Uhalali wa uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga uliofanywa na Rais

Matojo Cosatta

JF-Expert Member
Jul 28, 2017
234
390
UHALALI WA UTEUZI WA MAKAMU MWENYEKITI WA BODI YA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA ULIOFANYWA NA RAIS.

1. SWALI
Mwana JF anayetumia Username ya Hand Hand aliuliza swali hapa JF kuhuu uhalali wa kisheria wa Uteuzi uliofanywa na Rais Samia wa kumteua Bi Mtumwa Khatibu Ameir kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA). Swali la Hand lilijikita katika fact kwamba Bi. Mtumwa ni Mzanzibari na je kwa hadhi hiyo ya Uzanzibar je anaweza kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ambayo inajihusisha na maswala ambayo sio ya Muungano? Mtizamo wa Hand ni kuwa Mamlaka ya Anga ya Tanzania iko chini ya Wizara ya Miundo Mbinu na Uchukuzi na ana mashaka kama Wizara hii inajihusisha na mambo ya Muungano

2. JIBU
(a) Mambo ya Usafiri wa Anga na Usafirishaji wa Anga ni mambo ya Muungano yapo kwenye orodha ya mambo 22 ya Muungano kwa mujibu wa Ibara ya 4 (3) ya Katiba ikisomeka kwa pamoja na Aya ya 11 na 17 ya Nyongeza ya Kwanza (First Schedule). Hivyo, kuna uwezekano kuwa Wizara ikawa inajihusisha na baadhi ya mambo ya Muungano na baadhi ya mambo ambayo sio ya Muungano. Soma Katiba (Swahili version) Toleo la 2005 soma ukurasa wa 15 utaona Ibara ya 4 (3) ya Katiba na muhimu sana soma ukurasa wa 128 kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano hususani soma Orodha Na. 11 na Orodha Na. 17 ambazo ziko kwenye Nyongeza ya Kwanza (First Schedule) ya Katiba .

(b) Hakuna masharti yoyote ya Katiba au sheria ya Jamhuri ya Muungano ambayo yanamzuia Mzanzibar yoyote kuwa Waziri, mkuu wa taasisi, mtendaji mkuu au mtumishi wa umma katika wizara, taasisi au idara ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inajihusisha na mambo ya Tanzania Bara ambayo sio ya mambo ya Muungano (Non-Union Matters). Ni halali kikatiba na kisheria kwa Mzanzibar kuteuliwa kushika madaraka katika izara, taasisi au idara ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inajihusisha na mambo ya Tanzania Bara ambayo sio ya mambo ya Muungano labda mpaka pale sheria itakapo badilishwa.

(c) Hivyo basi, uteuzi wa Rais Samia kumteua Bi Mtumwa Khatibu Ameir kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA) ni halala kisheria.

Imeandikwa na Matojo M. Cosatta.
 
Back
Top Bottom