Uhalali wa plate namba za magari

Brodre

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
2,351
1,372
Nilikua navuka kuingia upande wa kigamboni leo nikakutana na gari kama 4 hivi zina plate namba za kijani kuonesha ni za wafanyakazi wa east african community na nyingine ilikua ni DFP.

Cha ajabu zilikua zinaendesha na wachina pamoja na wazungu tupu kulikua hakuna mbongo huko afu inaonekana kama walikua wanatoka beach kulingana na mavazi waliyokua wamevaa. Je ni halali kwa hizo gari kutumika hivo?

Kwanini wawepo wazungu na wachina ilihali gari zinaonekana ni za jumuiya ya africa mashariki au mimi ndo sifahamu nijuzeni tafadhali
 
aseeeeeee mkuuu hapa unashangaa nini ??? Huku rombo kuna gari za serekali zinatumika kubeba makreti ya bia na majani ya ngombe
 
aseeeeeee mkuuu hapa unashangaa nini ??? Huku rombo kuna gari za serekali zinatumika kubeba makreti ya bia na majani ya ngombe

Dah na hapa zinawekewa mafuta kwa kutumia kodi za wananchi
 
Mbona magari ya jwtz unaweza kuta yanaendeshwa na wachina,wazungu? Hapo hakuna shida,hata niishipo kuna magari manne ya DFP yote yanaendeshwa na wazungu
 
Hapa ndipo Serikali yaenda chaka sasa si ndo mengine unakuta kabisa yanavusha vitu ambavyo havielezeki kisa eti yana namba za serikali kwa stahili hii tutaelekea wapi? Mi nahc kuna ulazima wa Trafiki kuanza kusimamisha haya magari na kukagia documentation maana nahic mengine namba ni feki
 
cio namba zote za kijani ni za East Africa. Zingine ni za Ubalozi kama cjakosea mkuu
 
mimi nina kamshangao kidogo wadau, hizi alphabet on license plate zinasogea kweli na tumeshifikia kama sio kupita herufi "CCM" na "CCJ" ila napata mshangao kidogo.

na kuzurura kwangu kooote kama messenger Dar na mikoani nimefanikiwa kukutana na gari1 aina Toyota Verosa ndio ina herufi za CCM. Kwa hiyo ya CCJ nimekutana nazo mbili, moja ni Land Cruiser VX v8 nyeusii na tinted nyeusiii na ya pili yake nimepishana nayo leo kinondoni Toyota Rav4 short chasis nyeusiii na tinted nyeusiiii.

hivi kuna uhusiano wowote hapa au mawenge yangu tu?

**Naosha kinywa tu wadau, sijaandika kimtazamo wa kisiasa.!
 
Hata pickning zinatumika tu

IMG_0438.JPG
 
Kuna STK moja niliona imapeakia ndama na mbuzi inapeleka shamba (pick up). Yaani Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote!! Nchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana!! Nilalapo nakuota wewe niamkapo ni heri mama weeeeeeeeeeeeeeeeeeee.. Tanzania Tanzania........................ Shamba la bibi hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee ...wajukuu mnakula matunda na miwa bibi hagombezi mjukuu ng'ooooooooooooooooooooooooooooo.
 
Nilikua navuka kuingia upande wa kigamboni leo nikakutana na gari kama 4 hivi zina plate namba za kijani kuonesha ni za wafanyakazi wa east african community na nyingine ilikua ni DFP. Cha ajabu zilikua zinaendesha na wachina pamoja na wazungu tupu kulikua hakuna mbongo huko afu inaonekana kama walikua wanatoka beach kulingana na mavazi waliyokua wamevaa. je ni halali kwa hizo gari kutumika hivo? kwanini wawepo wazungu na wachina ilihali gari zinaonekana ni za jumuiya ya africa mashariki au mimi ndo sifahamu nijuzeni tafadhali
Plate Number za Kijani zinakuwa kwenye magari ya Kibalozi na zile Plate Number nyeupe maandishi yake ni DFP zinakuwa kwenye magari yaliyotolewa Serikali kwa ajiri ya Miradi inayofadhiliwa na Wahisani kutoka nje, kwahiyo.....inawezekana wana haki kuyatumia hivyo.
 
Asante kwa kunielewesha mkuu
 
Nalo hilo la kushangaa? Ebu pitia sredi ya only in tz ndio utazimia kabisa!! Ukistaajabu ya mamvi utayaona ya jahcarhire.
 
kimsingi binafsi nimewahi kukutana na STK ina mzungu! Nilishangaa sana!
lakini pia nyingine zinakuwa zimeuzwa na walionunua wanakuwa hawajafanya transfer ya umiliki (Hisia zangu tu)!
 
Naombeni ufafanuzi wadau katika namba za magari hizi zinamaanisha nini?
DFP
STJ
STK
STL
ST inafuata namba lisha A
 
Back
Top Bottom