Uhalifu ni profession (kada) inayolipa sana Tanzania kuliko nyingine yoyote

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
2,178
2,000
Wewe leo hii nenda kasimame mbele ya watu kama akina chenge et al.... uwaambie uhalifu haulipi. atakutizama kwa dharau sana na halafu atacheka mpaka mbavu zimuume. maana atakuona unaongea jambo la kipuuzi kabisa.
Tanzania ni moja ya nchi ambazo UHALIFU unalipa sana kuliko kazi nyingine yoyote. kama huamini angalia wale waliohusika na Kashfa ya RADA, angalia Mgodi wa KIWIRA, angalia waliokula pesa Za Richmond,angalia IPTL, nenda kwaangalie wale waliohusika na uuzaji wa meno ya tembo na twiga.... ok..unawafahamu mapapaa.....wangapi ambao jamii inafahamu kwa kina wanahusika na madawa ya kulevya lakini wala hakuna wa kuwahoji? unafahamu jinsi gani mtoto wa mheshimiwa mmoja ameibuka kuwa Bilionea ghafla baada ya baba yake kuukwaa? halafu bila haya unasimama na kusema uhalifu haulipi? haulipi kwako peke yako. acha kwa wale unaowalipa waendelee mbele.
naongea mambo haya nikitizama sana kwa kina kuwa mimi mtoto wangu akasomee nini maana sasa kuna haja ya kuangalia degrees ambazo zitamfundisha mtoto uhalifu. hata akipata PHD yake au akiwa profesa MUONGO wala haitakuwa shida ili mardi tu afuzu vizur katika kufanya uhalifu halali katika nchi hii. sasa wewe kwa upeo wako mdogo uanataka kufananisha uhalifu huu na uhalifu wa kuku na simu? utakufa. utafungwa miaka mingi sana kwa kumsumbua hakimu na askari.
kama unataka kufanya uhalifu fanya uhalifu wa maana sana huo haufungwi na hata kama watu watapiga sana kelele basi utapewa mapumziko kidogo ili ukale pesa yako kwa amani. kwani uongo? nani kafungwa kweli kweli katika kesi nilizotaja hapo juu? accha hizi sarakasi za bungeni na kwenye media.ukweli unabaki kuwa wahalifu wakubwa wana kinga kubwa sana kikatiba kuliko hawa wadokozi tu ambao huwa wanatolewa sadaka mara nyingi na Hata Mkuu wa Polisi naye anapata nafasi ya kuonekana kwenye TV amekamata watu wana BINDUKI na mapanga. hawa wameua watu wachache sana ukilinganisha na wale ambao wamefanya ufisadi kwenye ESCROW,IPTL,TEMBO,TWIGA,MADAWA YA KULEVYA,MIGODI HIYO YA MEREMETA na myenzake, nk. au hujui kuwa kama hawa waheshimiwa kwa kufisadi mamilioni ya pesa wamesababisha mama,baba,dada,kaka,bibi,babu,mjomba,shangazi,shemeji,mtoto,mdogo,ndugu,jiran na jamaa zako wafe kwa kukosa dawa? kukosa matibabu?kukosa kinga?
hujui hilo. unakaa hapa kulalamika kuwa kuna watoto wa mbwa mwitu na panya road ni hatari unasahau watu kama akina chenga,seti,pindwa,welema,yona,muongo n.k ?
mtoto wangu anasema akikua anataka asome ili naye awe kama profesa MUONGO....nikakosa la kumjibu maana naye ameshuhudia ya kushuhudia.anasema atakuwa anawapiga watu chenga tu kwenye siasa za ulaji siku zote na kuwafunga kwa magoli mengi mengi....
KAMA UNASEMA UHALIFU HAULIPI NENDA KAWAULIZE WALIOKULA PESA ZA ESCROW USIKIE WATAKUJIBU NINI.
 

harakat

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
2,896
2,000
Ni kweli unachosema mtoa mada hawa ni zaidi ya majambazi wa silaha ila watanzania wangapi tunaoliona hili ndio shida
 

Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
6,181
2,000
Mkuu itategemea mwanao atakapo kua mkubwa chama gani kitakua madarakani, kama ni ccm hi sidhani pia kama atafanikiwa cause sasa hv huoni wanavyo rithishana? kama ni chama cha upinzani basi mwanao atafanikiwa tu kama nacho kitadumu madarakani for 20 years, kama vitakua vinabadirika badirika hiyo ndoto kwa mwanao haitakua mkuu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom