dk Ulimboka wakati huo alikuwa akiendelea kuvuja damu katika baadhi ya majeraha yake huku akiwa hana suruali na kubaki na bukta tu, huku akizungumza kwa taabu.

  Kituo cha Polisi Bunju

  Baada ya kumfikisha kituoni hapo, walitoa maelezo namna walivyomwokota na kumsaidia kumfikisha hapo.

  Polisi baada kumhoji Dk Ulimboka, aliwatajia namba ya simu ya rafiki yake aitwaye Dk Deo. Walipompigia na kumweleza tatizo hilo, aliamua moja kwa moja kwenda Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, kutoa taarifa hizo na hatimaye kuandamana na watu kadhaa kutoka hapo akiwamo Mkurugenzi wake, Hellen-Kijo Bisimba.

  Wawasili kituoni
  Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania wa kituo hicho, Onesmo Olengurumwa, anasema waliwafika Polisi Bunju saa 3:36 asubuhi na kumkuta Dk Ulimboka akiwa amekalishwa kwenye benchi huku damu ikiwa imeganda kwenye majeraha mwilini.

  Olengurumwa anasema waliwahoji polisi waliokuwa kituoni hapo kwa nini wakae na mtu aliyeumia kiasi hicho muda mrefu bila ya kuita gari la wagonjwa kumchukua ili kuwahi kupatiwa matibabu.

  Olengurumwa anasema polisi walisema kwamba, walikuwa wanawasubiri ndugu zake wafike.

  Baada ya muda mfupi, akiwa ameingizwa kwenye gari kupelekwa hospitali, Dk Ulimboka aliomba maji ya kunywa akisema ana kiu sana, lakini alipopewa, alikunywa kidogo akashindwa.

  Anasema wakiwa njiani, alikuwa akilalamika kuwa anasikika maumivu makali huku akisisitiza kuwa tukio la kutekwa na kupigwa lilikuwa la kumuua.

  "Jamani hawa watu walitaka kuniua walikuwa wamepanga kuniua," alisikika mara kwa mara akisema Dk Ulimboka wakati anapelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupatiwa matibabu.

  Maelezo ya Dk Ulimboka
  Baada ya Dk Ulimboka kuokotwa aliweza kuzungumza na kurekodiwa muda mfupi baada ya kutolewa msituni na mazungumzo yake yalikuwa hivi;

  "Nilikamatwa na watu hao usiku wa Jumanne nikiwa maeneo ya Leaders Club, Kinondoni na daktari mwenzangu baada ya kupigiwa simu na mtu mmoja ambaye alidai kuwa anafanya kazi Ikulu.

  "Kuna jamaa mmoja anafanya kazi Ikulu, kama siku tatu mfululizo alikuwa akitaka kukutana na mimi ila nilishindwa kukutana naye kwa kuwa nilikuwa na kazi nyingi na wakati mwingine mpaka usiku," alisema Dk Ulimboka.

  Huku akizungumza kwa taabu kutokana na mdomo wake kuvimba, alisema siku hiyo mtu huyo alimpigia tena simu na kumtaka wakutane.

  "Jana (Jumanne) alinipigia simu na nikamwambia daktari mwenzangu twende tukaonane naye, wakati huo alitueleza kuwa alikuwa maeneo ya Kinondoni Stereo," alisema Ulimboka na kuongeza:

  "Tulipofika maeneo hayo tukampigia simu na akatueleza kuwa alikwisha ondoka, baadaye tukamweleza sehemu tulipo mimi pamoja na mwenzangu."

  Alisema kuwa, wakati anakutana na mtu yule maeneo ya Leaders Club, hakuwa na amani.

  "Kwa kweli siku ile nilivyoonana na mtu yule sikuwa na amani kabisa ya kukaa eneo lile," alisema Dk Ulimboka.

  Alisema kuwa wakati wakiendelea na maongezi ya kawaida, bado aliendelea kuwa na mashaka na mtu yule.

  "Katikati ya maongezi nikaona ameanza kuzungumza na simu, kila tukitaka kuagana alikuwa akizungumza na simu, sijui nini kilikuwa kinachelewesha sisi kuagana," alisema Dk Ulimboka na kuongeza:

  "Ghafla walitokea watu kama watano na kusema kuwa hawana tatizo na mtu yeyote katika eneo hilo isipokuwa mimi.

  Wakati sijakaa sawa, waliniburuza hadi barabara ya lami kwa kuwa eneo hilo lilikuwa karibu na barabara."

  Aliongeza, "Nilipowauliza wananipeleka wapi, wakaniambia kuwa mimi nasumbua sana na nitajua hukohuko, waliniingiza katika gari jeusi, lakini halikuwa na namba. Niliwauliza kosa gani nimefanya? Hawakunijibu kitu na kusema, we twende utajua hukohuko.''

  Alisema alipokuwa ndani ya gari hilo watu hao walimpiga na kwamba walipofika maeneo ya Victoria, walichukua sweta nyeusi na kumfunga usoni, jambo lililomfanya ashindwe kuona kinachoendelea ikiwa ni pamoja na alikokuwa akipelekwa.

  "Walinipiga mateke ya mbavuni, wakati mwingine walitumia vitako vya bunduki, kila nilipokuwa najaribu kuangalia ninapokwenda nilishindwa," alisimulia Dk Ulimboka.

  Alisema kuwa watu hao walimpeleka katika nyumba moja ambayo hakujua iko sehemu gani ambapo walimshusha na kuanza kumshambulia kwa mateke mfululizo kila sehemu ya mwili. Wakati huo, wote walimshinikiza awaambie nani yupo nyuma ya mgomo wa
  madaktari.

  "Tangu saa sita usiku mpaka saa 9:00 alfajiri walikuwa wananipiga tu, kuna wakati nilijaribu kukimbia wakapiga risasi juu nikasimama na sikuweza kukimbia tena," alisema Dk Ulimboka na kuongeza:

  "Nilisimama, wakaendelea kunipiga, niliwasikia wakisema ama wanichome sindano ya sumu nife au kunikanyaga na gari. Baadaye wakaanza kuning'oa meno na kucha kwa kolea huku wakinilazimisha kusema nani yupo nyuma ya mgomo wa madaktari."

  Alisema kuwa, watu hao walikuwa na bunduki kubwa ambayo hakuweza kuitambua ni aina gani.

  "Waliniambia kuwa ninajua ninachokifanya hivyo wanaweza kunichoma sindano ya sumu nife au wanikanyage na gari nife," alisimulia.

  Dk Ulimboka alisema kuwa awali hakuwa na shaka na watu hao kwa kuwa alidhani ni polisi, lakini baadaye alishindwa kuwaelewa kwani watu hao walimchanganya.

  "Sikuweza kuwatambua ila naweza kusema ni askari, walipokuwa wananipeleka niliwauliza mnanipeleka wapi na wakati huo nilikuwa sioni mbele ila ilikuwa kama maeneo ya Mwenge hivi," alisema Dk Ulimboka.

  Alisema kuwa baadaye alipoteza fahamu na hakuweza kuona chochote zaidi ya kusikia sauti za watu hao kwa mbali.

  "Nilikuwa sioni na nilipoteza fahamu nikawa nasikia tu wakinibeba, gari lilitembea muda mrefu, sikujua ni wapi tunakwenda, kumbe ndio huko Mabwepande," alisema.

  Alisema kuwa walifika maeneo ya barabara ya vumbi na baadaye wakamshusha na kumbeba hadi msituni.

  "Waliniburuza na kuniacha huko na muda wa saa kumi alfajiri ndipo nikazinduka na kuanza kujiburuza kuelekea barabarani ambako nilisaidiwa na mtu mmoja ambaye simtambui," alisema Dk Ulimboka.
   
 2. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli udhaifu wa JK ni tatizo kubwa sana. Dr Slaa alisema kuichagua ccm ni maafa, hv JK kwanini anaamini mgomo wa ma dr unasababishwa na maadui zake? Kwani usalama na majeshi wanamsaidiaje mwenyekiti wa chama cha mapinduzi?
   
 3. a

  artorius JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 758
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  At the beggining I thought this was just a conspiracy theory but now I have realised,this was really a conspiracy,the government now has a lot to explain,NO Doubt the government had its hand on dr.ulimboka
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Wao wajipange haraka wanunue XRay CT Scan machines hospitali zote Utra Sound na waboreshe hali za hospitali zetu waone kama Dr wataendelea na mgomo!kwa nini wanaboresha bungeni tu?wangepunguza matumizi bungeni na kuboresha sekta zingine
   
 5. j

  jigoku JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Walaaniwe wale wote waliomtesa ,waliopanga kumtesa na waliwatuma kumtesa huku wakidhani angelikufa kabla ya kusema neno kwa watu wakalisikia,sasa tumesikia kamtaja Msangi na taarifa zingine zimetupa kujua kumbe serikali inahusika.
  Liwalo na liwe
   
 6. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Tungependa kupata waandishi wa habari shujaa watakaoweza kuweka hizi story kwenye magazeti na kwenye redio, ili kila mwananchi ajue serikali ya Kikwete ni serikali ya aina gani. Yafaa pia taarifa kama hii ifikishwe kwenye vyama vya wanaharakati, ili wasiendelee kusema watu wasiojulikana bali waseme moja kwa moja kwamba alitekwa na kuumizwa na serikali, ieleweke moja.
   
 7. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  IKULU ina laana,imechafuka,if i was to be the next president nahisi nisingekaa pale,UDHAIFU ni hatari!
   
 8. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Hata tukijua (100%) ni serikali imefanya hivyo kuna lolote la kuifanya? nauliza tu.
   
 9. MAN OF CHANGES

  MAN OF CHANGES JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 508
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Very sad,yani Tz kwa sasa kila kitu kunaumiza na kuendelea kuvunja wananchi moyo na matumaini.viongozi wabovu wasio na utu na wenye kujipenda wenyewe ndio chanxpzo cha matatizo na sababu ya hapa tulipo sasa.TUSIFE MOYO WA TZ WENZANGU,MUNGU YUPO NASI KUTUTETEA,ZAIDI TUENDELEE KUPIGANIA HAKI ZETU BILA KUJALI YANAYOTUKUTA NA YATAKAYOTUKUTA.
  NAKUOMBEA DACTARI ULIMBOKA,MUNGU AKUPONYE.AMINA.
   
 10. R

  Ruppy karenston JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aiseee,habari ya huzuni sana mpaka nimelia!
   
 11. mkonowapaka

  mkonowapaka JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 1,483
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  so sad ndugu zangu...better mtu upigwe risasi ufe kuliko mateso hayo...serikali ya jk inahusika moja kwa moja na tukio hili...ninalaani kwa nguvu zote tukio hili la kikatili na mateso makubwa namna hiyo kwa binadamu huyu...kumtesa mtoto wa mtu aliezaliwa na baba na mama yake;akasoma kwa taabu na kisha kuwatumikia watanzania wenzako kwenye sekta nyeti kama hii ya afya hakukubaliki ata kidogo..na cc watanzania tunakaa kimya kwa tukio kama hili???wanaharakati mnasemaje au na nyie mmetishwa??...hapana.hatupaswi kukaa kimya
   
 12. d

  dada jane JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tunalo sana. Wewe subiri kidogoo!
   
 13. M

  Mundu JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hata wabunge wa upinzani naona ni wanafiki tu katika suala hili la mgomo wa madakatari...kwanini wasigome kuingia bungeni kushinikiza Serikali kutatua tatizo la mgomo wa madaktari upesi.

  Kama ni suala la maslahi hilo ni jepesi na sioni kwa nini Serikali inasuasua kulitatua... Lakini suala la maboresho, hilo ni suala la mipango...lahitaji muda kwani hata kama ni ununuzi wa vifaa ama upanuzi na uboreshaji wa majengo hauwezi kufanyika kwa muda mchache...na ni suala linalogusa maendeleo ya Sekta ya utabibu Tanzania nzima, hususani vijijini. Niliangalia documentary moja, katika kituo kimoja cha TV hapa nchini, kuna hospitali/despensari moja kijijini ambayo inategemewa na watu wengi, hususan akina mama, haina umeme, wagonjwa huitajika kwenda na mafuta ya taa ili wapatiwe huduma nyakati za usiku. Hakuna pia maji na hakuna dawa. Ni gharika kupata huduma katika dispensari ile.

  Sasa kama ni tatizo la maboresho ya miundo mbinu...sijui katika kile kikao cha muafaka na Pinda walipeana ultimatum ama vipi? Sikumbuki kama nilipata kusikia ama kusoma mahali popote kuwa walipeana muda fulani kuhakikisha masuala haya ya miundo mbinu ama yaananza kushughulikiwa , ama yawe yamefikiwa katika kiwango ambacho madaktari watakuwa wamekubaliana nacho! Na hii ni katika hospitali zote, za rufaa, za mikoa na wilaya, za kata na za vijijini.

  Hapa ndipo ninapopata taabu ya kuelewa maana ya vikao vya muafaka; vikao hivi vinapaswa viwe na 'critical path' . Kuwe na mtiririko wa matukio, kuanzia hapa tulipo hadi kule tunakotaka kwenda; na nani anahusika na katika suala lipi na anapaswa alitekeleze ndani ya muda gani.

  Vinginevyo vitakuwa kama vikao vya migahawani ambavyo mwisho wa siku watu hukung'uta miguu, na kuamka kesho yake kuwa kama ilivyokuwa jana yake! Hatua tisa mbele, na kumi nyuma!

  Na makubaliano haya yawe ya kimaandishi, na mintaarafu kwa kuwa ni masuala ya kitaifa basi nasi wananchi yapaswa tuelezwe maendeleo yake...ili tuweze kuhoji.


  Vinginevyo watu watabaki kuwa na kizungumkuti na kufikiri kuwa mgomo wa madaktari umechochewa na haja ya madaktari kudai maslahi bora pekee; kumbe nia yao ...ambayo kwa wananchi wengi iko nyuma ya pazia ni kudai maslahi na hali bora ya sekta nzima ya afya hapa Tanzania. Hatuhitaji mama Kijo Bisimba, ama mama Ananilea Nkya kufafanua haja hii nyeti na muhimu (huduma bora, vifaa bora, hali bora) siku ya kumsafirisha Dr. Ulimboka kwenda nje kwa matibabu. Mungu Ibariki Tanzania!
   
 14. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  watanzania nani katurog.. Nasema hapana tumezidisha upole what is the way forwad, TISS,ikulu na polisi intakiwa itueleze kinaganaga
   
 15. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Ukiona mwenzako ananyolewa na wewe tia maji...
  Mhandishi gani huyo wa kuandika haya TZ.
   
 16. mhalisi

  mhalisi JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,181
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  serikali ya Kikwete ni serikali ya kishetani. wako wapi wale waliosema Kikwete ni chaguo la Mungu?
  waliomtendea Dk.Ulimboka unyama huu hakika laana hiyo itawaandama maisha yao yote na vizazi vyao vyote.
   
 17. Mujumba

  Mujumba JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 854
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  this should be a good lesson to other vimbelembele....lazima mjue nchi haichezewi hovyo hovyo eboo
   
 18. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  alipata mateso makubwa,kutolewa jino bila ganzi uwi sipat picha,apone haraka
   
 19. d

  dguyana JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Halafu wakigoma kuingia ndio muanze kusema chadema inahusika sio? Serikali yako ni DHAIFU!!!!
   
 20. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,010
  Trophy Points: 280
  .
  Hivi gazeti la Kubenea litatoka lini? Nalisubiri kwa hamu kwani ndilo lenye uthubutu thabiti!!
  .
   
Loading...